Je ungependa mbunge wako awe mbunge jimbo au mbunge maslahi ya taifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ungependa mbunge wako awe mbunge jimbo au mbunge maslahi ya taifa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jatropha, Nov 29, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Kifungu cha 63 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinaanisha wazi majukumu ya Mbunge kuwa "Kuisimamia na Kuishauri Serikali". Maana yake ni kuwa haiwezekani watanzania wote tukaende bungeni kuismiamia serikali.

  Hivyo kila jimbo hutoa mwakilishi mmoja ili kwenda kuisimamia serikali
  katika ukusanyaji wa mapato wa serikali ili fedha nyingi zaidi ziweze kupatikana kutoka vyanzo mbali mbali
  kama vile kodi za iana mbali mbali, raslimali, madini, utalii, biashara n.k;na kutunzwa vyema. Na pia mwakilishi huyo wa wananchi wa jimbo aweze kuisimamia serikali katika matumizi ili fedha nyingi zaidi ziweze kuelekezwa katika miradi ya maendeleo yenye tija kwa wananchi badala ya hali ilivyo sasa ambapo kiwango kikubwa cha fedha zinazokusanywa na serikali hutumika kugharimia mishahara, posho, safari, warsha, semina, mikutano na gharama zingine za uendshaji zisizo za lazima kama vile serikali kununua magari makubwa na mengi sana ya kifahari n.k. Hii inatokana na serikali ya Tanzania kukosa kusimamiwa na wawakilishi wa wananchi baada ya wawakilishi wetu (wabunge) kugeuka ni wabunge majimbo yaani wasaka maendeleo ya majimbo badala ya wabunge Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye dhamana ya kuisiamamia serikali.

  Ili Mbunge mwenye jukumu la kuisimamia serikali aweze "kuisimamia na kuishauri serikali" ni lazima awe mtafiti na mfuatiliaji ili aweze kuja bungeni akiwa na taarifa sahihi na zilizotafitiwa vyema. Shughuli hiyo ni lazima itatumia muda mwingi wa Mbunge kuliko anavyoweza kushughulikia masuala ya jimbo lake pekee.

  Kwa ilivyo sasa ndani ya Bunge letuili Mbunge aweze kupata miradi mbali mbali ya maendeleo kwa jimbo lake ni lazima ajikombe na kujibembeleza kwa mawaziri wa serikali ambayo anatakiwa kuwasimamia katika ukusanyaji na matumizi ya fedha. Hali inayodhoofisha dhana nzima ya wabunge kuwa wawakilishi wa wananchi wenye dhamana ya kuisimamia serikali.

  Athari za kuwa na wabunge majimbo yaani wale wanaojishughulisha na kutafuta maendeleo ya majimbo yao pekee na sio maendeleo ya kitaifa ni kuiacha serikali bila usimamizi hivyo viongozi na watendaji wa serikali kujifanyia wapendavyo katika ukusanyaji na matumizi ya fedha za serikali; matokeo yake ni nchi na wananchi wake kuendelea kugubikwa katika lindi la umaskini katika nchi ya maziwa na asali hata baada ya miaka 50 kutokea tupate uhuru.

  Serikali kukosa kusimamiwa kushamirisha ufisadi baada ya viongozi na watendaji wa serikali kutumia nyadhifa zao kujinufaisha hivyo kuhujumu mapato ya serikali; na fedha kidogo zilizokusanywa kufujwa bila kuwaletea wananchi maendeleo yaliyokusudiwa mifano halisi ya hali hiyo ni miradi sub-standard iliyotapakaa nchi nzima na kuwakosesha wananchi huduma zilizotarajiwa. Baada kufisadi mapato na na fedha za serikali wabunge majimbo wanaojikomba kwa viongozi na watendaji wa serikali mafisadi humegewa fedha kidogo kati ya nyingi zilizoibiwa kutoka serikalini kwa ajili ya kupeleka miradi kiduchu ya maendeleo katika majimbo yao ili waweze kuchaguliwa tena ili waendeleze kuunga mkono ufisadi ndani ya chombo cha wananchi cha kuismiama serikali.

  Je wewe mwana JF ungependa Mbunge wako awe ni Mbunge Jimbo au Mbunge Taifa?
   
 2. minda

  minda JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  miongoni mwa maneno yaliyotumika katika kuwafitini baadhi ya wabungu wa bunge lililopita ni hilo la 'wabunge wa taifa badala ya wabunge wa jimbo' ( cf. zyansiku kuhusu bashe vs selelii).


  baadhi ya wabunge akiwepo selelii walituhumiwa kuwa wabunge wa taifa badala ya jimbo kwa kutekeleza wajibu huo wa kuisimamia na kuishauri serikali; matokeo yake wakadondoshwa.


  ni wazi wabunge wanatakiwa kuisimamia na kuishauri serikali bungeni na wakati huo huo kuwakilisha wananchi wa majimbo yao.

  baadhi ya wabunge kama akina mhe lowassa, aziz nk walikuwa wakimya muda mwingi bungeni lakini waliwakilisha wananchi wao na kushiriki katika kutatua matatizo yao kiasi kwamba walionekana mashujaa ambapo walioichachafya serikali kama akina selelii, malecela, shelukindo (Me) waliishia kukejeliwa kwa kuitwa wabunge wa taifa kisha kufuatiwa na kuangushwa kwao kwenye kura za maoni.
   
 3. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mimi nafikiri kuna watu wamekuwa wanafanya kazi za kitaifa akiwa kama mbunge, kuna Dr. Slaa, Arfi, Ndesamburo, Zito Mdee lakini ishue ya msingi ni kuwapa wananchi feedback maana kinachowaangusha wengi kujiita mpambanaji then unaishia bungeni ili kujipanga kwa nafasi za juu, fanya kila kitu kwa maslahi ya wananchi, CCM hawataweza kukutoa mbona Slaa wameshindwa kumn'goa toka 1995 hadi alipopendekezwa na chama chake kugombea urais na bado jimbo na halmashauri iko upinzani.
   
 4. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mbunge anamuwakilisha mwananchi wa Jimbo lake bungeni (hii ni kutumikia jimbo)
  Pia Mbunge anashiriki kutunga sheria za nchi (hii ni maslahi ya Taifa)
  Pamoja na hayo kufichua ufisadi wowote pia ni kazi ya Mbunge, hivyo hakuna cha mbunge wa Taifa wala Mbunge wa jimbo!!!!
   
 5. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Si rahisi kulitetea jimbo lako kipekee pekee tu,mfano linapokuja swala la kilimo kwenye utoaji pembejeo na ruzuku sera inakuwa ya kitaifa halafu mgawanyo wa majimbo unafuata.Hapo mbunge atakuwa na wajibu wa kuchangia mjadala kitaifa na pia kutetea jimbo lake kwa kueleza kwa nini yeye apewe umuhimu zaidi pale ambapo rasilimali zilizopo hazitoshi wote kupewa lakini.Hivyo mbunge kama katiba inavyosema ni sahihi kabisa kwani anawatumikia wananchi wake na taifa kwa wakati huo huo.Kupigania jimbo peke yake ni pale shida iliyoko jimboni kwake inakuwa ya kipekee sana mfano madhara ya maafa nk.
   
Loading...