Je unayajua haya ya Tanganyika kabla ya uhuru?

jamani hawa walioongoza harakati za uhuru ni vizuri wote wakatajwa na kukumbukwa, mi sioni tatizo. hata historia ya zanzibar inafichaficha baadhi ya wanaharakati wake. but wanasiasa si miungu ni watu na wanaweza kuwa wanafiki. tusikatae kuwa kuna majin ahayatajwi sana ila pia tusibishe kuwa hatuwezi kumtaja kila aliyepigania uhuru, manake orodha yaweza kuwa ndefu kama mlima kilimamnjaro wakitajwa wote. mohamed ana hoja nyingi moja ikiwa vuguvugu lilianzia mikoa ya pwani, hilo nalo si la kubezwa, bali lapaswa kuboreshwa zaidi kuwa kuzingatia na mapambano ya mahsujaa wengine wa nchi yetu kutoka sehemu nyingine mbali na pwani kama akina mkwawa, isike, mirambo, nk

nijuavyo mie TAA ilianzishwa kama chama cha starehe na burudani na baadaye kikabadili malengo yake na kuwa ya kisiasa consequently jina likabadilika nalo kuwa TANU na lilizaliwa lummba, hapo sidhani kama panahitaji ubishi. inawezekana kuwa kujiunga kwa vijana wasomi kama mwalimu nyerere, kuliongeza chachu ya kudai uhuru na kujiamini zaidi. inaonekana hata wazee wetu wale akina sykes na wengine anaowataja mohamed walimwamini mwalimu pia na kumpisha akamate madaraka ndani ya tanu kirahisi. ni jamabo zuri kuaminiana na linaimarisha mshikamano. ila napata shida kuhusu hisia za udini zinaibukia wapi. nionavyo mimi badala ya kufikiri amambo kidinidini, ni bora tukasalia katika hoja ya msingi ya kuwatambua na kuwaenzi mashjaa wetu wote wa uhuru kadiri inavyowezekana

Kwa hakika kama kuna kitu cha kujivunia katika maadiko nyaliyo wahi kuandikwa na TAA basi ni ile memorya TAA Political Subcomitee iliyotayarishwa na mwaka 1950 Na uongozi wa TAA na kusainiwa na viongozi wa TAA hawa wafuatao Abdulwahid Sykes, Sheikh Hassan bin Amir kama mufti wa Tanganyika na Zanzibar, Dr Vedasto kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia na Stephen Mhando. Waraka huu ndio Nyerere alikwenda nao Umoja wa Mataifa mwezi March mwaka 1955. Na kuusoma mbele ya baraza la udhamini. Hiki ndio kitu cha kuringia na kujivunia si katika ya TANU iliyo nyambiluliwa kutoka kwa Nkurumah. Inasemekana hatma iliyoikumba kazi ile ya historia iliyoandikwa na Abdulwahid Sykes kuibiwa pale Makao Makuu ya TANU imeikumba na nyaraka hii muhimu ya kihistoria iliyotayarishwa mwaka 1950 na uongozi wa TAA. Haishangazi leo ukisikia baadhi ya viongozi wakiikashifu TAA wakinadi kwa vinywa vipana na bila ya soni ati TAA hakikuwa chama cha siasa bali kilikuwa chama cha starehe kama usemavyo wewe dada yangu.
 
Mbona hizi kama njozi za Mohammed Said? Tulishajadilia jambo hili humu JF pamoja naye mwenyewe Said mpaka mods wakatuambia mjadala umetosha.
 
Mbona hizi kama njozi za Mohammed Said? Tulishajadilia jambo hili humu JF pamoja naye mwenyewe Said mpaka mods wakatuambia mjadala umetosha.

Nini maana ya njozi? Hizi zi njozi kumbe mods hawataki watu wajue historia ya kweli ya nchi yao? Nilikuwa sifahamu na inaonyesha basi mods hawaipendi histiria ya kweli ya ukombozi wa mtanganyika. Nadhani hata kama mjadala ulishajadiliwa hauwezi kuachwa kuendelea kujadiliwa. Maisha ya mwadam yana ambatana na historia si dhambi kujua historia yako ni jambo la busara mtu kujua atokapo, alipo na anapoenda hali kadhalika si dhambi mtu kujua historia ya taifa lake. Asiejua historia yake ni mtumwa kwenye nchi yake.
 
Tangu lini waislamu waliacha kuwa na ubaguzi na wakristo?

Waislam ndio waliokaribisha mwalimu wakampa madaraka ndani ya chama ambacho majority walikuwa waislam kina Abdulwahid Sykes na Zuberi Mtemvu wangekuwa na ubaguzi sidhani kama leo hii kuna watu wangemjua Nyerere.
 
Back
Top Bottom