Je, unaweza kuishi na mwenza ambaye kamwe hakuambii neno “nakupenda”?

Mapenzi ni matendo sio maneno, anaeza kukuambia anakupenda kumbe hana hata hayo mapenzi na wewe, na anaeza asikuambie ila matendo yake ni uthibitisho tosha.
 
Neno nakupenda lina maana kubwa saana kwenye maisha ya ndoa, tusiishi kwa mazoea ndio hupunguza hisia za mapenzi na mwisho mnaishia kuchepukaa.

Kama unampa kila kitu kuonyesha unampenda, inakugharimu nini kumwambia nakupenda!!! Mwambie nakupenda mara nyingi uwezavyo huo ndo ubavu wako bwana!!!!!
 
Good day all

Hii maada nimeiona sehemu nikaipenda nimeona sio mbaya ku share hapa!

wewe kama mwanamke au hata kama Ni mwanaume Unaweza kuishi na mtu ambaye upo naye katika mahusiano na kamwe hajawahi kukutamkia “Nakupenda”?

Your partner anaweza akawa anakupenda na kukuonesha kwa matendo tu kuwa anakupenda na kukujali lakini kukutamkia neno Nakupenda kwake ni tatizo.

Au mwingine anakujibu tu pale wewe unapomwambia unampenda lakini yeye hajawahi kuanza kukuambia wewe.

Binadamu tumeumbwa tofauti, wengine huwa wanaamini kuwa wanapendwa pale tu ambapo wenza wao watawatamkia kabisa na wengine huwa wanaona kuwa neno hilo halina mana yoyote. Unakuta mtu huyu anaweza kumwambia ndugu, mtoto au hata rafiki yake kuwa anampenda lakini kamwe asimtamkie mwenza wake.

Wewe je, unaweza kuishi na mtu ambaye kamwe hajawahi kukuambia neno “Nakupenda?

hayo mbona yapo tuu...
 
Neno nakupenda lina maana kubwa saana kwenye maisha ya ndoa, tusiishi kwa mazoea ndio hupunguza hisia za mapenzi na mwisho mnaishia kuchepukaa.

Kama unampa kila kitu kuonyesha unampenda, inakugharimu nini kumwambia nakupenda!!! Mwambie nakupenda mara nyingi uwezavyo huo ndo ubavu wako bwana!!!!!
like it..........
 
Nilikutana na mpenzi wangu pasipo kuambiana nakupenda yani ilikuwa kama emergency nikajikuta niko nae kimwili amekuwa mpenzi wangu kwa muda wa miezi mitatu siku moja ndio niligundua kumbe nampenda, siku hiyo ndio nilimtamkia nakupenda ingawaji yeye alikuwa akinitamkia mara kwa mara alifurahi sana siku hiyo.
mkuu ilishawah kunitokea hio asee, mzigoni nikajikuta nimeropoka na sijawah kumtamkia kabla, alinishushua akaniambia mbona sijawah kumuambia kabla
 
haahaha not msichana ni mama pia!
THE SAME JINSIA......maana ndio mnaliliaga vitu kama hivyo. me kama mwanaume hata usinponambia hiyo kitu wala hainisumbui kichwa! but wadada wao itakuwa shida....unakuta eti analiwa na mtu kisa tu anamwambia umependeza kila siku na eti baby wake hamwambiagi ( this is stupidy kwa kweli) inabidi tu uelewe kuwa kuishi na mwanamke sio kazi ndogo so anapoamua kujifunga na wewe jua anakupenda kweli so u dont have to worry kuwa anakwambia anakupenda kila siku au la....
by the way ukiona mwanaume haishi kukwambia nakupenda ujue anapiga nje so anajaribu kusawazisha......well just a thought.
 
hayo ni mawazo yako, kumwambia mwenzio unampenda wala haitumii nguvu, ila wengi wanashindwa kutamka kwa sababu hawako romantic pia, kwa hiyo sio makosa yao ila wameumwa hivyo
 
Natamkaga hilo neno kuuwa ugomvi au kusawazisha tofauti baina yetu..
 
Back
Top Bottom