Je, unazijua tofauti za kijinsia baina ya mwanaume na mwanamke?, Nini athari za tofauti hizi?

venchwa

JF-Expert Member
Aug 5, 2016
1,677
1,592
Je wa kwako yuko hivi?

1. Ubongo - mwanamke anaubongo uliounganika (more connected) kuliko mwanaume. Hii inamfanya mwanamke kuweza kufanya mengi wakati mmoja kuliko mwanaume

2. Mawasiliano - Mwanamke anapenda na anaweza kuwasiliana na kutoa taarifa mapema na kwa urahisi zaidi kuliko mwanaume. Ugumu wa kuwasiliana kwa wanaume ni ishu ya kimaumbile zaidi ya kitabia

3. Hisia - Mwanamke anahisia kali na halisi kuliko mwanaume. Mwanamke akikuhisi kitu basi ujue anazaidi ya asilimia 75 yuko karibu na ukweli tofauti na mwanaume. Mwanamke anaweza kuhisi au kuona mambo kabla hayajatokea kupitia vitu kama vile ndoto, maono, hisia kali, mshtuko nk.

4. Kwenye kuuliza maswali - Mwanamke anauliza wakati ndani yake anajua au anahisi ukweli wa jibu na maranyingine anauliza kupata uhakika kwahiyo unapomdanganya inampashida maana tayari anauhakika na alichokihisi tofauti na mwanaume ambaye akiuliza unakuta anataka tu taarifa.

5. Tendo la ndoa - Mwanaume anakiu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa mara kwa mara tena hata akiwa na hasira tofauti na mwanamke ambaye hata akiwa amehemshwa tayari kwa tendo, akiumizwa kidogo hisia au moyo wake basi hamu yote kushnei.

6. Manunuzi - Mwanamke anafurahia manunuzi (shopping) kuliko anavyofurahia chakula na anawezakwenda shopping kuangalia tu wakati hana hela wakati mwanaume manunuzi ni jukumu tena asilolifurahia sana na akinunua kitu basi ni kile alichokipanga, mwanamke yeye anaweza kupanga kwenda kununua mapazia na akirudi anarudi na kapeti, kwake hiyo ni sawa tu. Zipo tofauti tele baina yetu na usipozijua vema mahusiano yatakusumbua. Ungana nami PM madada njoo na namba zenu
 
Ukweli wa story hizi ni pale utakapo ziamini,kinyume na hivyo ni vitu ambavyo havinaga uhalisia kabisa.
 
hapo ninayiamini ni hyo namba tano (5) tuuuu,namba 1 am not sure ntachunguza,na uzi umekosa mfano katka hili.namba 2 siamini hyo ,nayo haina mfano labda ningeelewa.namba 3,imeongelewa tofauti na nilivyotarajia nikajua hisia kama vle hasira,majonzi nk,hisia za kuhisi vitu na vikawa kweli hiyo imekaa kiimani zaidi.4&5 ni za kitabia na sio kimaumbile.
 
Na ikitokea mwanaume anayafanya ulioeleza ni ya mwanamke na mwanamke anayafanya ya mwanamme, watachukuliwa aje hao?
 
Nimeikopi sehem, hizi ndo tofauti

1. Ubongo - mwanamke anaubongo uliounganika (more connected) kuliko mwanaume. Hii inamfanya mwanamke kuweza kufanya mengi wakati mmoja kuliko mwanaume

2. Mawasiliano - Mwanamke anapenda na anaweza kuwasiliana na kutoa taarifa mapema na kwa urahisi zaidi kuliko mwanaume. Ugumu wa kuwasiliana kwa wanaume ni ishu ya kimaumbile zaidi ya kitabia

3. Hisia - Mwanamke anahisia kali na halisi kuliko mwanaume. Mwanamke akikuhisi kitu basi ujue anazaidi ya asilimia 75 yuko karibu na ukweli tofauti na mwanaume. Mwanamke anaweza kuhisi au kuona mambo kabla hayajatokea kupitia vitu kama vile ndoto, maono, hisia kali, mshtuko nk.

4. Kwenye kuuliza maswali - Mwanamke anauliza wakati ndani yake anajua au anahisi ukweli wa jibu na maranyingine anauliza kupata uhakika kwahiyo unapomdanganya inampashida maana tayari anauhakika na alichokihisi tofauti na mwanaume ambaye akiuliza unakuta anataka tu taarifa.

5. Tendo la ndoa - Mwanaume anakiu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa mara kwa mara tena hata akiwa na hasira tofauti na mwanamke ambaye hata akiwa amehemshwa tayari kwa tendo, akiumizwa kidogo hisia au moyo wake basi hamu yote kushnei.

6. Manunuzi - Mwanamke anafurahia manunuzi (shopping) kuliko anavyofurahia chakula na anawezakwenda shopping kuangalia tu wakati hana hela wakati mwanaume manunuzi ni jukumu tena asilolifurahia sana na akinunua kitu basi ni kile alichokipanga, mwanamke yeye anaweza kupanga kwenda kununua mapazia na akirudi anarudi na kapeti, kwake hiyo ni sawa tu. Zipo tofauti tele baina yetu na usipozijua vema mahusiano yatakusumbua. Ungana nami katika Leo Tena ya Clouds fm saa 5.40 asb nikuchambulie hivi vitu kwa kina #ChrisMauki
Huu ni ukweli kabisa, na badala ya kuukana ukweli huu ni vema jinsia zote zikaelewa mambo ya jinsia nyingine kwa itasaidia kuishi kwa amani zaidi.
 
Dah..hapo sijaiona tofauti ya msingi kabisa..iliyowapa hayo majina yao ....au siyo muhimu??:cool:
 
Back
Top Bottom