Je,unaweza kuwa na Uchumi imara bila Siasa safi? Kipi kianze Siasa au Uchumi

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,762
3,337
Wachambuzi karibuni.
Mwl. Nyerere alisema,ili tuendelee tunahitaji mambo kadhaa,muhimu ikiwa ni Ardhi, Watu ,Uongozi bora na Siasa safi . Hapo kwenye kuendelea,naamini alimaanisha ni pamoja maendeleo ya kiuchumi.
Je kwa hayo yote bado mtizamo wetu ndiyo uleule ?
 
Wachambuzi karibuni.
Mwl. Nyerere alisema,ili tuendelee tunahitaji mambo kadhaa,muhimu ikiwa ni Ardhi, Watu ,Uongozi bora na Siasa safi . Hapo kwenye kuendelea,naamini alimaanisha ni pamoja maendeleo ya kiuchumi.
Je kwa hayo yote bado mtizamo wetu ndiyo uleule .
Uchumi ya raia kuwa na chuki kwa wanayofanyiwa huo uchumi hauna maana. Mku huo uchumi usionekana zaidi kinachoonekana ni vilio vya hali kuzidi kuwa mbaya.
Kwa hiyo ni siasa kwanza
 
Siasa na uchumi ni vitu viwili tofauti sana siasa ni maisha ya kila siku huku uchumi ni mipango ya kila siku na hakuna nchi Duniani liyokosa siasa. Democrasia pekee ndio inatofautisha nchi na nchi lakini unapozungumzia swala ya uchumi unazungumzia mipango ambayo inaitaji watu walio vizuri kichwani sio siasa ambayo hata asiyejua kusoma na kuandika anaweza kufanya
 
Ungefafanua kwanza maana ya Siasa safi ni nini la sivyo utakua unatupotezea muda hapa.
Caroline,sina uhakika kama wakati huo Mwl. Nyerere anaeleza hayo mambo manne ulikuwa tayari shule au bado. Kwani alifafanua kwa kirefu maana ya kila jambo kati ya hayo manne. Siasa safi alisema ni ile siasa inayoruhusu watu kujiamulia mambo yao,kuheshimi utu wa mtu na uhuru wake nk ambayo kwa kipindi kile aliamini ni "siasa ya ujamaa na kujitegemea"
 
Nickname, siasa ndiyo huzaa dira na mfumo wa kiuchumi. Uchumi wa Kenya ni imara kwa sababu kadhaa; mojawapo ni ya kihistoria. Wakoloni walifanya Kenya ndiyo kitovu cha biashara Afrika Mashariki. Pili, tangu uhuru Kenya wamejikita kwenye uchumi wa soko bila kujaribu kitu kingine chochote. Ingawa nasi tumerudi kwenye uchumi wa soko tangu awamu ya 2, hivi karibuni tumeanza kutuma 'mixed signals' kwa wawekezaji.
 
Siasa safi ni nini? au ni ile ya kuruhusu tu watu kujiropokea wanayotaka? ama ni ile ya kuruhusu hata matusi mitandaoni kwa mwamvuli wa uhuru wa kutoa maoni?
Basi kama ndivyo umaanishavyo, hakuna haja ya kuwa na siasa safi.
 
Ndugu,pitia vizuri maana niliyoieleza ya siasa safi kulingana na mawazo ya Mwl. Nyerere na Baba wa Taifa letu. Tuanzie hapo katika kujenga hoja ya thread hii.
 
k
Siasa na uchumi ni vitu viwili tofauti sana siasa ni maisha ya kila siku huku uchumi ni mipango ya kila siku na hakuna nchi Duniani liyokosa siasa. Democrasia pekee ndio inatofautisha nchi na nchi lakini unapozungumzia swala ya uchumi unazungumzia mipango ambayo inaitaji watu walio vizuri kichwani sio siasa ambayo hata asiyejua kusoma na kuandika anaweza kufanya
Kama siasa ni maisha ya kila siku basi na uchumi moja ya maisha ya kila siku maana maisha ya kila siku ni kila kitu
tangu mwanadamu alipoanza kuishi katika makundi yaani social groups ndipo siasa ilipoanza ili kuongoza uchumi na maisha kwa ujumla
kumetokea maendeleo duniani ya siasa, uchumi sayansi na teknolojia. katika siasa ni pamoja na demokrasia na mifumo ya kuitawala.
Kimsingi ni siasa kwanza kisha uchumi, katika haatua ya juu kabisa ya maendeleo hakuna cha kwanza kwa sababu uchumi unapoharibika unaathiri siasa chukua mfano wa mataifa makubwa kama USA huwezi kusema nini kianze. Kwa Afrika tunahitaji sana siasa safi kujenge uchumi imara.
 
Hoja zako kama zina maono fulani mazuri
 
Caroline,sina uhakika kama wakati huo Mwl. Nyerere anaeleza hayo mambo manne ulikuwa tayari shule au bado. Kwani alifafanua kwa kirefu maana ya kila jambo kati ya hayo manne. Siasa safi alisema ni ile siasa inayoruhusu watu kujiamulia mambo yao,kuheshimi utu wa mtu na uhuru wake nk ambayo kwa kipindi kile aliamini ni "siasa ya ujamaa na kujitegemea"
 
k

Kama siasa ni maisha ya kila siku basi na uchumi moja ya maisha ya kila siku maana maisha ya kila siku ni kila kitu
tangu mwanadamu alipoanza kuishi katika makundi yaani social groups ndipo siasa ilipoanza ili kuongoza uchumi na maisha kwa ujumla
kumetokea maendeleo duniani ya siasa, uchumi sayansi na teknolojia. katika siasa ni pamoja na demokrasia na mifumo ya kuitawala.
Kimsingi ni siasa kwanza kisha uchumi, katika haatua ya juu kabisa ya maendeleo hakuna cha kwanza kwa sababu uchumi unapoharibika unaathiri siasa chukua mfano wa mataifa makubwa kama USA huwezi kusema nini kianze. Kwa Afrika tunahitaji sana siasa safi kujenge uchumi imara.
Hoja za msingi
 
Siasa na uchumi ni vitu viwili tofauti sana siasa ni maisha ya kila siku huku uchumi ni mipango ya kila siku na hakuna nchi Duniani liyokosa siasa. Democrasia pekee ndio inatofautisha nchi na nchi lakini unapozungumzia swala ya uchumi unazungumzia mipango ambayo inaitaji watu walio vizuri kichwani sio siasa ambayo hata asiyejua kusoma na kuandika anaweza kufanya
Hata siasa inahitaji weledi na ubobefu wa kitaaluma,usichanganye kujua kusema na menejimenti ya siasa menejiment ni taaluma husomewa ,kusema sana hata asiyesoma.anaweza kusema tu.hivyo siasa sitahiki inahitaji wasomi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom