Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane

Status
Not open for further replies.
Huenda udongo ni kichanga sana, na maji hupotea haraka

Pia yaweza kuwa ni wadudu hasa white flies, hao huleta virusi vya majani vinavyosababisha majani kujikunja kwenda juu

PIGA BOOSTER NDANI MIX NA DIMETHOATE TENA PIGA JUU NA NYUMA YA MAJANI, RUDIA KILA BAADA YA SIKU 14, CHINI ZUNGUSHIA YARAMILLER WINER MBOLEA GRAM 300 KWA MICHE YENYE UMRI ZAIDI YA MWAKA 1 (GRAM 300, NI SAWA/WASTANI NA VIGANJA 3 VYA MKONO WAKO MMOJA, WEKA MAJI KWANZA NDIO MBOLEA IFUATE)

KAMA SHAMBA NI LAKO, WAKATI WA MASIKA WEKA SAMADI YA KUTOSHA KWA KILA MCHE, DEBE 1 KWA MCHE

Mkuu.
Naomba msaada Kwa mara nyingine kuhusu mipapai yangu.
Baadhi yake inakausha majani ya kileleni kama vile imeungua na baadaye eneo la juu inapinda.
Miti miwili imekausha majani yamebaki kileleni.
Nilitumia dawa aina Dimethionate na huimwagilia kila baada ya siku moja.
Ni tatizo gani na nitumie dawa gani.
Natanguliza shukran
 
Huu ni ugonjwa gani kiongozi? nimeona miche miwili ina hii shida mkuu!!

Majani kama hayana nguvu kabisa, nnachoshangaa ni kwamba kuna maji!!

1273_0.jpeg
Hata mimi imenitokea mkuu... Kuna solution au dawa ya kutibu?? Je kinga yake ni dawa gani?? Tupe hata kwa kifupi mkuu ...
 
Huenda udongo ni kichanga sana, na maji hupotea haraka

Pia yaweza kuwa ni wadudu hasa white flies, hao huleta virusi vya majani vinavyosababisha majani kujikunja kwenda juu

PIGA BOOSTER NDANI MIX NA DIMETHOATE TENA PIGA JUU NA NYUMA YA MAJANI, RUDIA KILA BAADA YA SIKU 14, CHINI ZUNGUSHIA YARAMILLER WINER MBOLEA GRAM 300 KWA MICHE YENYE UMRI ZAIDI YA MWAKA 1 (GRAM 300, NI SAWA/WASTANI NA VIGANJA 3 VYA MKONO WAKO MMOJA, WEKA MAJI KWANZA NDIO MBOLEA IFUATE)

KAMA SHAMBA NI LAKO, WAKATI WA MASIKA WEKA SAMADI YA KUTOSHA KWA KILA MCHE, DEBE 1 KWA MCHE

Asante mkuu.
Labda upendekeze aina ya booster. Pia ni kweli ardhi ina kichanga na wiki iliyopita Niliweka yara winner gram 60.
Lakini leo nafanya ulivyoelekeza. Wasiwasi wangu nilikuwa nikifikiri unaweza kuwa ni ukungu.
 
Mkuu wetu usituchoke maana unatufaa haijawai kutokea na wengi tutakuja kukushukuru kwa namna yake tafadhali.
 
Shida yangu Leo ni hii..
IMG_20170923_085019.jpg

IMG_20170923_085010.jpg
Huyu bwana ananisumbua sana kwenye matango yangu,yaani ananivunja moyo sana kila nikipiga dawa aina ya Novathion fentrathion 50EC kesho yake asubuhi namkuta keshatafuna sana majani naomba nishauri nitumie dawa gani.
 
tzhello
POLESANA (NIMEKUJIBU KULE INBOX), LAKINI KWA FAIDA YA WENGINE

TAFUTA DAWA ZA WADUDU HIZI,1. KARATE MIX NA 2. DIMETHOATE (DUME), MIX KWA KIPIMO CHA MILS 10 KILA MOJA KWA MAJI LITA 15, KISHA SPRAY ASUBUHI AU JIONI, ILA NAWE UWE NA PPE MAANA DAWA HIZO NI KALI SANA ZIKIKUINGIA MACHONI/MFUMO WAKO WA UPUMUAJI. HIYO DUME ITASAIDIA SANA MAANA IKO NA CHUMVI NDANI INAZUIA UPUMUAJI NA KUATHIRI NGOZI YAKE

Shida yangu Leo ni hii..
View attachment 603728
View attachment 603730 Huyu bwana ananisumbua sana kwenye matango yangu,yaani ananivunja moyo sana kila nikipiga dawa aina ya Novathion fentrathion 50EC kesho yake asubuhi namkuta keshatafuna sana majani naomba nishauri nitumie dawa gani.
 
Kajirutaluka
POLE SANA MKUU

HIYO HUITWA BAKA JANI WAHI (EARLY BLIGHT)

upload_2017-10-12_15-23-53.png

upload_2017-10-12_15-25-58.png

upload_2017-10-12_15-27-25.png

DAWA ZINGINE UNAZOWEZA KUTUMIA, KUTIBU UKUNGU/FANGASI, NI MULTI POWER PLUS 78WP, NATIVO, NA OTHELLO (AZOXTROBIN 250g/L)

KWA SASA NG'OA HIYO MIMEA, NA TIBU UDONGO, NA PANDA MIMEA JAMII YA GALLIC (VITUNGUU) , RUDIA TENA MAZAO KAMA HAYO ULIYOWEKA (SOLANACEAE) BAADA YA MIEZI 4-6)

KILA LAKHERI
==========================
 
Habari kiongozi,

Ningependa kupata ushauri wa kilimo, mm ni kijana ninae penda kufanya kilimo biashara maeneo ya ruvu mnazi na nimepata shamba huko ambalo lipo karibu na mto ruvu, mazao ambayo ningepanda kuanza nayo ni pilipili mbuz Pamoja na nyanya chungu, kwa ushauri wako mkuu. Je huu ni muda muafaka wa kufanya hiki kilimo. Naomba ushauri wako mkuu.

Kazi njema
 
Junior Nicky

Kiongozi salamu, nimepata ujumbe wako

Unaweza fanya kilimo hicho

Kama unategemea mvua basi fanya kabla ya mvua kuanza na kabla ya mvua kuisha

Kama utapenda kutumia njia za kumwagilia (Kuweka drip line) unaweza kufanya wakati wowote wa kiazi, endapo utakuwa na kisima au maji ya mto jirani

Bei nzuri kwa mazao hayo mara nyingi ni December hadi may, lakini yote itategemea sana na mipango yako namna ya kuuza, maana madalali ni changamoto kubwa sana, anaweza pata faida mara 3 zaidi ya utakayopata.

Kabla ya kuzalisha anzia sokoni kwanza, ujue mahitaji ya soko, aina gani za hiyo bidhaa zinatakiwa, utaratibu wa uuzaji n.k

ASANTE

Habari kiongozi,

Ningependa kupata ushauri wa kilimo, mm ni kijana ninae penda kufanya kilimo biashara maeneo ya ruvu mnazi na nimepata shamba huko ambalo lipo karibu na mto ruvu, mazao ambayo ningepanda kuanza nayo ni pilipili mbuz Pamoja na nyanya chungu, kwa ushauri wako mkuu. Je huu ni muda muafaka wa kufanya hiki kilimo. Naomba ushauri wako mkuu.

Kazi njema
 
Habari mkuu,

Asante sana kwa ushauri wako..

Nitafanya hiyo research kuhusiana na masoko pamoja na hali ya masoko jinsi yalivyo.. Na kwa ushauri zaidi nitawatafuta kwa ushauri zaidi pindi nitakapo anza hii project.

Najerea kusema tena asanteni, Mungu awabariki.
 
Umejaribu kutafuta dawa ya wadudu (Jina la kibiashara=karate) ukamix na nyingine (Jina la kibiashara=Match) umespray imeshindikana mkuu??

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom