Je, unawezaje kufanya biashara ya Nyumba za Kulala wageni Lodges, Guest Houses ukiwa mbali na Upate faida?

Weka utaratibu wa kumpa commission, mbali na mshahara unaweza kumwambia katika kila 3M utakayoingiza yeye ana laki mbili. Grahams
 
Ni biashara nzuri ila inategemea pia umejenga wapi penye wateja

Asante Mkuu kwa Ushauri wako boss, hilo pia ni muhimu sana kuliangalia.

Huku nilipo ikifika Alhamisi hadi Jumatatu vyumba kwenye Lodge na Guesthouse zote hujaa. Hiki ni kiashiria kwamba hii biashara inalipa kwa maeneo yetu.
 
Mimi nna wazo kama lako ila nachotaka nikikamilisha kila kitu natafuta mzoefu wa hizo kazi nampangisha tunawekeana makubaliano kila baada ya miezi mitatu au sita anaweka mpunga kwenye account namuwekea terms and conditions za kufanya marekebisho madogo madogo na kila mwisho wa mwaka naenda kukagua na kufanya maboresho sehemu iwe na mvuto muda wote.
 
Biashara yoyote ikikosa mhudumu mwaminifu lazima ikufe ... kuna vitu vidogo vidogo vya kumfanya anayesimamia biashara yako aipende na kuiona kuwa yake na wewe kukuletea faida japo wengi wanapenda kuweka mstari wa utofauti kati ya boss na mwajiriwa
Kazi yoyote ile ili aipende mfanya kazi mlipe vizuri.
 
Back
Top Bottom