je unampenda aliyependwa? fanya yafuatayo...!!!

Mr.Thinker

Senior Member
Dec 13, 2013
125
137
Habari zenu wakuu!!
tuzungumzie kumpenda aliyependwa, Kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii wala kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa msichana ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndio umeshapenda.
Hayo ndiyo mapenzi jamani!, mwanaume unaweza kujikuta unaangukia kwa msichana ambaye tayari ana mpenzi wake yaani ameshapendwa. Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?

Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kama yafuatayoo
Kwanza… Chunguza
Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye future naye.
Pili… Usitafute uadui
Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko‘serious’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.
Tatu… Una nafasi kwake?
Sawa umetokea kumpenda msichana/Mvulana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi
anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.
Nne… Ni rahisi kubadili uamuzi wake?
Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.
Tano… Pingana na moyo wako

Ifike wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na mwanamke/mwanamme ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.
 
Hawa watu mkuu siku hz wamebadilika sana. utamu wao umehamia kwenye pochi zao, ukizijaza pochi zao kwa hela utamu mwanaume unakuwa mtamu.

mapenzi yao yamehamia kwenye macho ya kuona vitu <materials>. ukiwa na dalili ya kufulia mapenzi yanahama.
 
Kama sio yako sio yako tu kama ana mtu tafuta mwingine vinginevyo utajikuta unapoteza mda wako bure na utaumia kila siku unaona demu anaingizwa geto kila siku mlaango unafungwa uku ni kujitafutia magonjwa yamoyo bure
 
kweli kbs
 
Hawa watu mkuu siku hz wamebadilika sana. utamu wao umehamia kwenye pochi zao, ukizijaza pochi zao kwa hela utamu mwanaume unakuwa mtamu.

mapenzi yao yamehamia kwenye macho ya kuona vitu <materials>. ukiwa na dalili ya kufulia mapenzi yanahama.
Yeah!! hali hiyo ipo kbs, lkn kuna masalia ya wanawake wachache wenye mapenzi ya kweli
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom