Je,unasumbuliwa na shimo la choo kujaa maji?

Simbamteme

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
784
2,063
Kwa wale wenzangu na mm tuliojenga vibanda vyetu sehemu ambayo water level ipo juu sana,hii inakuhusu..

Mbinu hii alinipa fundi mmoja hivi..Mimi nilikuwa nasumbuliwa na hii hali kwa karibu miaka zaidi ya 3..yani kila baada ya miezi kadhaa ilikuwa ni lazima niwaite watu wa kuvuta maji taka waje kuvuta uchafu shimoni..sasa kama ww umeshajenga shimo tayari(haya local)na hautaki kuingia gharama ya kujenga mashimo haya ya kisasa ambayo gharama zake ni kubwa kidogo..hii ni simple solution

Kwa kawaida maji ambayo yapo kwenye mkondo(chini)huwa hayawezi kupanda juu kuzidi level ya ardhi(labda kuwe na chem chem kali)..wale tuliotumia maji ya visima vya kuchimbwa watanielewa..hata mvua iwe kubwa vipi,maji hayawezi kujaa mpaka kutoka nje ya kisima

So cha kufanya,bomoa shimo lako,ile sehemu iliyopigwa zege..pandisha shimo lako juu centimeter kuanzia 60(rula 2) mpk 70 au 80 kutoka usawa wa ardhi then piga zege upya..then bomba linalotema maji shimoni kutoka kwenye chemba liweke kwa mtindo wa kutema kupitia juu ya shimo na sio pembeni ya shimo....baada ya hapo maji hata siku moja hayawezi kujaa hadi kufikia level ya kurudisha maji kwenye chemba!!

Mimi nilifanya hivyo b4 mvua za dar zilizoisha hv karibuni na tatizo halijajirudia tena mpk leo!!

Kama kuna mdau ana mbinu nyingine isiyo na gharama sanaaa karibu tushee ideas

Adios
 
Ukitaka usinyonye mavi chimba shimo lako jengea baada kujenga kabla ujafunika chukua tipa moja ya mawe mimina ktk shimo funika endelea na maisha yako utoita nyonya mavi!
 
Back
Top Bottom