barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
PICHA: Mnyama Nyegere
PICHA: Mtu aliyedhuriwa na mnyama Nyegere
PICHA: Nyegere akipambana na Simba
Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani. Chakula chake kikubwa ni asali,yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula. Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma hakuna chochote kinatokea
Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike
Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke,mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake(ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii.
Nyegere ndio mmoja kati ya "fearless animal" duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda,anasaidiwa na ngozi yake ngumu na kucha zake, awapo katika hatari ya kushambuliwa hukakamaa na ngozi yake kuwa ngumu kama "defensive mechanism" yake.
Kuna makabila ambayo waganga wa kienyeji hutumia mchanganyiko wa Nyegere kutengenezea limbwata,Yaani wamama huchukua dawa hiyo kuwawekea waume zao ili wawe na "upendo" wa Nyegere.
Wivu wa Nyegere hufanya awachukie sana binadamu wanaume,mwanaume ukiwa porini ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano, huona wivu kuwa utamtamani jike,hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.
Nyegere hula nyoka wa aina yoyote,ana sumu kali ambayo akimng'ata nyoka wa aina yoyote haponi.
Ogopa sana kukutana na mnyama mwenye wivu Nyegere...
Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja, akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya.
ZAIDI TAZAMA HAPA
===
MICHANGO YA WADAU KUHUSU MNYAMA HUYU
1.Ni mnyama mdogo anayekula nyoka, kenge, majani, matunda, kenge, mizoga ya binadamu, chui, simba, duma, ndege n.k...kwa kifupi anakula kila kitu
2.ngozi yake ni ngumu sana kiasi kwamba mishale na mikuki au risasi ni ngumu kupenya..ukitaka kumuua ni kumpiga katika fuvu la kichwa chake na kitu kizito au risasi kichwani,
3.katika guines world book of records yeye ndio the most fearless creature on the planet
4.mwili wake haudhuriki na sumu ya nyoka wa kawaida na ikitokea ameumwa na nyoka mwenye sumu kali na sumu ikapenya kwenye damu yake itamfanya alale kwa masaa kadhaa tu kisha ataendelea na mambo yake
5.Ana meno makali/magumu sana yenye uwezo wa kupasua hata jumba la kobe
6.Ashawahi kukutwa akipigana na simba na hata tembo na vifaru katika nyakati tofauti
7.Anapenda kula asali, huwa anaupulizia hewa chafu mzinga na nyuki wote kulewa hivyo kula asali na kuondoka zake
8.Ni vigimu kumshambulia kwani ngozi yake inamfanya iwe rahisi kwake kujikaza na kujizungusha katika upande wowote anaotaka na kukujeruhi.
9.Ni mvivu katika maswala ya nyumba yake hivyo basi anapojisikia uvivu hujilaza sehemu yoyote inayomfaa..ishaonekana akiwa kajiliza katika pango la mbwa mwitu kama kwake.
Mengine angalia link ya youtube nimekuwekea chini
---
---
Fuata hiyo link kuju ukweli wa mnyama huyo bila chumvi.
---
---Ha ha ha ha ha jamani huyo Nyegere wacha habari zake kabisaaa, huyo mimi nilikutana nae kwa Bibi huko sehemu za Iringa,nikiwa bwana mdogo nimeenda likizo,sasa babu akawa amenambia twende na watoto wa kina shangazi na baba mdogo kuchunga
Tukakutana nako huko porini..maana mi nilikuwa napenda sana asali,sbb nimetoka town kila mtu ananipenda na anataka kuonyesha mwamba,tumeenda tumekuta asali tukapakuwa,tumeenda jua linazama tunarudi zetu kunywesha ng'ombe maji
Ee bwana ee, kumbe kijamaa kinatufatilia nyumanyuma muda mrefu...tumefika home tukasikia mbwa wanalia sana nyuma ya zizi,kwenda tunakuta mbwa wamekula sana kichapo...palikuwa na varangati la kufa mtu,yaani ukongwe wa babu tu ,akasema "Beee mele taa ikisonzo kilipanzingo ipo"
Babu alikuwa mfugaji na mwindaji, akavaa ngozi ngumu kiunoni, akaanza kukabliana nako....It was a fighting of one hr and ahalf
Jamani huyu mdudu msikieni tu, kwanza mbishi halafu mgumu sana kufa...yaani sitaki hata kumkumbuka
---Habari wakuu, Leo katika pita pita zangu nikakutana na post MTU kapost hiki kimnyama akasema kinaitwa NYEGERA ila suala kwangu halipo kwenye jina lake, suala lipo katika mojawapo ya sifa nilizoziona kuwa ni balaa hata kuliko simba yaani eti ukikutana nako ni balaa
Jaman kwa wajuaji wa haka kadude ni kweli? Au ni figisu tu za kutaka kukapaisha maana haingii akilini kidudu kidogo kama hiki kimtoe jasho mwanaume wa bariadi labda wa dar
View attachment 1411898View attachment 1411899
Nyegere , melesi au mhilu ( Mellivora capensis) ni mnyama mdogo wa familia Mustelidae anayetokea Afrika, Mashariki ya Kati na Uhindi .
Nyegere huishi peke yao kwenye shimo analolichimba yeye mwenyewe.
Ni wachimbaji wazuri sana. Vile vidole vyao vyenye kucha ndefu na ngumu humsaidia sana kwenye kazi hii. Hata kama ardhi ni ngumu sana, ana uwezo wa kuchimba shimo linalomtosha kujificha katika kipindi kinachokadiriwa kuwa ni dakika kumi tu.
NYEGERE (Honey burger) a.k.a "The fearless animal" TABIA NA MAMBO YAKE MENGINE Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari, maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere, anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke, mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake (ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii.
Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja, akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi
porini kimya kimya Ni mnyama mdogo anayekula nyoka , kenge, majani, matunda, kenge, mizoga ya binadamu, chui, simba, duma, ndege n.k...kwa kifupi anakula kila kitu na ngozi yake ni ngumu sana kiasi kwamba mishale na mikuki au risasi ni ngumu kupenya..ukitaka kumuua ni kumpiga katika fuvu la kichwa chake na kitu kizito au risasi kichwani,
katika guines world book of records yeye ndio the most fearless creature on the planet mwili wake haudhuriki na sumu ya nyoka wa kawaida na ikitokea ameumwa na nyoka mwenye sumu kali na sumu ikapenya kwenye damu yake itamfanya alale kwa masaa kadhaa tu kisha ataendelea na mambo yake.
Ana meno makali/magumu sana yenye uwezo wa kupasua hata jumba la kobe. .Ashawahi kukutwa akipigana na simba na hata tembo na vifaru katika nyakati tofauti. Ni mvivu katika maswala ya nyumba yake hivyo basi anapojisikia uvivu hujilaza sehemu yoyote inayomfaa..ishaonekana akiwa kajiliza katika pango la mbwa mwitu kama kwake. Wanapatikana India ,Kusini magharibi barani Asia na Afrika.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyegere kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari .