Je, Uongozi huu unalinda usalama kwa ajira/uwekezaji/biashara/haki zako?,2020 piga kura kwa maono?

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
6,063
2,000
Je uongozi huu unalinda haki zako za kikatiba?2020 utapigia kura serikali ambayo ukipost neno mitandaoni kuikosoa inakukamata?uko tayari kupigia kura kifungo chako cha jela ambacho kitakutenga na familia yako?uko tayari kuipigia kura serikali ambaye imekataa wewe mwananchi usisikilize bunge lako na mbunge wako?uko tayari kuipigia kura serikali ambayo imekataa kuteua jaji mkuu kwa karibu mwaka ?uko tayari kuipigia kura serikali inayominya Uhuru wa habari?

Tafakari sana kabla hujapiga kura yako,you might be next,vita haina macho,chagua serikali itakayokuheshimu na kukuthamini utu na haki zako,usifate mkumbo,kura yako ni muhimu

Je uongozi huu unalinda ajira yako?uko tayari upigie kura watu ambao watafukuza kazi watanzania 10,000 kwa mpigo? Je 2020 ukiwapigia kura,INA uhakika utakuwa salama au ndio itakuwa umesaini hati ya kufukuzwa kazi? Je utapiga kura CCM ili ufukuzwe kazi jukwaani na kudhalilishwa?je utapigia kura ccm ili unyimwe ongezeko la mshahara bila sababu? Je 2020 utapiga kura ccm ili wakuu wa wilaya na mikoa wakushambulie mbele ya jamii?

Ewe mfanyakazi,itafakari kwa umakini kura yako ya 2020

Je uongozi huu unalinda biashara na uwekezaji wako? Je serikali inajali uchumi wako au inakubeza na kufurahia unapoanguka kibiashara?Serikali isiyovutia uwekezaji wa matrilioni kwa kigezo eti wakisafiri watatumia milioni 100,kwa hiyo bora wasiende kuvutia uwekezaji wa trilioni moja ili waokoe milioni mia kama gharama za safari

Kijana,umeona Sera yoyote inayoakisi ndoto zako? Mkuu wetu umeshasikia akiongea na vijana na kuwasikiliza ndoto zao?anajua kwamba una shida ya ajira?kama anajua kwa nini anakuimbia wimbo wa uhakiki?hajui una majukumu na inahitaji kujitegemea? Kwa nini hakujali?ukimpa kura 2020 unadhani atabadilika?

Kijana,usizame kwenye ushabiki,kura ina maana sana,tena kubwa,ona kura yako ilivyokugharimu,miaka inafika mitatu uliowapa kura wamegoma kukuajiri,unadhani 2020 ukiwapa kura watabadilika?

Kijana itafakari sana kura yako

Mkulima,bendera ya chama chetu ina alama ya jembe na nyundo,jembe kuwakilisha wakulima,ulishamuona mkuu wetu akihudhuria sherehe za nane nane?walau kukupa matumaini? Unajua bajeti ya pembejeo imeshuka sana na walioishusha ni hawa na hawa uliwapa kura wewe?

Mkulima, unajua mbaazi inauzwa kilo Tsh 200 kutoka Tsh 2000? Wakulima wa Tabora na mpanda tumbaku imewadodea wakati majuzi tu ilikuwa ni Dhahabu?

Je wewe mmiliki wa jengo,unaona wenzako wanavyobomolewa?unadhani wewe uko salama? Kura yako ndiye kinga yako na jengo lako na watoto na mkeo,wenzako sasa wanalala nje,Nyumba zao zimebomolewa bila fidia,unadhani 2020 ukishapiga kura ukawapa,wataacha kubomoa?

Ntaendelea......napumzika kwanza sasa
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,426
2,000
WAPINZANI achananeni na AGENDA za BUNGE LIVE, KATIBA, DEMOKRASIA, UHURU WA KUONGEA mtaendelea kuburuzwa MIAKA 2000!

- Hivi mtu ana WIKI NZIMA hajala unaenda kumwambia BUNGE LIVE atakuelewa, au UHURU WA MAONI ??

- Zungumzeni AGENDA za WANANCHI WANAOTESEKA :

- AJIRA
- MAJI
- SHULE
- KODI
- MIKOPO MIDOGO MIDOGO
- MATIBABU
- ARDHI
- MIUNDOMBINU
- BEI YA MAZAO
- UNYANYASAJI ( KWENYE AJIRA )
- HAKI ZA WATUMISHI

Mnatumia muda mwingi kupigania mambo yenu halafu mnalazimisha watu wasiojua hata WATALALA wapi WAWAUNGE MKONO. Zindukeni !
 
Kweli kabisa mkuu
 
Kasongo

JF-Expert Member
Jul 29, 2007
3,048

Umeandika pointi nzuri sana.Na kwa serikali pia ikisema inapigania wanyonge,wanyonge lazima wakione hicho wanachopiganiwa hapo itapendeza sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
2,000
2020 tutapiga kura kuondokana na "watu wasiojulikana" ambao wamelisumbua taifa kwa muda sasa
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,426
2,000
Umeandika pointi nzuri sana.Na kwa serikali pia ikisema inapigania wanyonge,wanyonge lazima wakione hicho wanachopiganiwa hapo itapendeza sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena serikali ya Magufuli imetelekeza kundi kubwa la WANYONGE ambao wanaumia kweli kweli ila wamekoswa msemaji

- VIJANA ( Tangu 2015 mpaka leo 2017 ) haijatoa AJIRA watu WANATESEKA balaa na hawana msemaji

- MACHINGA wanaburuzwa kila siku na serikali imepanga tena kuwatwisha mzigo wa kulipia Tsh 10,000 kwa mwezi

- Kina mama hawana matumaini kabisa ( Wanategemea sana Mikopo midogo midogo na Biashara ndogo ndogo ) lakini serikali imewatelekeza kabisa

- Wanavyuo ndio kabisa hawana hamu na utawala huu ( Mfumo wa mikopo umekuwa mgumu na unapata kwa Tochi )

- Bei za mazao hazieleweki kabisa

IN SHORT HAKUNA JAMBO KUBWA NA LA MAANA SERIKALI IMEFANYA KUBORESHA MAISHA YA WATU. Watu WAMEFUKUZWA KAZI, WENGINE WAMEPUNGUZWA KAZINI.
 
Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
8,869
2,000
Duhhh!! itategemea nani atasimama upinzani, kama ni haohao akina Ngombale mwiru, Sumaye na lowassa, sitawapa kura upinzani aisee maana bora akabaki Magufuli ila siyo kumpa nchi Sumaye na Ngombale Mwiru.

Tatizo la upinzani ni kuwa:-
1. mnayoyahubiri si matendo yenu
2. Hamna mbadala halisi wa rasilimali watu, mfano unamweka Sumaye kuwania urais dhidi ya Magufuli lazima mshindwe, mimi binafsi nawapenda sana wapinzani ila huwa nawapinga sana wakianza kulazimisha niamini 1 kuwa ni 8.

Ngw'ana Kabula
 
Hahaaa,ng'wana kabula
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom