Je, unaweza kumshtaki mpenzi aliyekuacha baada ya mahusiano ya muda mrefu?

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
376
Habari zenu waungwana?
Niliwahi sikia juu ya sheria kuhusiana na mwanamke ambaye ameishi na mwanaume kwa muda mrefu kimahusiano, kisha mwanaume huyo au mwanamke akamuacha mwenzake baada ya muda mrefu wa kimahusiano.
Je kesi hizi Tanzania zipo vipi na unatumia sheria zipi na unaanzia mahakama ipi.
Ahsanteni sana.
 
Je unaweza kumshtaki ex wako akulipe fidia endapo mmekaa muda mrefu katika mahusiano kisha akaoa mtu mwingine? Sio kuishi pamoja bali kuwa naye kimahusiano kwa mihadi ya ndoa huko mbeleni.
Kuna mkataba mliandikishiana kisheria wa kukaa naye muda mrefu katika mahusiano ili akuoe?
 
Haki ya kudai fidia kwa kuvunjwa ahadi ya kuoa/kuolewa (ndoa (Right to damages for breach of promise of marriage)

Kifungu cha 69 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinatoa haki kwa wapenzi kupeleka shauri mahakamani na kudai fidia kutokana na kuvunjwa ahadi ya ndoa. Suala la msingi kuzingatia ni kwamba, hakuna shauri litakalokubalika kisheria kama mdaawa katika shauri hilo wakati wa ahadi alikua na umri chini ya miaka kumi na nane.

Pia, fidia haziwezi kutolewa zaidi ya hasara ambayo ndio dhahiri kwa upande wa mdai ambayo ilitokana na gharama alizoingia wakati wa ahadi hiyo na mambo mengine kama hayo.

Je, ni muda gani umewekwa kisheria kwa ajili ya kufungua madai ya fidia kutokana na kuvunjwa kwa ahadi ya kuoa/kuolewa (ndoa)?

Kifungu cha 70 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinaweka ukomo wa muda wa kupeleka shauri mahakamani kudai fidia za uvunjifu wa ahadi ya ndoa kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu ahadi hiyo ilipovunjwa.

Zawadi za wachumba (Gifts between engaged couples)

Suala jingine la msingi kuzingatia ni zawadi baina ya wachumba. Katika jambo hili, swali la msingi kabisa kujiuliza ni je, zawadi hio ilitolewa na mchumba kwa mwenzake kama rafiki wa kawaida tu au kwa matarajio ya kuja kuwa mke/mume hapo baadae?

Kama zawadi hio ilitolewa kwa lengo la pili, yaani kwa matarajio ya kuwa mume na mke hapo baadae, basi zawadi hio itakua yenye sharti yaani“conditional”. Ila kama zawadi hio ilitolewa na mmoja kati ya wachumba hao kama mtu wa kawaida tu, pasipo sharti, basi zawadi hio itakua ni mali binafsi ya mchumba huyo aliyepewa zawadi hio na inaweza kurudishwa.

Kifungu cha 71 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971, kinatoa haki ya kurudishiwa zawadi zilizotolewa na mmoja kati ya wachumba hao kwa matarajio ya kufunga ndoa lakini kwa sababu moja au nyingine ndoa hiyo haikufungwa.

Hivyo mtoa zawadi ana haki ya kufungua shauri mahakamani kudai zawadi alizompa mchumba wake arudishiwe kwa kuithibitishia mahakama kua zawadi hizo alitoa kwa sharti la kufunga ndoa (that the gift(s) was conditional on the marriage being contracted) na sio vinginevyo.

Mahakama lazima ijiridhishe kwamba zawadi hizo zilitolewa kwa sharti kwamba wachumba hao wana nia ya kufunga ndoa.

Sababu za msingi zinazoweza kepelekea uchumba kuvunjika;

1. Kutokuweka bayana masuala ya msingi kwa mchumba wako, hasa masuala yale ambayo kimsingi unatakiwa kuyaweka wazi. Mfano; utofauti wa dini na taifa (difference of religion and nationality), ugonjwa wa ulevi (dipsomania), utasa au ugumba (sterility) na kadhalika.

2. Kuvunja makubaliano. Mfano, kama mmoja kati ya wachumba hao anafanya matendo kinyume na maadili na mtu wa tatu (kama kuchepuka – neno lisilo rasmi) au mmoja kati ya wachumba hao anakataa pendekezo la kufunga ndoa kwa muda mrefu pasipo sababu za msingi.

3. Mabadiliko makubwa kutokea kati ya wachumba baada ya kuingia katika uchumba huo ambayo yanahatarisha kufanikisha kufungwa kwa ndoa rasmi. Mfano; uhanithi “impotence”, wazimu/ukichaa “insanity” baina ya wachumba na kadhalika.

Credit by Mung Chris
 
Back
Top Bottom