Je, unaungaje chakula chako kwa kutumia nazi?

Shadeeya

JF-Expert Member
Mar 12, 2014
48,321
115,321
Habarini Wakuu. Leo nataka tupeane mawili matatu ya namna ya kupika kwa kutumia nazi hapa haijalishi nazi iwe ni ile ya kukuna mwenyewe au zile zinazouzwa madukani.

- Je unaandaa tui lako katika sehemu ngapi?
- Au hata kama ni zile tui za kununua madukani unapikaje pikaje au unaliweka kwenye upishi wako wakati gani?
- Je unaungaje wewe mpaka kikawa tayari hicho chakula chako cha nazi?
-Unatanguliza nini kisha unamalizia na nini?
- Pia unaweka nini na nini kwenye huo upishi wako ambao ndani yake unaweka nazi?

Mfano: Mimi nikitaka kupika maharage ya nazi huwa naandaa tui langu katika makundi mawili moja lile zito na lingine la kawaida tu ila chache.

Basi nikishayachemsha na maji yakaiva hayo maharage huwa nakatia kitunguu maji kikishachemkia na maji na kuweka maji kidoogo, yakikauka huwa naweka lile tui la pili ambalo wakati wa kuchuja lilikuwa la kwanza nakoroga kisha naweka chumvi ya saizi yangu baada ya hapo namalizia lile tui la nazi la mwanzo ambalo hapa huwa la mwisho kisha naliacha lichemke kidogo baada ya hapo maharage yanakuwa tayari kwa kuliwa.

Haya wenzangu mnapikaje iwe ni
- Maandazi
- Ubwabwa
- Mboga za majani
- Mchuzi wa samaki
- Dagaa wa nazi
- Njegere
- Makande
- Ndizi
- Viazi vitamu
- Visheti
- Mkate wa Mchele
- Mihogo
- Magimbi
- Maharage

Yaani chakula chochote kile ilimradi ndani yake unaweka nazi.

KARIBUNI TUBADILISHANE UJUZI.
 
Mfano:- Mi nikitaka kupika maharage ya nazi huwa naandaa tui langu katika makundi mawili moja lile zito na lingine la kawaida tu ila chache.

Basi nikishayachemsha na maji yakaiva hayo maharage huwa nakatia kitunguu maji kikishachemkia na maji na kuweka maji kidoogo, yakikauka huwa naweka lile tui la pili ambalo wakati wa kuchuja lilikuwa la kwanza nakoroga kisha naweka chumvi ya saizi yangu baada ya hapo namalizia lile tui la nazi la mwanzo ambalo hapa huwa la mwisho kisha naliacha lichemke kidogo baada ya hapo maharage yanakuwa tayari kwa kuliwa.
Simple na haipotezi asili/ ladha ya maharage hua napenda hivi maaana kuna watu wana njonjo mpaka unakua huelewi unakula nini.
 
Nikipika wali naa kuku naa.
Nakuna nazi moja kwanza ambayo ni ya mboga. Naweka matui mawili la kwanza zito na la pili sio zito. Naweka mafuta kidogo then kitunguu maji hoho na carrot za kukata box vikichemka kidogo maweka kuku pilipili na saumu. Kisha nyanya, ikiiva naeka chicken masala halafu tui la pili naacha ichemke lipungue kidogo ndio naweka tui la kwanza ikichemka naipua.
Machicha yake nakunia nazi nyingine ya wali kwa juu. Nakamua kiasi kitakachotosha kuivisha mchele. Nabandika jikoni tui langu likichemka natia chumvi na iliki ya unga naweka mchele na carrot ya kusaga. Na kama kuna kamchicha nakawekea tui iliyobaki kidogo ile ya wali ambalo sio zito.

Napenda sana chakula cha nazi.
 
Me too napenda chakula cha nazi,kinakua kitamu + kinanukia vzur

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipikavyo Ndizi mshale za nyama ambazo naweka nazi:

Hapo nyama nishaiandaa iko jiko inachemka huku namenya ndizi zangu kisha nazikatakata saizi na muundo ninaoupenda kisha naziosha na kuweka kwenye sufuria.

Nyama ikishakauka yale maji ya kwanza naiepua ikiwa imeiva kidogo basi naichukua kisha naimimina juu ya ile sufuria yenye ndizi kisha nakatia kitunguu maji , nyanya halafu naweka chumvi , kabla sijazibandika jikoni nazipeta ili zichanganyike kisha naziweka maji kidogo ya kuzichemshia ili ndizi ziondoke ule ubichi.

Wakati zinachemka huku nachuja tui langu katika sehemu mbili zito na lile la kawaida ambalo linakuwa kidogo ili ndizi zangu zipate kukolea hiyo nazi.

Yale maji yakishakauka naweka tui langu lile la pili halafu nawacha zichemke baada ya lile tui kuchemka na kukauka namalizia lile zito nalo likikauka ndizi zangu zinakuwa tayari kwa kuliwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom