Je, unatafuta mke? Basi usihangaike tena...... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, unatafuta mke? Basi usihangaike tena......

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WomanOfSubstance, Oct 5, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mke ni bidhaa hadi atafutwe kama vile ni kuku au ng'ombe?
  Nimekuwa nasikia watu hasa wanaume wakiomba watafutiwe wake na dada au mama zao.Tena wengine hudiriki hata kwenda vijijini kwa ajili ya kusaka mke.JF katika thread mbalimbali kumekuwa kunatolewa ushauri kwa akina kaka wenye kutafuta wake kuwa waende vijijini.
  Swali:
  Wewe kaka huoni ni hatari kutafutiwa mke tena kijijini ambako wewe labda hujakaa au umetoka siku nyingi?
  Je unapoletewa ina maana moja kwa moja unaenda kufunga ndoa au ndio mambo ya kutest kwanza kama mali iko sawa kufuatana na matarajio yako?
  Wanawake na wanaume wote mnakaribishwa kuchangia.
   
 2. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Whats the point here???
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  You will see if you need to see it.
   
 4. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,733
  Trophy Points: 280


  1. Kufunga ndo siyo sawa na kuoana.
  2. Kuoa hakuna cha kuonja maana ndoa, mke/mme, siyo ngono wala mapishi.
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  sawa kabisa mkuu Sophist...naomba maoni yako kuhusu hili la kutafutiwa mke.
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...VeraCity, hata mimi ningeweza rudisha nyuma miaka, ningewaomba dada zangu na kina mama ninaowajua wanisaidie kutauta mke atayenifaa... Haya mambo ya u-Girlfriend wengine wanaficha sana makucha yao bana...
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huko kutafutiwa ndio sijaelewa mchakato unavyokwenda,Ina maana wanakutambulisha au ndio wanafanya negotiations zote kwa niaba yako?
  Kuhusu kuficha makucha hata hawa wa kutafutiwa huweza kuficha.Isitoshe ukimtoa mtu kijijini akaja mjini ujue akishauzoea mji, kuna uwezekano akagundua hukuwa chaguo lake akakutoroka na kukuacha kwenye mataa.
   
  Last edited: Oct 5, 2009
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ukitafutiwa usishangae ukitafuniwa.
   
 9. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  VeraCity kwa nini umebadilisha jina bana? Mimi nilikuwa nashinda kupekenyua tu mabandiko yako. Sasa hili jina jipya lilinifanya unipige chenga kidogo. Lakini mzungu si athumani nimekukamata....

  Mada husika....

  Kuna sababu nyingi zinazoweza kumfanya mwanaume akabidhi mtu mwingine zoezi la utafuta mke:
  1) Kutojua mbinu za kusogea karibu kwa wadada
  2) Kutokuwa na muda wa kusogea karibu kwa wadada
  3) Kuvunjika moyo na kukata tamaa na mambo ya mapenzi
  4) Mila na desturi za ukoo
  5) Nk nk
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Lol!
  Basi kauka ivo ivo!!!
  Asante kwa mchango wako.Mimi nimejikuta nakabiliwa na wakati mgumu pia pale mtu anapokuomba kabisa kuwa naomba unitafutie mchumba maana naogopa likija kuharibika lawama nitabebeshwa.Yakinyooka basi hapo ni kicheko.Dhamana ya kumtafutia mtu mchumba ni kubwa mno na siyo kitu kidogo eti!Fikiria umemtafutia mtu halafu anakuja kulikwaa gonjwa la UKIMWI!
   
 11. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Katika ndoa kuna kitu muhimu ambacho ni kuendana kitabia, ikiwa umetafutiwa mke bila kujua tabia zake kuna hatari ndoa itakuwa na kugombanagombana kila siku kama tabia zenu haziowani.
  Mimi siafiki mtu kuchaguliwa Mke ila naelewa kwa nini wanaume hasa wale waliokwisha kuwahi kuoa na kuacha hupendelea ndugu zao wachague mke huko vijijini.
  Mara nyingi hawa wachumba wa vijijini wana heshima na kwakweli wana malezi na hufunzwa kuheshimu mume na wazazi. Hata kama ukimkuta na tabia za kishamba inakuwa ni rahisi kumrekebisha aende vile unavopenda wewe mume. Hawa wanakuwa wanatii amri za mume,na sababu nyengine ni fitina za mjini, asilimia kubwa ya wanawake wa mjini si kutwa ukakuta wana historia ambayo mara nyingi hata ukimuomba akueleze ukweli atakuficha, matokeo unakatiza mitaa watu waakudiscuss . Huyu wa kijijini hawamjui na hakuna atakaekuja na uzushi wowote, na asilimia kubwa ya hawa kuku wa kienyeji mchinjaji unakuwa wewe mwenyewe, kwahio unakuwa umeua uzushi.
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  nimekusoma = wanaotaka kutafutiwa wanahitaji heshima, utii na kuwa wa kwanza....
  Sasa ndugu yangu inategemea ni vijiji vipi maana kuna vijiji navijua mie, hakuna tofauti na mijini.
  Na je, muoaji naye yuko tayari kutoa heshima, na kuwa mtiifu na mwaminifu au ni upande mmoja tu?
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...la hasha!

  kutafutiwa ninakomaanisha mimi ni ...

  -Unawaeleza (wapelelezi wako) dada/mama zako unataka mke wa aina gani; i.e -umri, -tabia, -wajihi/maumbile, -elimu, -nk...Wao wanagawana majukumu nyumba zipi wakachungue binti anayefaa au anayekaribiana na vigezo.

  -Wanakuletea feedback ya uchunguzi wao, i.e mabinti waliofanikiwa kukidhi vigezo, kisha mnakaa chini kuwajadili na wewe unachagua yupi anayeonekana ana mvuto zaidi kwako.

  -Unawatuma wakusanye nguvu na busara kumshawishi huyo binti awe mchumba'ko... kisha posa inapelekwa, ...kisha mahari, ..harusi, halafu unajilia 'honeymoon' ya kiukweli ukweli.... :D

  Japo waswahili husema 'heri ya jini likujualo' lakini kwa muono wangu naona hilo jini likujualo ni disappointment tosha likijabadilika tabia baada ya kuliweka ndani kuliko huyu mpyaaaaaa (wa kutafutiwa) ambaye wote mnaanzana na tabia zenu mpyaaaa!
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huenda kuna uzuri wake..... kama unatoa vigezo vyako na hatimaye kufanya uchaguzi, basi safi sana hiyo!
   
 15. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  I too like Quemu prefer WoS:D
  Kweli kuna vijiji ni afadhali ya mjini, sio kwamba wa vijijini wote wana tabia nzuri ndio nikasema asilimia kubwa = sio wote.
  Na sio jambo la kupingika kwamba "women knows better about women", m/ke anaweza kumsoma m/ke mwenzie within days tofauti na wanaume, na ndio sababu mtu huamua kumtumia dada/mama kwa uzoefu/umakini wao.
  Nadhani mara nyingi ikiwa mouaji kaamua kuwashirikisha wazazi kuchagua mke anakuwa tayari kutoa heshima, kwani kama angalikuwa hachukulii serious na kuchelea kuwapa aibu dada/mama asingechukua hatua hii, angalitafuta mitaani mwenyewe.
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  Mtu yoyote yule awe mwanamke au mwanaume ana paswa kutafuta mwenza wake mwenyewe. Ukitafutiwa mke na mtu mwingine huyo mtu ata kutafutia mwanamke kwa kulingana na preference zake na si zako. Bora tafuta mwenyewe anaye kupindeza ili mwisho wa siku usianze kulaumu kuwa umetafutiwa mke ambae siyo. Na siku hizi siyo kama zamani. Hakuna atakaye vumilia ndoa na mtu asiye mpenda kisa tu ime pangwa na familia.


  By the way ukisha letea mwanamke na usimpendee uta tafutiwa wangapi? Si chanzo cha kuonekana mhuni tu?
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  mhhh!! Interesting aspect.
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  A woman knows better about a woman but a man knows better about the woman that will suit him. Mama ako aki kuchagulia mke basi ata kuchagulia mwanamke ambae anafanana na yeye(yani mama ako) na dada ako aki kuchagulia mke basi ata chagua mtu ambae ana sifa za kuwa rafiki yake. What is common in both scenarios? Hakuna atakae kuchagulia mke kutokana na unacho penda wewe.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,851
  Likes Received: 83,275
  Trophy Points: 280
  Hii kali unaweza kujuta for the rest of your life..GOD FORBID!
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,851
  Likes Received: 83,275
  Trophy Points: 280

  Especially kwa wanaume inabidi uchakarike kivyako vyako tu, uweke criteria za mke wa namna gani ikiwemo elimu yake, kazi na vigezo vingine. Kama uko serious na hutaki kutest wanawake wanne au watano zaidi kabla ya kumake your final decision lazima utampata tu.
   
Loading...