Je unamjua Gaurav Tiwari Bingwa wa kusuluhisha masuala ya Utata wa kiroho

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,500
1,930
Habarini za mchana wakuu.
Nitawaletea kidogo habari kuhusu huyu bwana mdogo kutoka india ambaye dunia imepata kuona mchango wake katika masuala ya kuchunguza ishu za Kiroho pamoja na Hali zilizo na utata karibuni.

Gaurav Tiwari alizaliwa tarehe 2 Septemba 1984 na kufariki mwaka 2016 tarehe 7 mwezi julai. Alizaliwa katika familia ya Kihindu familia yeye kufuata malezi na maswala yote ya kidini ya Kihindu. Ijapokuwa alikuwa na elimu ya urubani lakini kabla alikuwa ana ndoto ya kuwa mwigizaji pamoja na msanii. Hii sio kitu kigeni kusikia kutoka kwa Wahindi. Lakini alipokuwa anasomea urubani aliwasikia rafiki zake wakiongea kuhusu masuala ya kukutana na mauzauza pamoja na vitu vya kuogofya. Hii ilimpelekea kubadili maamuzi ya kuendelea na taaluma yake ya urubani kwani baada ya kuhitimu tu aliingia katika imani ya kutaka kuwa mvumbuzi wa masuluhisho yanayowasumbua wanajamii wake. Hii pia ilimpelekea kutoka katika imani yake na kuanza kutafuta maarifa zaidi kuhusu maisha ya mwanadamu pamoja na haera kwa ujumla. Kupitia chama cha Paranexus Association of USA kilichopo Marekani alipata nafasi ya kuwa mmoja katika ya wahitimu walio tayari kuanza kufuatilia mambo haya pamoja na kutafuta suluhisho.
Mwaka 2009 alirudi kwao India na kuanza kusaidia watu katika mambo ya kuona Mapepo na hata hali zenye utata sana hasa nyakati za usiku au uwepo wa giza.
Chanzo kimoja cha India linadai kuwa alisaidia kutatua kesi za namna hiyo zaidi ya 50 kwa ufasaha kabisa yaani kupata suluhu zao.
Tatizo lililompa jina kubwa sana India baada ya kulichunguza lilikuwa ni pale ambapo aliweza hata kuzitolea ufumbuzi picha ambazo kwa hali ya kawaida zilikuwa hazina maana ila ukitazama kwa umakini huyu jamaa aliweza mpaka kutoka na ishara hata zaidi ya tano kutoka katika picha moja tu.
Alipata umaarufu mkubwa sana ndani na hata nje ya india. Mpaka kufikia kuitwa katika mahojiano makubwa kama Mtv India na Paranomal Society Channel. Msukumo pekee wa Gaurav ilikuwa ni kuwapa elimu na kutoa msaada kwa dunia kuhusu masuala haya yenye kuumiza kichwa sana.
Kifo chake:
Tarehe 7 Julai Bwana Mdogo Gaurav alikuwa akioga ila ghafla kulikisikia kelele na wanafamilia walipokwenda kuangalia ni nini kilichomsibu wakakuta mlango umejifunga kwa ndani hivyo walivunja na kuingia ndani ila kwa bahati mbaya walikumkuta kijana wao akiwa hana fahamu zake huku akiwa amelala sakafuni. Walipomuangalia waliona alama shingoni kama mtu aliyenyongwa vile. Walipojaribu kumuwaisha hospitali alikuwa ameshafariki. Hii ni kwa mujibu wa familia yake. https://en.m.wikipedia.org/wiki/Gaurav_Tiwari#cite_ref-1
Kuna watu mbalimbali wanaodhani kuwa kifo cha huyu bwana haikuwa bahati mbaya kwani kinaweza kuwa ni mshahara wake wa kupeleka pua huko.
Asante sana.
I Stand to be corrected anywhere where.
FB_IMG_15546290547470968.jpg
FB_IMG_15546290043635262.jpg
Screenshot_20190407-122358.jpg
Screenshot_20190407-122340.jpg
Screenshot_20190407-122444.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wanaofanya hivi hasa ni kina nani? au ni nguvu za Giza tu kama mizimu au uchawi na kama ni hivyo huyu jamaa si alisomea kabisa kwa maana alijua pia namna ya kujilinda katika kazi yake?
Inaaminika kuwa ni mishe za Paranormal ndo zimemtoa kwenye mstari maana alikuwa anawaumbua wanaohusika na hizi mambo kwa ufasaha mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wanaofanya hivi hasa ni kina nani? au ni nguvu za Giza tu kama mizimu au uchawi na kama ni hivyo huyu jamaa si alisomea kabisa kwa maana alijua pia namna ya kujilinda katika kazi yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli alisomea namna ya encounter nzima ya ghosts pia na ishu ya paranormal activities ila inaonekana alikuwa ni mwiba mchungu kwao kwani alitoa mpaka msaada for free tu ila lengo kubwa ni kufichua mambo yote hayo.
Maiti yake ilikuwa na kimstari kidogo cheusi shingoni kumaanisha kuwa alinyongwa ila sasa wash room ilipo ilikuwa ni ghorofani na hakukuwa na mtu aliyeweza kuingia kwa urahisi ndo maana Wengibe Wanasema kuwa ilikuwa ni mbinu ya kumtoa nje ya mstari tu

Noma

ndo maana Wengibe Wanasema kuwa ilikuwa ni mbinu ya kumtoa nje ya mstari tu

Mkuu huo mstari sijauelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rafiki yake na Tiwari anataka kuanza kuchunguza ni nini haswa kilichomuua rafiki yake ijapokuwa amekatazwa na baadhi ya ndugu zake na Gaurav. Je kuna kitu nyuma ya pazia??????
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom