BABA TUPAC
JF-Expert Member
- Sep 30, 2015
- 1,526
- 3,801
NOTE: Thread hii haijamlenga mtu yeyote yule, thread hii inalengo la kuelezea ugonjwa huu ambao inaonekana wanasiasa wengi wanao.
‘’Narcissistic personality disorder’’ ni aina ya ugonjwa wa utu, ugonjwa huu unachangiwa na mtu kujiona wa muhimu sana, anahitajika kuonekana zaidi na pia kupendwa kupita kiasi. Mtu mwenye ugonjwa huu huwa hana mahusiano mazuri na kukosa huruma kwa watu wengine, mgonjwa huyu huwa na hali ya kujiamini kupita kiasi. Ugonjwa huu humfanya mtu kuwa kukosa furaha endapo hajapewa kipaumbele katika baadhi ya mambo au kupewa heshima ambayo anahisi anastahili, mtu na wa namna hii si rahisi kuwaamini watu waliokaribu na yeye.
DALILI ZA UGONJWA HUU
Kujiamini kupita kiasi, Kuhitaji heshima na kupendwa muda wote, Kujiona mshindi katika kila jambo hata kama si kweli, Kujisifu katika mambo usiyostahili, Kutawala katika mazungumzo ili aonekane yeye tu, Kutokuwa na uwezo wa kutambua mahitaji na hisia za wengine na Kujihisi upo sahihi katika kila jambo.
Watu wenye ugonjwa huu wa ‘’narcissistic’’ hupata wakati mgumu sana pindi; wasiposifiwa hata wasipofanya jambo la maana, hawana uwezo wa kuzuia hisia na tabia zao, kudharau wengine na kuwafanya hawana lolote la maana na muda wote wanajihisi hawapo salama.
CHANZO CHA UGONJWA HUU
Sababu kubwa za ugonjwa zipo tatu; 1. Mazingira – hii hutokana na kutokuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya wazazi na mtoto wakati wa ukuaji 2. Tabia ya kurithi 3. Uhusiano wa ubongo, tabia na fikra
Tafiti zinaonyesha kwamba ugonjwa huu unaathiri sana wanaume kuliko wanawake na mara nyingi huanzia utotoni.
Pamoja na madhara mengi ya huu ugonjwa, moja kubwa ni kwamba hupelekea mgonjwa kujiua.
MATIBABU
- Ugonjwa huu hauna dawa, ni vema kwa mgonjwa kumuona mwanasaikolojia kwa ushauri zaidi.
Sources:
American Psychiatric Association
Center for Substance Abuse Treatment