Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Dada Shadeeya mie nitaonyesha ufundi wangu wa kupika mbaazi za kukata
Nimeshaandaa mbaazi zangu zipo jikoni zinachemka wakati wa kuzichemsha hutakuw kutia maji mengi maji kidogo kidogo ili kuepuka zisiorojeke zikiiva unaziepua unaeka pembeni epuka zisiorojeke


Viambaupishi
Vitunguu maji 2
Hoho
Karoti
Chumvi
Pilipili mwendokasi
Nazi 3/4
Binzari ya njano


Jinsi ya kuziunga mbaazi zako
Kuna nazi yako vizuuuri ichuje na maji kidogo kidogo tupate lile tui zito tu ukishamaliza hapo chukua mbaaz zako ambazo tyr zimeshaiva zimimine kwenye chujio theni chukua jagi la maji mimina yale maji kweny zile mbaazi maan huwa zina kauchungu flan tunafany hiv ili kukaondoa kale kauchungu ukishamaliza kuzimiminia maji ziwache mpk zijichuje maji yote zoezi hilo likiisha chukua sufuria yako ambayo utatumia kuziunga sasa ktk lile tui ulilochuja mimina kidogo tui kweny sufuria kidog sana then katakata hoho pis ndogndog vitunguu pic ndog pia na karot pis ndog pia ukimaliza hapo mimina zile mbaazi kwenye hiyo sufuria ulimokatia hivyo vitu tia na chumvi kidog bandika kiasi viive vile viambaupishi tu vikikauka epua chini weka pembeni

Zoezi la mwisho ni kupika tui sasa ukiharibu hapa umeharibu maan nzima ya mbaazi za kukata

Tyr umeshachuja nazi yako tui lipo kwenye sufuria hakikisha umetumia tui zito tu ukimaliza hapo katia katia hoho karot vitunguu maji na binzari yako ya njano hapa utakadiria wewe mwenyewe tui liwe njano vitu vyote hivyo ukate pic ndog ndog tia na zile pilipili zako ili kuleta ladha zaidi Hakikisha viambaupishi vyote unavitia tui likiwa lipo chini ukishamaliza kuliunga tui lako libandike jikoni hakikisha ukibandika tui lako mkono wako hautakiw kutoka jikoni unatakiwa ulikoroge mpk lile tui lishikane liwe zito tui likishaiva unaepua unaweka pembeni unaacha lipoe likishapoa unchukua sufuria yako yenye zile mbaazi nazo zitakuwa zimepoa tui likipoa unalimimina kwenye zile mbaazi hapo tayr zitakuwa zipo tyr kwa kuliwa mbaazi zako unaweza kula kwa chapati maandazi mkate wa kumimina ni mimi mpishi wenu Ukhty....
Shadeeya@Rogie@Sesten zakazaka
umenikumbusha mbali duuuuh na maandazi au chapati:p mambo yanakua mazuri
 
Kij
Wee tena yalete mdogo wangu nimeyakumbuka lol.

Mi napenda yale ambayo ukiyatafuna yana nata nata yaani huwa ni mwendo wa kujilamba tu😀😀😀
Kijaluba
Mahabubaa
Kopaa
La mchanaa
Ukililaaa
Lanatanaa

Walisikika watoto wale wakiimba na kucheza
Umenikumbusha utoto wangu Wallah 😘😘🤣🤣😀
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom