Je, Unatakiwa kumwambia mwenza wako idadi ya uliowahi kufanya nao ngono?

MR LINKO

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
2,811
3,091
happy-young-couple-royalty-free-image-530577612-1538407721.jpg

Kumuuliza mpenzi wako kuhusu historia yake ya ngono inaweza kuwa kama kutazama filamu ya kutisha, unataka kujua kinachoendelea lakini pia hutaki kujua.

Wataalamu wa mahusiano wanaeleza kuwa kufanya hivi kunaweza kuwa na faida lakini pia hasara kwa upande mwingine.

Hizi ni faida na hasara za kuweka wazi idadi ya wapenzi wako wa zamani ulioshiriki nao ngono.

Sio lazima kuweka siri Sarah Ryan, mtaalam wa mahusiano anaamini kuwa muwazi kunaweza kusaidia kupeleka uhusiano wako katika kiwango kinachofuata, kwa kuwa uhusiano unaodumu hujengwa kwa mambo mawili ya msingi ikiwa ni uaminifu na heshima.

“Ikiwa uko kwenye uhusiano ambao unataka yafike mbali, basi kwanini ujizuie kutoa uzoefu wako kutoka kwa wenza wako wa zamani? Kuzuia mambo kwenye maisha kunahitaji nguvu zaidi kuliko kukabiliana nayo na kuyachilia,” anasema Matukio yako ya zamani ni sehemu ya jinsi ulivyo leo.

Bila shaka uzoefu wako wa zamani wa kimapenzi na ngono huchangia kukuunda jinsi ulivyo, na jinsi unavyoishi katika mahusiano yako ya sasa, hivyo inaweza kumsaidia mwenza wako kukuelewa zaidi.

Je! Nini hasara ya kuwa muwazi juu ya idadi ya wapenzi ulioshiriki nao ngono? Ukosefu wa usalama

Mtaalam wa uhusiano wa NYC na Mwandishi wa Breakup Triage, Susan Winter anasema kufafanua kwa kina kuhusu historia yako ya zamani ya ngono kunaweza kusababisha matatizo kwa mwenzi wako, kwa kuwa aina hii ya habari huleta ulinganisho na ukosefu wa usalama kwenye mahusiano.

Inaweza kuwa ishara kwamba mwenzi wako anadhibiti sana.

Ikiwa mpenzi wako anauliza juu ya hili kwa hali ya kawaida, basi hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, lakini ikiwa anakushinikiza au kukashifu, unapaswa kulitafakari hilo.

Ishara ya uhusiano mzuri ni kuhisi kama unaweza kumwambia mwenza wako ikiwa unataka, lakini sio kuhisi kama lazima ufanye hivyo. Ikiwa anakulazimisha kutaja idadi ya watu ulioshiriki nao mapenzi, inaweza kuwa dalili za kutaka kukudhibiti, inaweza kusababisha madhara zaidi kuliko manufaa.

Kulingana na Dk. Robi Ludwig, mtaalamu wa magonjwa ya akili anasema watu wanataka kujua kuwa wako na mtu ambaye amekuwa na historia nzuri ya mapenzi huko nyuma, lakini maelezo ya maisha ya ngono ya mtu mara nyingi ni ngumu kwa mtu yeyote kuyafurahia kwani inaweza kusababisha madhara kwenye uhusiano hasa mwanzoni.

Mwisho wa siku namba ni namba, hivyo hakikisha hujitesi sana kuhusu kujua uzoefu wake. Ikiwa mpenzi wako hataki kukuambia idadi ni sawa kuuliza kwa nini, lakini usimlazimishe kujua kwani unapaswa pia kuheshimu faragha yake.
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
36,591
39,320
Ukimwambia mwanaume wa bongo, eti niliwahi tembea na wanaume kumi au hamsini, si ndo itakuwa tusi lako .....

Kuna wakati tulikuwa kwenye mazungumzo ya kawaida na wadada wa umri wa kati, walipoulizana swali kama hilo majibu yalikuwa ni aibu, mmoja alisema ukiwaweka wanaume aliotembea nao basi la mwendokasi linajaa na kuzidi, sasa ndo umwambie mume hivyo, ndoa si ndo imeisha?

Anyways, nitarudi kutaja idadi yangu ila ni ndogo sawa tu na namba za viatu vya watoto., I'll be back.
 

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
7,805
5,923
Safari ni safari iwe Kwa miguuu ama Kwa basi au Kwa baiskeli, kwangu Mimi kumuuliza mwanamke habari za nyuma ni jambo jema sana kwani linakupa picha ya aina ya mwanamke uliyenaye kwamba huyu Pamoja na kuwa nampenda au anaonekana kunipenda ila nikimtibua panga mkononi, au huyu nikijifanya namlaza mzungu wa nne wiki nzima nimeliwa kwasababu zege kwake halilali! Kiufupi kujua historia ya mwenzako ni jambo zuri na la muhimu wengine Wana urithi wa magonjwa hivyo lazima ujue usiegemee tu kujua idadi ya wanaume aliolala nao.
 

Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
7,805
5,923
Ukimwambia mwanaume wa bongo, eti niliwahi tembea na wanaume kumi au hamsini, si ndo itakuwa tusi lako .....

Kuna wakati tulikuwa kwenye mazungumzo ya kawaida na wadada wa umri wa kati, walipoulizana swali kama hilo majibu yalikuwa ni aibu, mmoja alisema ukiwaweka wanaume aliotembea nao basi la mwendokasi linajaa na kuzidi, sasa ndo umwambie mume hivyo, ndoa si ndo imeisha?

Anyways, nitarudi kutaja idadi yangu ila ni ndogo sawa tu na namba za viatu vya watoto., I'll be back.
Ndio Iko hivyo uambiwe kontena linajaa bado ung'ang'anie unafikiri nyimbo za vibamia zimetokana na nini
 

Interlacustrine R

JF-Expert Member
Jan 22, 2022
1,762
3,433
Hivi hili nalo ni la kufungulia uzi hapa JF?Jando zirudishwe tena kwenye Jamii maana si kwa uvulana huu.
 

Tipstipstor

JF-Expert Member
Nov 29, 2021
1,538
3,153
Hakuna haja ya kuulizana kuhusu masuala yaliyopita wakati mmeufungua ukurasa mpya. Hususani ikiwa ni mahusiano ya zinaa (dating) ila kwa ndoa unaweza kumuuliza mwenza wako, je umeolewa au umeoa ndoa ya ngapi??
 

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
5,542
7,309
Watu wengi kwenye mahusiano hawasemi ukweli kuhusu back group zao hata kama aliwahi kuwa na wapenzi 1000 atakupunguza na kusema labda watano au watatu full stop.

Fix ni nyingi sana kwenye mahusiano.
 

notyfeky

JF-Expert Member
Apr 17, 2022
263
168
Kwani inaacha alama? Au kuna mihuri. Weka tangawizi, kamulia limau, kitu inabanaaaaa, kama bikra vileee.
Kule Zenji Hadi damu inatoka, mzee unashangilia kuvunja kikombe kumbe zoba tuu, dem anacheeeekaaaa kumoyo!!!
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
48,025
66,467
Kwahio muda huo mnakua mmekaa wapi? Ukikuta ka-date na Baba Yako? Stress nyingine mnajitakia wenyewe tu then mnaishia kuchomana moto au visu
 

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
13,867
17,777
Ukimwambia mwanaume wa bongo, eti niliwahi tembea na wanaume kumi au hamsini, si ndo itakuwa tusi lako .....

Kuna wakati tulikuwa kwenye mazungumzo ya kawaida na wadada wa umri wa kati, walipoulizana swali kama hilo majibu yalikuwa ni aibu, mmoja alisema ukiwaweka wanaume aliotembea nao basi la mwendokasi linajaa na kuzidi, sasa ndo umwambie mume hivyo, ndoa si ndo imeisha?

Anyways, nitarudi kutaja idadi yangu ila ni ndogo sawa tu na namba za viatu vya watoto., I'll be back.
Ujue kuwa uongo ni dhambi, sema tu 800 ili ujuwe kuwa anakupenda au la...
 

Kelsea

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
6,786
15,229
Akikuambia wapo 100+ utaendelea kumpenda? Naona haina haja tuanzie tulipokutana.
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
34,852
39,755
Kwanza niulize ili iweje,maana mimi mwenyewe hata idadi ya niliowagegeda siifahamu wala siikumbuki. Mimi najua mashine ni yangu kuanzia nilipomuoa hayo ya nyuma sitaki kuyajua. Let bygone be bygone
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom