Je unayajua haya ya Tanganyika kabla ya uhuru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je unayajua haya ya Tanganyika kabla ya uhuru?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohammed Shossi, Jan 19, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Ndugu zanguni wanaJF naona kuna mjadala mkubwa umeibuka tangu yalivyotekea mauwaji ya Arusha, binafsi sijapendezewa mtu kufa kwenye kadhia ile na kila mmoja anawajibu katika kifo kile kuanzia vyama vya siasa, serikali, mashirika ya dini na ya kiraia. Nimeona niwaleteeni hii habari ili muone kwanini waislamu watoe waraka unaoonekana kama wa uchochezi? Je ni sote tunaojua historia ya Tanganyika? ENDELEA>>>>>[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]

  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]MWALIMU alianza siasa za kudai uhuru wa Tanganyika katika mazingira ya Dar es Salaam akiwa amezungukwa na Uislamu na Waislamu. Kulikuwa na tofauti kubwa kati ya kiongozi huyu na wale aliowaongoza. Siku hizo Mwalimu kijana mdogo wa miaka thelathini. Kivazi chake kilikuwa ni kaptula na soksi za stokingi. Mavazi rasmi ya wasomi wa miaka ya thelathini.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]

  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Katika TAA aliwakuta vijana wenzake. Marehemu Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally, Waziri Dossa Aziz na wengineo. Halikadhalika walikuwepo vijana wengine kama Hamza Kibwana Mwapachu, Steven Mhando na Zuberi Mtemvu. TANU ilipoundwa mwaka 1954 kukawa na baraza la wazee chini ya Sheikh Suileman Takadir. Baraza hili lilijumuisha wazee wengi maarufu wa mjini na Masheikh. Katika hali kama hii ungelidhani kuwa Mwalimu angejihisi yupo ugenini. La hasha, Mwalimu alikaa vyema katika kundi la Waswahili na Masheikh.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Mwalimu siku moja katika kuwakumbuka rafiki zake wa zamani akizungumza na Dossa Aziz na wageni wengine nyumbani kwake Msasani, katika kuelezea kile alichokiita "the TANU spirit" yaani moyo wa upendo wa wana-TANU, alisema kuwa, siku moja wakati wa kudai uhuru alikuwa anatoka nyumbani kwake Magomeni akija Kariakoo kwa miguu kuelekea sokoni kutafuta mahitaji yake, lakini mfukoni alikuwa hana senti moja. Njiani akakutana na Mzee Mshume Kiyate. Alipomuuliza anakwenda wapi, alimfahamisha kuwa anakwenda sokoni lakini hana fedha za kununua chochote. Mzee Mshume aliingiza mkono katika koti lake na akatoa shilingi mia mbili akampa. (Ukitaka kujua thamani ya fedha hizo ikutoshe tu kuwa nyumba ya vyumba sita kujenga Kariakoo ilikuwa inagharimu shilingi mia tano). Kutokana na hali hii Mshume Kiyate aliona itakuwa ni kumtwisha Mwalimu mzigo mzito ikiwa atakuwa anashughulika na kuwatafutia wanawe chakula na wakati huo huo anafanya kazi za TANU. Mzee Mshume akajitolea kuihudumia nyumba ya Mwalimu kwa chakula. Alifanya hivyo hadi uhuru ulipopatikana.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Baada ya uhuru Mwalimu alimwomba Mzee Mshume aache kufanya hivyo lakini alikataa na akamtafadhalisha Mwalimu aendelee kula chakula chake na kile ambacho kinatolewa na serikali kwake yeye kama mkuu wa nchi alimuomba Mwalimu awape wageni wake. Baada ya maasi ya wanajeshi wa KAR tarehe 20 Januari, 1964 kuzimwa na jeshi la Kiingereza, TANU ilifanya mkutano mkubwa sana Jangwani. Mzee Mshume kwa niaba ya wazee wa TANU alipanda jukwaani na kumvisha Mwalimu kilemba kama ishara ya kuunga mkono uongozi wake.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Pengine ni vyema tuangalie mtiririko wa kupigania uhuru wa nchi hii ili tuone mchango wa Mwalimu na tupate kumuenzi:[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1929: TAA yaundwa ikiwa na wajumbe wafuatao:[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1. Kleist Sykes, 2. Mzee bin Sudi, 3. Ibrahim Hamis, 4. Zibe Kidasi, 5. Ali Said Mpima, 6. Suleiman Majisu, 7. Raikes Kusi, 8. Rawson Watts, 9. Cecil Matola.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1950: TAA yawasiliana na KAU; Abdulwahid alikwenda Nairobi kukutana na Jomo Kenyatta ili kujenga mawasiliano na chama cha Kenya African Union (KAU).[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1951: Kuundwa kwa tawi la siasa la TAA; likiwa na wajumbe wafuatao:[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1. Abdulwahid Sykes (Secretary)[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]2. Sheikh Hassan bin Amir[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]3. Hamza Kibwana Mwapachu.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]4. Said Chaurembo[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]5. Dk. Kyaruzi.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]6. John Rupia.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]7. Stephen Mhando[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1951: Kenyatta akutana tena na viongozi wa TAA. Safari hii mkutano huo ulifanyika Arusha. Wajumbe wa TAA walikuwa Abdulwahid Kleist Sykes, Dossa Aziz na Stephen Mhando.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1952: Abdulwahid alichaguliwa kuwa Rais wa TAA.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1952: Mwalimu Nyerere atambulishwa kwa Abdulwahid na Bwana Kasela Bantu. Baada ya utambulisho huo ikawa kila Jumamosi Mwalimu Nyerere akawa anakutana na akina Dossa Azizi, Bw. Ally Sykes, Abdulwahid Sykes, Dustan Omar na Mhando kujadili mustakbali wa nchi ya Tanganyika.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Mikutano hiyo ama ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Dossa Azizi mtaa wa Congo au mtaa wa Stanley nyumbani kwa Abdulwahid.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Alikuwa ni Dossa Azizi ambaye mara nyingi alikuwa akimrudisha Mwalimu Nyerere kwa gari lake Pugu (St. Francis College) baada ya mkutano.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1953: Mwalimu achaguliwa kuwa Rais wa TAA. Wazee waliompa nguvu ya kisiasa Mwalimu mara baada ya kuingia katika TAA/TANU.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mzee Mohammed Jumbe Tambaza, Mshume Kiyate na Mwinjuma Mwinyikambi. Wengine walikuwa Rajab Diwani, Makisi Mbwana, Sheikh Haidar Mwinyimvua na Idd Faiz Mafongo. Aidha walikuwepo Idd Tosiri, Sheikh Mohamed Ramia na Mashado Ramadhani Plantan.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Oktoba 10, 1953 Mwalimu Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia walikutana kujadili namna ya kuibadili TAA kuwa chama kamili cha siasa.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1954: TANU yaanzishwa. Wajumbe wa mkutano uliojadili kuibadili katiba ya TAA kuwa TANU walikuwa Abdulwahid Sykes, Julius Nyerere, Tewa Said Tewa, Dossa Aziz, Ally Sykes, Kasela Bantu, ,
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Abubakar Ilanga na Saadan Abdu Kandoro. Wengine walikuwa S.M. Kitwana, C.O. Milinga, Patrick Kunambi, Gerimano Pacha, Japhet Kirilo na L.M. Makaranga. Walikuwa pia Joseph Kimalando na John Rupia.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Mkutano wa kuizindua rasmi TANU ulihudhuriwa na wajumbe wafuatao: Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia na Mshume Kiyate. Wengine walikuwa Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajab Diwani, Schneider Plantan na Marsha Bilali. Walikuwepo pia Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Idd Faiz Mafongo, Idd Tulio, Denis Phombeah na wengine.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]
  [/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Julius Nyerere alipewa kadi ya TANU Na. 1, kadi Na. 2 ikaenda kwa Ally Sykes na Abdulwahid akachukua kadi ya TANU Na. 3, Dossa Azizi alichukua kadi Na. 4, kadi Na. 5 ikaenda kwa Phombeah. Dome Okochi alipata kadi Na. 6, John Rupia Na. 7, Bibi Titi Mohamed kadi Na. 16 na Idd Tosiri kadi Na. 25.[/SIZE][/FONT]
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,742
  Likes Received: 4,966
  Trophy Points: 280
  ..harakati za kuupinga ukoloni hazikuanzia DSM peke yake.

  ..maeneo mengi tu mikoani walikuwa wameanzisha harakati za namna moja ua nyingine kumpinga mkoloni.

  ..alichoweza kufanya Mwalimu ni kuzipa sura ya UTANGANYIKA na kuleta umoja ktk harakati hizo.

  ..katika harakati za kudai uhuru na Tanu na Mwalimu walipata msaada toka kwa watu mbalimbali hata wale ambao haikutegemewa wangesaidia. sijui kama unafahamu mchango wa Machifu mbalimbali, au shirika la kidini la kikatoliki la Maryknoll.

  ..maandiko ya Mohamed Said yako kuwakweza zaidi watu wa Pwani, na kupuuza mchango wa wananchi wa maeneo mengine ya Tanganyika ktk harakati za uhuru.
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Labda ungetoa mfano wa hizo harakati za mwalimu zilianza lini na je kabla ya hapo hakukuwa na harakati? kwanini historia hasemi kuwa harakati zilianza tangu 1929 ilipoanzishwa TAA?

   
 4. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Na swali la kujiuliza ni
  Je hao wapigania uhuru walipigania uhuru wa watu fulani tu au sehemu fulani tu au walikuwa wanapigania uhuru wa nchi nzima ya Tanganyika?
  Walijitambulisha kama Watanganyika au Watu wa dini fulani au wa sehemu fulani tu?

  Mimi naamini walikuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika. Na watanzania wote tunatakiwa kuwaenzi, wala historia yao haitakiwi kuonekana ni mali ya watu fulani tu.
   
 5. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Vuguvugu la kupigania uhuru lilianza sehemu ya mwambao wa Tanganyika yaani Dar es Salaam, Tanga na Bagamoyo na kusambaa Kigoma na Tabora.... Tabora ni mji muhimu sana kwenye historia ya nchi hii lakini ni sehemu ambayo imesauhaulika katika historia na kimaendeleo....

   
 6. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nia ya kuleta uhuru ilikuwa ni kujitawala kwa watu watanganyika ikumbukwe kuwa waislamu hawakuwa na ubaguzi kwa wakristo.
   
 7. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  una aina fulani ya kutaka kuleta u...........utamalizia mwenyewe, ni tabia za watu wa aina hiyo kulalamika tu mlitaka afanyeje, na kama mlijua si wa.. yenu hamukuwa na watu wenu??? hapo kuna kitu waliowatangulia waawaficha na kuwapeni fikira mbofumbofu
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,742
  Likes Received: 4,966
  Trophy Points: 280
  Mohamed Shossi,

  ..vuguvugu za kudai uhuru zilianza sehemu mbalimbali za Tanganyika.

  ..hao watu wa Pwani unaodai walikuwa mstari wa mbele ktk kudai uhuru toka kwa Muingereza, walikuwa part ya utawala wa kikoloni wa Mjerumani kama maakida na majumbe.

  ..Kiswahili, lugha ambayo iliwaunganisha wananchi wakati wa harakati za uhuru toka kwa Muingereza, infact kilikuwa ndiyo Colonial Official language ya Mjerumani.

  ..ndiyo maana kuna maeneo mengine mikoani kiswahili si lugha inayoheshimiwa.

  ..harakati za uhuru ni more COMPLEX zaidi ya jinsi ambavyo Mohamed Saidi ameelezea ktk vitabu vyake.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Kwani mwalimu alifanya mapinduzi ya kijeshi ili kuongoza mapambano ya uhuru?Kama ni free will ya watu ambao wanadaiwa ndio waasisi wa mapambano hayo, nini kilipelekea kufanya hivyo?
  Nionavyo mimi, uongozi sio wa kupeana kwa kuangalia dini au umaarufu....ni kutokana na uwezo wa mtu. Aliye na masikio na asikie hili.
   
 10. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160

  Mkoa wa Tabora sio pekee uliosahauliwa. Singida unaionaje au kwa vile juzi imepata lami? Mtwara, Lindi, Ruvuma? Vile vyama vya ushirika vya Mbinga ambavyo vilikuwa na vuguvugu la uhuru unavikumbuka?

  Tukirudi Tabora, kama ni suala la madaraka, Samweli Sita amekuwa Waziri kwa muda mrefu sana pamoja na kushika nyadhifa zingine. Kapuya, amekuwa waziri, kwa muda mrefu. Lipumba anatokea kule. Je ni kitu gani kinafanya mkoa usiendelee? Hata akina Fundikira waliwahi kuwa serikalini.

  Ni uhaba wa rasilimali? Uvivu wa watanzania?
  Mimi nafikiri ni mipango mibaya tu ya CCM, na ubaya huo haupo Tabora tu.
  Umewahi kutokea Tabora kwenda Mbeya? ukikatiza wilaya ya chunya (ambayo inachukua nusu ya eneo la mkoa wa mbeya) mpaka utatamani kulia. Na hiyo ni wilaya yenye madini kama ilivyo tabora. Angalia mkoa wa Shinyanga, wapi utasema kuna cha maana pamoja na kuzalisha pamba? vumbi tupu na maji ya shida.
  Njoo Dodoma, ukiondoa pale mjini labda na mpwapwa, wapi kuna nafuu, vumbi tu na umasikini wa kutupwa. Haya Twende Tanga ambako unafikiri hakujasahaulika, umewahi kufika vijiji vya handeni? na Pangani? Kila ukipita ukiwaangalia watu, mpaka unatamani labda wewe mwenyewe uwe Rais ili upunguze umasikini. Kwa hiyo ndugu yangu, ni nchi nzima choka mbaya. In fact hata Dar es salaam kwenyewe, kuna nini cha maana? Mtu unakaa jijini halafu unatumia maji ya kununua kwenye vidumu. Shit! Nchi nzima ni maskini, na tuhahitaji sera mbadala.
   
 11. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Wewe ndio unahuo uusemao na sio hao waliomkaribisha mwalimu na inaonyesha waliokaribisha Mwalimu walikuwa na dhamira ya kuikomboa Tanganyika kutoka kwenye makucha ya wakoloni. Lakani Mwalimu alipata kunena
  Source kitabu kinaitwa Kwaheri ukoloni, kwaheri uhuru kitafute ukisome kipo bure mtandaoni.
   
 12. l

  limited JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  this isn good history of our country for the generation to come lakini kwa sasa watu wameacha kabisa uzalendo vitu kama hivi vilitakiwa viwe kwenye shule zetu za msingi lakini elimu imechakachuliwait is good piece of information kwa generation ya waliozaliwa kuanzia 80s
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mkuu nakubaliana na wewe wote hao wametoka Tabora na kwa kuongezea wakubwa wengi Serikalini wamesoma Tabora boys na girls, lakini Serikali kuu ndio yenye kupeleka maendeleo sehemu zinazohusika na sio kina Lipumba na Kina Samwel Sitta na sina kumbukumbu huyu Samweli Sitta alikuwa Waziri wa nini kwa miaka mingi unayoisema wewe.

  Ila faraja kwa kundi lililokuwa kidete kwenye harakati za ukombozi ni kuwa JK ataiwezesha Bagamoyo kuwa moja ya sehemu ya kibiashara na kuongeza pato la mwanachi wa Bagamoyo.
   
 14. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni kwamba umejadili hoja kidini. Hawa wazee walikuwa hawajioni kama wakala wa dini bali walijiona kama Watanzania. Tanzania haijawahi kuwa ya kidini bali ni watu wachache wanajaribu kuifanya iwe hivyo.
   
 15. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160

  Mawazo yako yakiegemea udini basi kila kitu ukikiona utakichukulia udini, swali linaloulizwa kwanini historia yetu haielezi kilipotoka TANU? inaonyesha CCM inamiaka ya karibia 100 tangu ilipoanzishwa iliwa inaitwa TAA, TANU na sasa CCM. Kwanini harakati za ukombozi hazielezewi kuwa zilianza tangu 1929? huo udini unaujua wewe maana tumeona hapo juu kuna kina John Rupia na [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]Kasela Bantu. Sasa sijui hao ni wa dini gani?
  [/SIZE][/FONT]
   
 16. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Hilo hata wakristo wenyewe wanalijua sana nyoyoni mwao ila wanafanya ukaidi na hila za makusudi ili waislamu ndio waonekane ni wenye udini. Lakini hao ni baadhi tu na kwa hakika hawaitakii mema nchi hii. Na katika hao ni wale walioiita serikali ya kikoloni kuwa ni serikali yao na walikuwa wakiwapinga wapigania uhuru wa Tanzania kwa wakati huo, baada ya uhuru waligeuka na kutafuta kila njia za kuingia serikalini na walifanikiwa na baada ya kufanikiwa kwao walipika majungu na waliowarithi wanayaendeleza kwa kutaka ionekane wao ni wema sana na kumbe ni kinyume chake.
   
 17. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  haha ha ha! Ungelimwambia yale majina ya waislamu ayaondoshe!? Hajajadili hoja kidini bali amewasilisha ujumbe kuwajibu wale ambao upeo wao haujaona mbali na hawataki kuona mbali zaidi ya pale walipooneshwa!
   
 18. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #18
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ndio maana kulikuwa na Paul Rupia na Kasela Bantu, hawa ndio waliosahaulika kwenye historia tukufu na sio waislamu peke yao mfano rupia alijitolea kwa hali na mali kwa ajili ya chama wakati wa harakati za uhuru, baadae mwanzo wa miaka ya 1961 kulikuwa na kina Oscar Kambona historia ya huyu "mkristo" mwanaharakati wa uhuru imefinyangwa pia. Ndugu zetu wakristo tunahitaji historia ya kweli kwa ajili ya vizazi vijavyo hakuna swala la udini hapa.
   
 19. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Paul Rupia na Kasela Bantu ni kina nani kwenye harakati za kudai uhuru unajua vizuri wamehusika vipi? Au hao ni waislamu? msiwe na fikra za kidini kila msomapo jambo muwe mnaweza ku reason out.
   
 20. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  HI NI NZURI, MAANA YAKE NI KWAMBA, NCHI HII HAINA UDINI NA TUSIKUBALI KUWA NA UDINI. KAMA WALE WAZEE WALIMHESHIMU MWALIMU NA KUMPA UONGOZI ILI HALI WAKIWA WANAFAHAMU TOFAUTI ZAO ZA IBADA TO ME MEANS WALIFAHAMU NA KUTAMBUA UWEZO WAKE WA KUONGOZA NA HAWAKUMPENDA MTU KWA DINI YAKE TOFAUTI NA SASA MTU AKISEMA KITU TU WATU MARA MOJA WAMEDAKIA TOFAUTI ZA DINI. UKISEMA SERIKALI SASA NA HASA UKIWA DINI TOFAUTI NA MTAWALA UTAAMBIWA UMESEMA KWA KUWA UNAMPINGA KWA DINI YAKE. WE SHARE COMMON GOAL. MAENDELEO NA KUPINGA WIZI. HAIANGALII DINI WALA CHAMA. MEYA WA ARUSHA NI MKRISTO BUT MAASKOFU HAWAMKUBALI KWA KUWA AMEKUWA Pale KINYUME NA TARATIBU, LAKINI WATU WENGINE NA VIONGOZI WA DINI ZINGINE WANAHISI ANAKATALIWA KWA KUWA MWENYEKITI WA CHAMA KILE NI MUISLAMU KITU AMBACHO KWANGU MIMI SIDHANI KAMA KIKO MAWAZONI MWA HAWA WA UPANDE WA PILI. TUFANYEJE KUWAELEWESHA WANA TANGANYIKA KUWA WE HAVE A COMMON GOAL AMBALO NI KUONDOA WABADHILIFU WA MALI YETU NA SI KUANZA KUINGIZA VITU AMBAVYO HAVINA MSAADA KWETU KAMA NCHI?
   
Loading...