Je unaweza kumweleza mpenzi wako idadi ya marafiki wa kimapenzi uliowahi kuwa nao kabla yake?

Hakuna kitu cha namna hiyo,labda kama umetoka mtaa mmoja yeye mwenyewe atakuwa anajua huyu jamaa alishapitia fulani na fulani.Tofauti na hiyo hakuna mtu anaweza kutaja idadi ya ex_wake
 
Inawezekana mkuu but ni moja kati ya vitu hatari katika mahusiano..maana inaweza kuleta hisia kuwa ni kicheche sana hivyo ikitokea tatizo jipya bas linaeza unganishwa na hiyo historia so ukaonekana hufai...ukweli kwenye mapenzi sio wa muhimu Ila busara ni muhimu zaidi
 
Mie naona ni vyema ukawa muwazi. Kama kweli umetembea na wapenzi wengu basi atajua kuwa hiyo ni tabia yako. No point in kumficha mtu...weka kila kitu wazi ili that person makes an informed decision.

Kama unaogopa kuonekana kicheche basi u are being accountable for ur own decisions...na mtu wa namna hiyo hafai.
 
Usijaribu hiyo kitu. Unaweza kuja kuulizwa sababu ya kila uhusiano uliovunjika. Utajibu nn? Utaonekana kimeo mapema mno
 
Inawezekana mkuu but ni moja kati ya vitu hatari katika mahusiano..maana inaweza kuleta hisia kuwa ni kicheche sana hivyo ikitokea tatizo jipya bas linaeza unganishwa na hiyo historia so ukaonekana hufai...ukweli kwenye mapenzi sio wa muhimu Ila busara ni muhimu zaidi
Ndo maana wengi huwa wanapunguza idadi kama alitembea nao 40 atakwambia 4
 
Hakuna kitu cha namna hiyo,labda kama umetoka mtaa mmoja yeye mwenyewe atakuwa anajua huyu jamaa alishapitia fulani na fulani.Tofauti na hiyo hakuna mtu anaweza kutaja idadi ya ex_wake
Tatizo linakuja anataka kujuwa hapo unafanyaje sasa.
 
Kumuelezea unaweza ila tu ujue adhari zake nikwamba mapenzi na uaminifu vitapungua kwa kiasi fulani … manake ubongo huweka kumbukumbu na kutafakari kumbukumbu hizi, sasa baada ya tafakari hapo ndio negative effects huja na baadae ndio mtu ataanza kupunguza mapenzi yale ya ndani na baadae atakuwa ana act tu kukupenda na baadae atashindwa …
 
Hilo si la maana sana kama mnaweza eleza idadi ya michepuko iliyochepuka baada ya kuwa pamoja na kwa nn mlichepuka ili kudhibiti hiyo hali ya kuendelea kuchepuka hata kwa wana ndoa
Kama kwa mchepuko unapewa pesa mwambie tu mpenzi mke au mume kuwa mm huwa napenda baada ya shoo nipewe pesa au unafanywa hivi na vile unasema tu mm huwa nachepuka sbb nafanya hivi na vile
 
Nimeshawahi kuwauliza wasichana kadhaa lakini kila mmoja aliniambia mimi ni wa tatu.... hapo nahisi ni ngumu kupewa idadi kamili...
 
Wadau habari za muda,
Kama mada inavyoeleza ni sawa kumweleza mwenza wako idadi ya wapenzi uliowahi kuwa nao
Mkuu kununua Gari Used Ni jambo la kawaida maana ni wachache wanaweza miliki mpya ,ila Kununua Gari iliyotembea kilometa nyingi zaidi na uku unajuwa, Dah apa kunahitaji mioyo ya mashujaa Saba waliokufa vita vya maji

Kwamimi siwezi maana nahisi nnamoyo mdogo maana hata kusukuma Damu tu shida je kujua idadi ya X wake
 
Back
Top Bottom