Je, unaziamini taarifa za jeshi la polisi juu ya majambazi sugu na silaha zao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, unaziamini taarifa za jeshi la polisi juu ya majambazi sugu na silaha zao?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Apr 27, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Wapendwa wanajamvi ningependa tujadili mada hii kama inavyosomeka katika kichwa chake. Awali ya yote ni mara nyingi jeshi lapolisi limekuwa na kawaida ya kutangaza mafanikio yake katika kupambana na na wahalifu. Mara kadha, tumeripotiwa na kuoneshwa watu mbali mbali wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi (tena majambazi sugu) na kushuhudishwa silaha zilizokamatwa zikihusishwa na watuhumiwa hao.

  Binafsi nimekuwa nikijihoji hivi taarifa za polisi zina ukweli usiohojika kama ukweli usiohojika wa biblia na Quran? Je, ni nani mwenye kuthibitisha kwamba silaha zinazotangazwa ni kweli zinahusika na ujambazi na uhalifu unaosemwa?

  Hoja zangu zinatokana na ukweli kwamba jeshi la polisi la Tanzania limetuhumiwa mara kadha kwamba lina kawaida ya kubambikia watu kesi, kuanzia za ujambazi hadi mauaji. Watu muhimu na taasisi na asasi kadhaa zimethibitisha haya.

  Aidha, mapema miaka ya 2000 hii kuna kijana, dereva wa daladala, aliwahikamatwa pale Maktaba Bar & Guest House eneo la Mabibo akituhumiwa kuwa ni jambazi. Alipofikishwa katika kituo cha Polisi cha Urafiki akaandikiwa ripoti kwamba kakutwa na silaha yeye ni jambazi sugu. Bahati ilioje kwa kijana huyu, alikuwa na mjomba wake, mwenye cheo katika serikali ya Mapinduzi. Huyu afisa akahoji ujambazi wa kijana wake na silaha hiyo aliyokutwa nayo.

  Mambo yakawamazito kwa ma-CID walioshika kesi hiyo. Alimanusura wafukuzwe kazi. Wakamsihi kijana (dereva) awasaidie kuwatetea. Basi tuhuma zikafutwa kijana akaachiwa huru.

  Na sio shuhuda chache zinazoelezwa kuwahusu polisi na jeshi lao lote. Mathalan, vijana na watu wengi wanaokatwa na polisi kwa tuhuma za uharifu mbali mbali, huwawanaombwa rushwa. Wanaposhindwa kutoa rushwa hutishiwa kubambikizwa kesi za ujambazi wa kutumia silaha.

  Sasa, swali ni je, tuendelee kumwamini afande wetu kila anapotuonesha silaha za majambazi? Wasi wasi ni kwamba jeshi hili linataka kujenga kuaminika kwa lazima wakati wananchi waliowengi wameanza kuhoji utendaji haki wa jeshi hili. Aidha, katika miaka ya hivi karibuni tumeona kwa macho yetu jeshi likifanya shughuli zake kwa maagizo ya wanasiasa wa chama kinachotawala.

  Baraza laa Congress la Marekani mwaka jana, lililitaja Jeshi la Pol.isi la Tanzania kwamba ni miongoni mwa vyombo vya dola vinavyoongoza kuvunja haki za raia na kufanya mauaji yasiyohojiwa na yeyote katika nchi ya Tanzania.

  Kwa hiyo, kwa machache hayo ukiondoa tuhuma za rushwa zinazofanywa na jeshi hilo, itaonekana wazi kwamba sio kila taarifa za jeshi hilo ni za kweli.

  NAOMBA KUWASILISHA!
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sehemu kubwa ya bunduki/silaha zinazoonyeshwa huwa zimechukuliwa/tolewa store/armoury na kuonyeshwa kama exibits za wanaoitwa majambazi kuzidisha uzito tu dhidi ya watuhumiwa. Jeshi la Polisi tz ni zaidi ya ulijuavyo!
   
