Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane

Status
Not open for further replies.
Shida yako inafanana na ya mjumbe hapo juu antimatter

Nilimjibu hivi, "Tatizo linaweza kuwa wadudu kama Amphids au upungufu wa Micro nutrients (Zinc, Boron, na Manganese), zaidi ya yote inaweza kuwa ni water stress (Upungufu wa maji kama ni kiangazi sehemu za huko)-hii ya water stress kwako si ishu.

Hivyo hayo mawili ya wadudu na lishe yanabaki valid, na unatumia samadi ya kuku ambayo ina Phosphorus na Nitrogen kwa wingi, lakini inaupungufu mkubwa sana wa Potassium ambayo haina uwezo wa kushikilia maua na matunda, tafuta booster pia zitasolve tatizo, na chini weka mbolea kama Yar Miller Winner au NPK ya 17:17:17, sijui umri wa miti yako lakini gram 100-500 zinatosha kwa mti mmoja.,tifua kidogo mtalo fanya kama sahani, na kisha uweke mbolea na uifukie kwa udongo
Asante Mkuu.
Lakini miti yangu ina umri wa miezi manane na mingine ina mwaka na nusu.
Ufafanuzi mkuu, kuhusu kipimo cha mbolea, ulichotaja sio kikubwa?
 
hiyo habari sijaipata mkuu

Kuhusu hiyo npk 16:16:16, inafaa pia, utofauti ni mdogo sana wa 1% concentration ya N, P, K , ukiipata tumia mkuu

Habari mkuu!!

Jana nimeenda sokoni kuulizia NPK ya 17 17 17 nikaambiwa siku hizi zimefungiwa nikapewa ya NPK ya 16 16 16!!

Je NPK ya 17:17:17 ina tofauti gani na NPK ya 16:16:16?? ni kweli npk ya 17:17:17 siku hizi zimefungiwa?
 
gram 100 ni resonable, utakachofanya utakuwa ukisplit/ kugawa hicho kipimo mara 3, unaweka gram 30 mwanzo mwa mvua, gram 30 katikati mwa mvua na 40 gram mwishoni mwa mvua, yaani msimu wa mvua ukiisha kila mti unakuwa umepata hizo gram 100. Kama unamwagilia tumia gram 40 tu kwa mara moja kila baada ya miezi2, Ukipata yara miller winner itakufaa sana, coz ya kirutubisho cha Potassium, inayosaidaia kutoa matunda ya Matunda ambayo ipo kwa wingi katika hiyo mbolea

QUOTE="johnmashilatu, post: 22904467, member: 26435"]Asante Mkuu.
Lakini miti yangu ina umri wa miezi manane na mingine ina mwaka na nusu.
Ufafanuzi mkuu, kuhusu kipimo cha mbolea, ulichotaja sio kikubwa?[/QUOTE]
 
Mkuu naomba msaada
Matikiti yangu yameanza kutoa matunda lakini baadhi ya matunda yanaoza nifanyeje?
maana hali si nzuri
 
Msaada wandugu. Wapi naweza kupata mbolea ya Yara Winner na Yara Nitrabo? Maana nimezunguka sana, kila mahali wanasema hawana.
 
Habari mkuu!!

Jana nimeenda sokoni kuulizia NPK ya 17 17 17 nikaambiwa siku hizi zimefungiwa nikapewa ya NPK ya 16 16 16!!

Je NPK ya 17:17:17 ina tofauti gani na NPK ya 16:16:16?? ni kweli npk ya 17:17:17 siku hizi zimefungiwa?
Habari mkuu??

Naweza apply NPK in solution form badala ya kuiweka ikiwa kwenye granular form,??

Vipi gani nitumie? Maji na mbole...
 
Mix na maji mkuu, Tumia mbolea kilo 2 kwa maji lita 100, mix na kisha koroga kwa nusu saa, na kisha kila mche upate mls 250 za maji+Mbolea
Nashukuru sana mkuu!! Zimeanza kutoa maua...nitafanya hivyo leo au kesho jioni!!!

Swali la mwisho...je kipindi hiki cha maua naweza tumia mbolea gani ingine tofauti na npk?? Au nitumia tu npk inatosha?
 
Mix na maji mkuu, Tumia mbolea kilo 2 kwa maji lita 100, mix na kisha koroga kwa nusu saa, na kisha kila mche upate mls 250 za maji+Mbolea
Ukitumia hii system ya water fertilizing inabidi urudie kila baada ya siku ngapi? Yani huo mchanganyiko unakaa siku ngapi ardhini?

Asha
 
Nutrient zinakuwa active ardhini hadi siku 21 tangu first day of application

QUOTE="ASHA NGEDELE, post: 23069614, member: 47629"]Ukitumia hii system ya water fertilizing inabidi urudie kila baada ya siku ngapi? Yani huo mchanganyiko unakaa siku ngapi ardhini?

Asha [/QUOTE]
 
[/QUOTE]
Asante

Asha
 
POLE HILO NI TATIZO LA LISHE, UPUNGUFU WA (VIRUTUBISHO VYA Calcium) na Maji. Tatizo linaitwa Blossom End rot-Kuoza kwa kitako cha tunda, Maji ni muhimu sana.

So weka maji kisha weka Mbolea yenye Calcium kama Yara Nitrabor, au CAN, kila mche upate gram 5. Tatizo litaisha

Habari mkui wangu. Juzi nimepita shambani nimekuta baadhi ya nyanya(tunda na sio mmea) zina doa jeusi kwenye kitako kwa chini kabisa je nini shida?? Na hilo doa ni kama limeoza flan hivi...

Msaada tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom