Je, unaweza kuishi na mwenza ambaye kamwe hakuambii neno “nakupenda”?

cheupe dawa

Senior Member
Apr 3, 2016
172
250
Good day all

Hii maada nimeiona sehemu nikaipenda nimeona sio mbaya ku-share hapa!

Wewe kama mwanamke au hata kama ni mwanaume unaweza kuishi na mtu ambaye upo naye katika mahusiano na kamwe hajawahi kukutamkia “Nakupenda”?

Your partner anaweza akawa anakupenda na kukuonesha kwa matendo tu kuwa anakupenda na kukujali lakini kukutamkia neno nakupenda kwake ni tatizo.

Au mwingine anakujibu tu pale wewe unapomwambia unampenda lakini yeye hajawahi kuanza kukuambia wewe.

Binadamu tumeumbwa tofauti, wengine huwa wanaamini kuwa wanapendwa pale tu ambapo wenza wao watawatamkia kabisa na wengine huwa wanaona kuwa neno hilo halina mana yoyote. Unakuta mtu huyu anaweza kumwambia ndugu, mtoto au hata rafiki yake kuwa anampenda lakini kamwe asimtamkie mwenza wake.

Wewe je, unaweza kuishi na mtu ambaye kamwe hajawahi kukuambia neno “Nakupenda?
 

Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,319
2,000
Neno nakupenda gumu san kutamka, niliwahi kumtamkia mtu mmoja tu,dada yangu labda na watoto wadogo wa ndugu na jamaa tukiwa tunataniana labda katoto kanasema wewe anko hunipendi baada ya kutokapelekea zawadi najitetea nakupenda.

Swali, kwanza unampendaje mtu ambae sio ndugu yako?
 

sinajinasasa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
2,291
2,000
Huu mwaka wa 14 sijawahi kumwambia mke wangu nakupenda hata yeye huwa haniambii lakini tunapendana, inategemea utamaduni wenu/wako.
Mfano ni nadra sana kwa wajapani kupeana kiss, hiyo sio culture yao
 

homo sapiens

Senior Member
Nov 5, 2016
162
250
"Ada ya Mja kunena, Muungwana ni vitendo" Ni watu dhaifu pekee huburudishwa na neno 'nakupenda' ,kumjali mwenza wako kwa matendo murua kunatosha kabisa kuelezea mapenzi ulo nayo kwake.
 

shiu yang

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
3,171
2,000
Nilikutana na mpenzi wangu pasipo kuambiana nakupenda yani ilikuwa kama emergency nikajikuta niko nae kimwili amekuwa mpenzi wangu kwa muda wa miezi mitatu siku moja ndio niligundua kumbe nampenda, siku hiyo ndio nilimtamkia nakupenda ingawaji yeye alikuwa akinitamkia mara kwa mara alifurahi sana siku hiyo.
 

The Messenger

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,528
2,000
Unavyosema "MWENZI" unamaanisha
- Mke/ Mume
- Mpenzi au
- Sex partner?
Upendo ndio amri kuu ila huwezi kua na wapenzi dunia nzima.
 

Clueless14

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
2,956
2,000
Nyie mlio kwenye ndoa na hamuwambii wenza wenu mnawapenda mna matatizo. Matendo yakiamnatana na maneno ya kumaanisha is even more perfect!

Hapo ndipo ilipo tofauti kuu ya kwanza ya mapenzi ya mzungu na mwafrika aka mtanzania.
 

Marlex Jr El

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
1,785
2,000
Kwa mazingira niliyo kulia kutamka neno NAKUPENDA ni mtihani mzito sana.

Kwahy mazingira atokayo mtu pia uchangia wepesi wa ulimi wake kutamka neno hilo.

Neno NISAMEHE kwangu pia uwa ni mtihani kulitamka hivyo ni rai yangu kwa wazazi na walezi kuwahusia watoto wetu juu ya umuhimu wa maneno kama hayo ktk maisha yao ya kila siku.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom