JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
1: Kifungu cha 31: Polisi au watekelezaji wa sheria wanaweza kutoa amri inayoruhusu kuingia, kupekua, au kutwaa vifaa na mifumo ya kompyuta, na kutwaa data au taarifa zilizohifadhiwa kwenye kompyuta
Wanaweza kufanya hivyo iwapo watajiridhisha kwamba kuna sababu za msingi kuamini kwamba mfumo huo wa kompyuta unaweza kutumika kama sehemu ya ushahidi
2: Kifungu cha 32: Kumtaka mtu anayemiliki data au taarifa zinazohitajika katika uchunguzi wa makosa au uendeshaji wa mashauri ya jinai kuweka wazi taarifa hizo
3: Kifungu cha 34: Kumtaka mtu anayemiliki taarifa au data zinazohitajika kwa ajili ya uchunguzi kuweka wazi, kukusanya, au kurekodi mwenendo wa taarifa au data za mawasiliano ya aina fulani, au kumruhusu na kumsaidia afisa wa utekelezaji sheria kukusanya au kurekodi taarifa hizo.
Taarifa au data hizo ni zile zinazoonesha chanzo, mwisho, njia, na muda wa mawasiliano husika
4: Kifungu cha 35: Polisi wanaweza kutoa amri ya kukusanya, kurekodi, kuruhusu au kusaidia mamlaka sahihi kukusanya au kurekodi data au taarifa yenye maudhui yanayoainisha mawasiliano fulani ikiwemo matumizi ya njia za kiufundi, kitaalam au kiteknolojia
5: Kifungu cha 37: Kinaruhusu polisi kutumia kifaa cha uchunguzi katika kukusanya data au taarifa kwa ruhusa ya mahakama, mwanzoni kwa muda wa siku kumi na nne