 3. m

  mwanakidagu JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ewe mtanzania unawaza vema sana.naunga mkono.hoja.watu wema wamekuwa wakiuawa kwa kisingizio cha majambz sugu.na silaha inachukuliwa store na kuwekwa pembeni ya muhuska
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Sipendi hata kuwasikia hawa basodaa!
   
 5. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Mkuu, unanikumbusha kesi ya wale wafanyabiashara wa madi kule mahenge.
   
 6. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Polisisisiemu haipo kwa ajili ya watanzania, bali kwa hao walioko madarakani. Wakumbuke kenya, utawala ukibadirishwa watanywea maji kwenye karai. Vitambi vyote kwisha, tutawanyima hata kazi za ulinzi wa nyumba zetu.
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,135
  Trophy Points: 280
  Usinikumbushe machungu yangu hawa washenzi walishaniweka mahabusu pale urafiki kisa nilikataa kuwapa rushwa
   
 8. M

  Mzee Kabwanga Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Askari polisi wengi hawana maadili leo nenda ktk vyuo vya polisi ndiyo utaelewa kuwa kuna nini .zile pgo sijui kama wanazima au zipo kwenye makabati ya ocs au ocd .
   
 9. O-man

  O-man JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Polisi wa TZ ni polisi wanaotakiwa kuwepo kisheria. Kiutendaji hapa ndipo kwenye matatizo makubwa. Mimi ni mtoto wa 'line' yaani, baba yangu (Mungu amrehemu) alijiunga na jeshi la polisi la ukoloni. Nimekulia humo mpaka nilipohitimu kidato cha 4 mwaka 1972 na mzee alipostaafu. Jeshi wakati ule na sasa ni vitu viwili tofauti. Maafande hawafanyi kazi ipasavyo, wengi wao wanangalia maslahi binafsi na hawafanyi kwa siri. Sasa ku-justify uhalali wa uwepo wao katika jamii ni kutoa taarifa za kusisimua. Vinginevyo hawana cha kuonesha zaidi ya zima moto wanayo itekeleza sasa. MY TAKE: mfumo mzima wa hii force uangaliwe upya kuanzia recruitment, utendaji wa kila siku na mfumo wa uwajibikaji. Kwa sasa jeshi hili linaendeshwa and not a force in itself. Hawataki kukubali lakini ukweli ni kwamba heshima kwa jeshi hili sio imeshuka la hasha, haipo kabisa. Vituo vya polisi vimegeuka vituo vya biashara. Ule msemo "unaingia bure, kutoka na pesa" haukubuniwa ndiyo hali halisi. Jamii nayo inapaswa kulaumiwa kwa upande mwingine kwa kuindeleza hii hali. Wabunge wa nchi hii wana safari ndefu yenye mazingira yasiotabirika.
   
 10. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,982
  Likes Received: 20,377
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi taarifa hizi za jeshi la polisi kuhusu ujambazi huwa zinatia mashaka sana, angalia mauaji ya wanaoitwa majambazi, wengi hupigwa risasi visogoni na wachache sana usoni. Rejea taarifa iliyosisistizwa sana ya wafanyabiashara waliokamatwa Sinza na kuuawa msituni, hawa uliambiwa ni majambazi aratibu wanafuthatari, kumbuka kifo cha Kombe, tulitangaziwa 'jambazi sugu la magari' limeuawa na wale vijana wa arusha waliokamatwa shell!!!!!!!!!!!

  Watendaji wa jeshi kwa sasa taratibu wamefutika kabatini na sasa wanaongozwa na taratibu inayoitwa uonevu na HELA, sakata la mtoto wa Mengi linaweza kuwa ni mfano mzuri namna ambavyo askari wanajipanga kumbambikizia mtu kesi kwa manufaa yao.

  Huo ushahidi wa bunduki na mapanga yenye damu nao huwa unashangaza, tunajua vidhibiti/exhibit wanakuwa navyo vya miaka na miaka na kufanya ubambikaji kuwa rahisi.

  Hili ndilo jeshi letu la polisi linaloamini katika mabavu huku likihubiri sheria bila shuruti
   
 11. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndugu, issue uliyoleta hapa ni ya muhimu sana. Ni ajabu tunaambiwa polisi wameua majambazi kadhaa waliokuwa wanarushiana risasi lkn hukuti hata kioo cha gari ya polisi kilichoharibiwa kwa risasi ya jambazi! Na tukumbuke polisi wanatakiwa kuwa na ujuzi na mbinu za kuwakamata wahalifu na kuwafikisha mahali husika, siyo kuwaua. Haiwezekani waue majambazi watatu na zaidi wakati hakuna ushahidi usio na shaka kuwa usalama wa polisi hao ulikuwa ktk hatari ya kiwango cha mwisho. Ni ajabu kuwa watu wa haki za binadamu na hata bunge lililosheheni magamba wameshindwa kbs kuhoji na kukemea mauaji yanayofanywa na polisi dhidi ya watu wanaoitwa majambazi bila udhibitisho wowote kuwa ni majambazi.
   
 12. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  polisi, zaidi ya mradi wa kufuga nguruwe.
   
 13. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  Niliwahi kushiriki kukamata wavuta unga usiku mmoja katika lindo la sungusungu. Siku hiyo tulikuwa na bahati ya kuwa na polisi wawili mmoja akiwa na smg. Wavuta unga walikuwa kikundi. Tulipotoa amri ya kuwataka kusimama pale walipokuwa, rundo walitokomea bondeni lakini mmoja wapo alikwa kalewa sana alishindwa kukimbia.

  Katika kundi letu alikuwapo mzee mmoja na upanga umenolewa sana. Inaelekea huyu mwenzetu alikuwa na usongo na vibaka. Alimkata ngwara yule zezeta hadi chini. Kuhamaki tayari yule babu kamkata panga kwenye paji la uso yule kijana. Baada ya mahojiano ilikuja kujulikana alikuwa mtoto wa mtu mkubwa sana akiishi Magomeni Mikumi. Sitaji jina kuogopa jarada kufungulia upya. Ni 1992 hapo, wakati wa zile sungusungu za Mrema.

  Kundi zima likawa limeingizwa katika hatia ya jinai sasa, ikiwa pamoja na wale njagu wawili. Maafande wakatupa somo ambalo sijasahau hadi hii leo. Tulitunga stori ya kuaminika sana, tofauti kabisa na lile tukio lilivyokuwa kujiepusha na shari, ikawa hivyo--na kesi ikawa hakuna! Sema tatizo pale lilikuwa mchanganyiko wa raia na polisi ndiyo maana hii stori leo unaipata.

  Wakiwa peke yao inakuwaje!
   
 14. Didia

  Didia JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 721
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Thread hii imenisababisha nilogin japo kwa mida hii sikupenda. Binafsi huwa nina wasiwasi sana na taarifa za Afande KOVA. Mara nyingi anaripoti kukamata majambazi sugu huku hakionyesha siraha. Huwa tunaambiwa uchunguzi unaendelea ili wapelekwe mahakamani na picha huishia hapo. Mbona sijaona vyombo vya habari vinaripoti kuwa majambazi yaliyotolewa taarifa yamefikishwa mahakamani? Nimewahi kuwa na hisia kuwa maranyingine Afande KOVA anatangaza mafanikio hewa
   
 15. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ningeshauri, kama kweli Polisi wana nia njema na wanataka kufanya kazi kitaalam, wangeweka record ya silaha zote zilizo mikononi mwao, hata zile wanazozikamata, ili ikitokea mtu amekamatwa iweze kuangaliwa silaha aliyokamatwa nayo isiwe miongoni ya zile zilizo kwenye milki yao. Hii itasaidia kujua kama kuna baadhi ya polisi wanaoshirikiana na majambazi na kuwakodishia silaha kama inavyodaiwa. Hii itawafichua hata askari wasio na maadili. Lakini kama Polisi hawataki kufanya hivyo, itakuwa ni wazi kwamba wanafanya makusudi ili kuwabambikia watu au ni kwa kulinda biashara yao ya kuzikodisha kwa majambazi
   
Loading...