Je unataka kuwa CCNA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je unataka kuwa CCNA?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kilongwe, Jul 17, 2010.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Makala hii imekopiwa toka AfroIT Blog

  Teknolojia tuyayoiamini ni ile inayobadilika ili kukidhi matakwa ya jamii husika, mabadiliko hayo ni lazima yaendane na ukuaji wa ufahamu kwa watu wanaoisimamia au kuivumbua ili kuwezesha kuvumbua mambo mengi zaidi kwani walenga walisema safari moja huanzisha nyingine. Kuna njia nyingi za kupima huo ufahamu au kiwango cha mtu katika teknolojia au elimu husika,njia kubwa inayotumika katika ulimwengu wa leo ni njia ya mitihani,kuna mitihani ya aina nyingi katika ulimwengu wa teknolojia ila leo tutaangalia huu mmojawapo,yaani CCNA kwa kirefu ni Cisco Certified Network Associate.NIcheti kinachotolewa na Cisco kwa mtu aliyefaulu mtihani wa CCNA.
  Je unataka kujua jinsi yakuinstall, kuconfigure and kudhibiti utendaji kazi wa mifumo ya mawasiliano? Je unataka kukuza na kuendeleza elimu yako kwenye masuala ya mawasiliano ya habari ? Hivyo basi CCNA ni chaguo murua kwako kama kama mwanzo wa safari.Mtihani sio tu kukariri na kufaulu bali ni kupata maarifa,kipindi unajiandaa na CCNA hadi kumaliza na kufaulu kwake ni dhahiri utakuwa umepata maarifa ya kutosha katika nyanja za mawasiliano.

  Kwanini CCNA?
  CCNA ni moja kati ya vyeti vinavyothaminika, leo hii CCNA imekuwa ni kigezo muhimu kwenye harakati za kazi.Watahiniwa watakaofaulu mtihani wa CCNA hutunukiwa cheti kutoka Cisco,kampuni kubwa kabisa na linaloongoza katika mlongo wa mawasiliano. Kwa kupata cheti hichi kitaweka kitu kipya na cheye kung’ara kwenye resume yako huku ukipata kutambulika au kuibuka mshindi mbele ya wafanyakazi wenzako

  Aina za CCNA
  Katika miaka ya karibuni,Cisco wameigawa CCNA kwenye makundi mengi, nimewahi kukuongea na watu wengi ambao waliniomba ushauri kwenye CCNA,wengi wao bado hawafahamu kwamba CCNA ina makundi kibao,hivyo leo hii nitakueleza makundi hayo ya CCNA.

  CCNA imegawanyika kwenye makundi makuu manne
  1. CCNA Wireless – Kwa wale wanaopenda mambo ya wireless
  2. CCNA VOICE- Hii inahusika sana na sauti kwenye IP (VOIP)
  3. CCNA SECURITY – Hii ni wale wanaojiandaa kutulinda na wavamizi au watu wabaya kwenye mawasiliano ya teknolojia
  4. CCNA R&S - Hii ni kwa ujumla,hapo zamani kulikuwa na CCNA moja tu ambayo ni R&S,tofauti ya hii ya leo na ile ya zamani ni kuwa hapo zamani kila kitu kiliwekwa kwenye R&S,hivyo ulikuwa unatakiwa kusoma mambo mengo kwa pamoja ila kwa juu juu, sasa mambo ni machache ila kwa udani kidogo.
  Hatua za kufikia CCNA

  Kuna njia kuu tatu za kuendea kupata hiki cheti cha CCNA,nitakufafanulia moja baada ya nyingine huku nikiorodhesha faida na hasara zake,mwishoni nitamalizia kwa kukupa ushauri binafsi ni njia gani inafaa kwa watu husika.
  Zifuatazo ni hatua za kufikia CCNA

  1. Kupitia vyuo vilivyohidhinishwa na Cisco
  Hii ni njia mojawapo ambayo hutumika kwenye vyuo vingi,njia hii imeanza kupoteza umaarufu kutokana na muingiliano wa masilahi ya kibiashara.Kwani vyuo vingni vinaona kwa kufanya hivyo vitakuw vinaipendelea Cisco.Kwa kutumia njia hii wanafunzi hupata mafunzo yote ya CCNA ambayo yamevunjwavunjwa kwenye mihula, baada ya kumaliza mihula yote na kufanya mitihani husika ya chuo matokeo huambatanishwa kwenye orodha ya masomo yako ikionesha vipengele vyote ulivyosoma. Wanafunzi huwa wanashauriwa kufanya mtihani wa Cisco baada ya kumaliza masomo ili kupata cheti kinachotambuliwa dunia nzima

  Faida:Gharama ni ndogo,kuna baadhi ya vyuo ni bure pia ni rahisi kusoma kwani hakuna msongo


  Hasara:Makampuni na wajiri wengi hawana imani nazo,hii ni kutokana na ubora wake hutegemeana na chuo husika .Hutumia muda mwingi, silabasi yote imagawanywa kwenye mihula.Kazi za vitendo ni haba; Ingawa CCNA haina kazi za vitendo vingi ila zinahitajika kwa uhaba wake,vyuo vingi huwa na wanafunzi wengi ambao wote hutegemea vifaa hivyohivyo hivyo humbana mwanafunzi kwenye kazi za vitendo

  2. Kupitia vituo vilivyothibitishwa na Cisco
  Hii ndio njia mojawapo ambayo imezoeleka mno ambapo mwanafunzi hupata kozi za CCNA toka kwenye vituo vilivyohidhinishwa na Cisco,vituo hivyo huweza kuthibitishwa kwa kutembelea website ya Cisco.Mwanafunzi hupata kozi ya CCNA kulingana na mpangilio wa kituo husika.Kwa kutumia njia hii kozi nzima ya CCNA hufundishwa kwa pamoja au katika awamu kuu mbili ambazo ni CCENT na ICND2.

  Faida:Muda,vyuo vingi hutumia wiki moja hadi mbili kumaliza kozi nzima ya CCNA hivyo humpa mwanafunzi muda mwingi wa kujiandaa na mtihani. Msaada,kwenye vituo vingi huwa na walimu wengi wenye ujuzi na level kubwa kama CCIE hivyo mwanafunzi hupata msaada wa uhakika pindi anapokutana na matatizo au utata.
  Hasara: Gharama,njia hii huitaji pesa nyingi kiasi ambazo ni kubwa kwa wanafunzi wa kipato cha chini.Kukariri:Kwakuwa vituo vingi hujivunia au kushindana kulingana idadi ya wanafunzi waliofaulu kutokea kwenye kituo chao hivyo vituo vingi huwapatia wanafunzi mitihani ya maandalizi(aka madesa aka Brain dumps) kwa ajili ya kujiandaa na mitihani ambayo ni mfanano wa mtihani husika hivyo hudumaza uwezo wa mwanafunzi na kuondoa lengo la mtihani.

  3. Kujisomea mwenyewe
  Hii ni njia ambayo inawafaa sana wale wenzangu na mimi ambao hawana muda au wale wenye uwezo wa kujisomea wenyewe,njia hii hufanyika either kwa kusoma vitabu pekee au kwa kuchanganya na kuangalia video zilizotengenezwa na makampuni yaliyojikita katika kutengeneza video za masomo mbalimbali kama CBT Nuggets, Train Signal, Lynda nk.Makampuni haya mengi huwa na walimu wenye uwezo mkubwa wa kufundisha hivyo humfanya mwanafunzi kujihisi kama yupo darasani,mfano mzuri ni Jeremmy Ciora.
  Katika nchi nyingi zilizoendelea kwenye masuala ya teknolojia,kuna makampuni ambayo hukodisha vifaa vya kufanyia majaribio kama Routers,switches nk kwa bei nafuu hivyo kwa kutumia njia hii ukujumuisha na online studying groups ambazo unaweza kukutana na wenzako wengi ambao nao wapo kwenye harakati za kutafuta cheti hichohicho unaweza kusoma hadi level za juu bila matatizo
  Faida: Faida kubwa ya njia hii ni unafuu kwenye gharama,muda, pia kusoma vitu vingi kwani matatizo mengi hukutegemea wewe mwenyewe katika kuyang’amua.Google huwa kiongozi mkuu kwa wale walioamua kufuata mtindo huu.


  Njia gani inakufaa(Muono wangu)

  Kuchagua njia inayokufaa ni suala binafsi ambalo hutegemea mambo mengi kama kipato,muda na uwezo wa elimu. Njia ya ya pili na tatu zinalingana kwa kiasi fulani. Kama kwako wewe muda sio tatizo ila pesa ni kikwazo basi nenda njia ya kwanza,ila kama pesa hazina tatizo ila muda ni tatizo unaweza kufikiria njia ya pili.Njia ya tatu ni rahisi kwa wale wanaojifunza CCNA kwakuwa CCNA sio ngumu kwa sana hivyo unaweza kujisomea mwenyewe kama utapata kuongozo mzuri pia gharama za lactures nyingi sio kubwa huku ukiwa na uwezo wa kupata student discount au kudownload bure kwenye torents kikao. Hii njia inawafaa watu wenye uwezo mkubwa wa kujisomea wenyewe huku ukiwa na uwezo wa kujichunga(self commitment),la sivyo utamaliza miaka huku ukiimba tu ninataka kuwa CCNA CCNA na CCNA

  Mpangilio bora wa kusoma CCNA
  Kufanya CCNA ni sawa kukamilisha project mojawapo hivyo unahitaji mpangilio utakaokuwezesha kupata cheti na elimu kwa urahisi,ufuatao ni mlolongo wa hatua muhimu za kuzingatia unapoanza kusoma CCNA.

  1. Weka malengo
  Jiwekee malengo kuwa unataka kuwa CCNA huku ukifikiria ni faida gani utazipata baada ya kupata hiyo CCNA,either iwe ni kupandishwa cheo au kupata misifa toka kwa wafanyakazi wenzako na familia kwa ujumla.

  2. Chagua aina ya CCNA
  Baada ya kuwa na malengo ni dhahiri utakuwa unajua ni aina gani ya CCNA inaweza kufikia malengo yako,mfano wewe ni Network Administrator basi CCNA security itamfanya muajiri wako akuweke kwenye hadhi ya juu na misifa kibao toka kwa wenzako utasikia wakikunadi “Jamaa ni noma Yule,hakuna hacker anayekanyaga kwake,hehe” huku mambo mazuri kibao yakipiga hodi.

  3. Lipia mtihani
  Ni mara ngapi umesikia watu wakisema mimi nataka kusoma CCNA,miaka inapita unaishia kuimba tu hiyo CCNA? Binafsi nina marafiki wangu wengi ambao walishasoma kozi zote za CCNA ila kozi zao ziliishia hewani kwani hawakufanya mtihani na kujikuta wakisahau yote waliyosoma,unapolipia mtihani unajiweka kwenye hali ya kujibana huku ukulazimika kuwa makini la sivyo pesa yako itakwenda na maji. Binafsi njia hii imenisaidia kwenye CCIE written pia Lab ambapo tarayi nimeshalipia na nipo kwenye chungu,siku hizi kila nikilala nawaza madola yangu,duh nisipokaza msuli dola zote zimelala.Amin asiamini hii njia ni nzuri.

  4. Chagua njia ya kusoma
  Nimeorodhesha njia tatu hapo juu,hivyo chagua njia inayokufaa,kumbuka pindi uchaguapo njia husika unaweza kushirikisha marafiki,wanafamilia hata wanajamii wengine ambao tayari wameshafanya CCNA au mitihani mingine kwani walenga walisema “Adhabu ya kaburi aijuaye maiti”,unaweza tembelea website mbalimbali za ICT,kwa Tanzania AfroIT ambapo binafsi napatikana kule, ethinker na Jamiiforums kuna wadau wengi waliojikita kwenye masuala haya.

