Je, unawezaje kufanya biashara ya Nyumba za Kulala wageni Lodges, Guest Houses ukiwa mbali na Upate faida?

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
11,049
34,002
Wakuu, habari za muda huu?

Naomba tupeane uzoefu, Je unawezaje kufanya ufuatiliaji wa biashara ya Nyumba ya kulala wageni iwapo utakuwa Mkoa tofauti na ulipofungulia biashara yako?

Nimepata wasiwasi baada ya kuona mmoja wa mtu aliyenihamasisha kuingia kwenye biashara hii nayeye akilalamika kupata hasara na hatimaye Lodge yake kupigwa mnada na Benki aliyokopa kwa kushindwa kufanya marejesho ya mkopo wake.

Ninatamani kwa dhati ya moyo wangu, niingie kwenye hii biashara hasa baada ya kuona inaweza kunilipa mapema gharama nilizotumia kuinvest kuliko nyumba ya kupangisha ambayo nitahitaji kusubiri zaidi ya miaka 15 kurudi.

Naomba tupeane abc wale ambao wamewahi kufanya biashara ya Lodges, Guest Houses. Watu wa Hotels pia mnaweza kunipa mwanga wa nini nifanye kuweza kufanya biashara hii kwa mafanikio.

1626338734948.png

 
Biashara yoyote ikikosa mhudumu mwaminifu lazima ikufe ... kuna vitu vidogo vidogo vya kumfanya anayesimamia biashara yako aipende na kuiona kuwa yake na wewe kukuletea faida japo wengi wanapenda kuweka mstari wa utofauti kati ya boss na mwajiriwa
 
biashara yoyote ikikosa mhudumu mwaminifu lazima ikufe ... kuna vitu vidogo vidogo vya kumfanya anayesimamia biashara yako aipende na kuiona kuwa yake na wewe kukuletea faida japo wengi wanapenda kuweka mstari wa utofauti kati ya boss na mwajiriwa
Asante kwa ushauri wako Boss.

Natakiwa nifanyaje ili Mhudumu aipende kazi yake na aione kama yake wakati huo Mimi napata hela yangu kama kawaida?
 
Asante kwa ushauri wako Boss.

Natakiwa nifanyaje ili Mhudumu aipende kazi yake na aione kama yake wakati huo Mimi napata hela yangu kama kawaida?
Kwa ninavoamini mimi na kitu ambacho kinanisaidia sana ni kuwa karibu na watu wanaokusaidia biashara zako , jenga nae mazoea ya kikazi na urafiki wa hali juu ila hapa kuwa makini na mabinti huwa wanawaza mengineyo ....kumfanya kuwa karibu nae huku mkiwa marafiki na mfanye asijione kama mtumwa wa ajira , kuwa nao karibu sana huku ukiwapa viofa ofa vya mara kwa mara ila kupitia kwenye faida unayopata
 
kwa ninavoamini mimi na kitu ambacho kinanisaidia sana ni kuwa karibu na watu wanaokusaidia biashara zako , jenga nae mazoea ya kikazi na urafiki wa hali juu ila hapa kuwa makini na mabinti huwa wanawaza mengineyo ....kumfanya kuwa karibu nae huku mkiwa marafiki na mfanye asijione kama mtumwa wa ajira , kuwa nao karibu sana huku ukiwapa viofa ofa vya mara kwa mara ila kupitia kwenye faida unayopata
Nimekupata Mkuu hasa "Jenga nae mazoea ya kikazi na urafiki wa hali ya Juu"

Vipi kuhusu kufunga Camera, inaweza kusaidia?
 
Nimekupata Mkuu hasa "Jenga nae mazoea ya kikazi na urafiki wa hali ya Juu"

Vipi kuhusu kufunga Camera, inaweza kusaidia??
Wengi wanaamini kuwa inasaidia ila kwa aina ya biashara mfano wa lodge sikushauri unaweza kufunga na wao wakatumia hicho kgezo kufanya biashara yako ife ..mfano yeye /wao wataamini huwaamini ndo maana umefunga camera na wanaweza kuwafanya wateja wasiwe huru kwa kuwa tunajua matumizi ya logde :D :D :D :D :D mteja anakuja mara moja siku nyingine harudi ....
 
Mlipe vizuri na muonyeshe upendo. Unamuachia asset yako kubwa aisimamie kwanini usimlipe vizuri ili aone unamjali na kumthamini.
Kwahiyo huenda malipo duni yakachangia kwa kiasi kikubwa kuibiwa??

Rafiki yangu anasema alikuwa anamlipa shilingi 250,000 Muhudumu na shilingi 100,000 aliyekuwa anafanya usafi wa Chumba na mashuka
 
wengi wanaamini kuwa inasaidia ila kwa aina ya biashara mfano wa lodge sikushauri unaweza kufunga na wao wakatumia hicho kgezo kufanya biashara yako ife ..mfano yeye /wao wataamini huwaamini ndo maana umefunga camera na wanaweza kuwafanya wateja wasiwe huru kwa kuwa tunajua matumizi ya logde :D :D :D :D :D mteja anakuja mara moja siku nyingine harudi ....
Nimekupata Boss, wasiwasi wangu ukizubaa kidogo muhudumu ananufaika na wewe mwenyemali unakuta unakufa kwa stress za marejesho ya Mkopo
 
Lazima uwe na system inayoweza kufanya monitoring ya kuingia na kutoka kwa wateja, CCTV, milango, check-in/out etc. enzi zangu ningekuandikia proposal kabisa ya mfumo ila vijana wapo humu wanaweza kufanya design na implementation ya mfumo kama huo
 
Sio mtaalamu wa kuelezea sana kuhusiana huo mfumo sijui hata nikuelezeje Ila tafuta kijana wa IT alafu naweza kumwelekeza na akafanaya mkuu
Shukrani Mkuu, nitakutafuta nikifanikiwa kuwasiliana naye kuhusu hili kama atakuwa amebobea humo
 
Back
Top Bottom