  5. Jiandae halafu fanya mtihani
  Baada ya kuchagua njia husika,unahitaji maandalizi ya kutosha,hii inajumuisha kufanya maswali na kazi nyingi za vitendo. Haijarishi umeamua kutumia njia gani kusoma CCNA, unahitajika kujiunga na makundi mbalimbali ya CCNA online,mojawapo ya makundi hayo ni AfroIT CCNA BOOTCAMP. Baada ya maandalizi yote na kufanya mitihani mbalimbali ya majaribio sasa upo tayari kwa kuchukua mtihani,uwanja ni wako, jiamini na utaweza. CCNA bado sio ngumu sana hivyo uwiano wa kufaulu ni mkubwa tuu.

  6. Feedback
  Baada ya kufanya mtihani haijarishi umefaulu au kufeli basi toa maono yako,hii itasaidia wengine ambao wapo kwenye harakati za kujifunza na kujiandaa kwa CCNA.

  Hitimisho: Kwa maoni,maswali na mengineyo tembelea AfroIT Forums kijiwe cha wana ICT Tanzania
  Part II: Je wazijua faida na kazi za CCNA?
   
 2. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Ni sifa gani mtu anayetaka kusoma CCNA anatakiwa awe nazo?
   
 3. The Spit

  The Spit JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Thanks a lot for this piece of info.I am planning to start going for my CCNA from the first of august.I have actually gained a lot of courage and information from your thread...I will take it through the third option you've mentioned above,nitakamua mwenyewe,njia ya 3,ndo inanifit.
   
 4. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  CCNA inawezwa kusomwa na mtu yeyote mwenye mapenzi na Networking ,cha muhimu ni kumaanisha kwani wengi wetu tumekuwa ni wazuri wa kuimba,CCNA CCNA hadi jua linazama.
   
 5. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwa materials unaweza kukodolea hapa Cisco « AfroIT Downloads
   
 6. g

  gambo99 New Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  great job! great tz product! never ever hog the forum and other related field! here towards ccna certification.
   
 7. Ciro

  Ciro Member

  #7
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wale watakaoamua kwenda na njia ya tatu ilotajwa na mtaalam apo juu bas Programs kama Cisco Packet tracer au GNS3 ni muhimu sana especially km huna Real cisco gears (equipments).... Napendekeza sana GNS3 except kwenye switch configurations itabidi utumie Cisco packet tracer.... its impossible kupasi CCNA exam bila ya kufanya Lab questions katika exam so practice ya configurations ni muhimu sana :)
   
 8. Ciro

  Ciro Member

  #8
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wale watakaoamua kwenda na njia ya tatu ilotajwa na mtaalam apo juu bas Programs kama Cisco Packet tracer au GNS3 ni muhimu sana especially km huna Real cisco gears (equipments).... Napendekeza sana GNS3 except kwenye switch configurations itabidi utumie Cisco packet tracer.... its impossible kupasi CCNA exam bila ya kufanya Lab questions katika exam so practice ya configurations ni muhimu sana :)

  :yell:If at first you don't succeed, try, try again. Then give up. There's no sense being a damn fool about it:yell:
   
 9. Robati

  Robati JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  ok, nice
   
 10. j

  junior05 Senior Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na kwa wale mtakao pata taabu kwenye uelewa zaidi haya mambo tuwasiliane tafadahli
   
 11. Bosco Ntaganda

  Bosco Ntaganda JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 551
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  kaka gharama za kufanya hiyo mitihani ya ccna zimekaaje kwa sasa? nahitaji sana kufahamu, ikiwezekana mwezi june niingie dimbani
   
 12. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nilipoona neno lipia nikaaanza kuwa na wasi wasi kama hii siyo scam kama ile ya scholarship za Belize. Mambo ya kwenye mtandao lazima uwe na shaka. Chungeni mnaotaka kuuvaa mkenge huu.
   
 13. qq.com

  qq.com JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 9, 2012
  Messages: 370
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
 14. dottoz

  dottoz JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 805
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 80
  Website yenu mbona inazngua?
   
 15. Bosco Ntaganda

  Bosco Ntaganda JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 551
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  jamani gharama ya hiyo mitihani ya ccna iko vipi kwa sasa? mwenye taarifa kamili tafadhari
   
Loading...