Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 18,589
- 20,895
AZIZ ALI DOSSA KIDONYO-MMOJA WA WAAFRIKA MATAJIRI WAKATI WA UKOLONI NCHINI TANGANYIKA
AZIZ Ali alijitengenezea umaarufu Kutokana na kwamba aliweza kumiliki majumba mengi na magari ya biashara ( yaani malori ya mchanga) pamoja na ya kutembelea na vitu vingine kadhaa, kutokana na kazi yake ya kuwa mtaalamu wa kujenga ( Building Contractor).
Hili jina la Aziz Ali alipewa na watu wa Dar es salaam kwa hisani na wema wake ,alikuwa ni tajiri na Contractor wa kujenga nyumba na mwafrika wa kwanza kununua magari na kujenga nyumba ya vigae na vioo mtoni.
Aziz Ali alikuwa ni mdigo aliyetokea sehemu za Tanga na kuja kuweka kambi mjini Mzizima ( sasa Dar es salaam) mwanzo wa vita kuu ya kwanza ya dunia (1914-1918) akiwa askari katika jeshi la wajerumani na baada ya vita aliajiriwa na Goa mmoja.
Mwajiri wake huyo alipoondoka nchini alimwachia Aziz Ali gari mbili na hizi ndizo alizoanzia kufanyia biashara hapo mwanzo na kufungua kampuni ya ujenzi na kuajiri Mafundi kadhaa. Mwezi wa Ramadhani milango ya nyumba yake ilikuwa wazi kuwahudumia kwa futari mamia ya watu, Temeke imehifadhi jina lake kwa eneo moja la "Mtoni kwa Aziz Ali).
Kwenye Nyumba zake alikuwa akitoa fursa kwa watu kumpa pesa kidogo kidogo kama malipo ya nyumba alizokuwa anawajengea na alikuwa mtu akishindwa kulipa alimpa muda hadi atakapoweza, Nyumbani kwake mwezi mtukufu wa Ramadhani alikuwa akitandika majamvi nje na kufuturisha hadi watu 100 asiowajua wakija wanafuturu na kuondoka.
Nyumba hii hadi leo ipo na sehemu hiyo kando kando ya barabara ya Kilwa na ndipo hapo pakaja kuitwa Mtoni kwa Aziz Ali. Lakini katika sifa yake kubwa sana Aziz Ali alikuwa akifanya ujenzi wa misikiti na kuihudumia misikiti hii ilikuwa miaka ya 1930 na hapakuwa na umeme kariakoo, Misikiti ilikuwa ikitumia karabai kuonea, Aziz Ali yeye alinunua karabai kwa kila msikiti na ikifika magharibi mwanae Hamza alikuwa akizitia mafuta na kuziwasha kisha akizipeleka kila msikiti tayari kwa sala ya Magharibi.
Inapomalizika sala ya Isha alikuwa anapita tena katika ile misikiti kukusanya karabai zake na kurudi nazo nyumbani kwao Mtaa wa Mbaruku na Kongo. Mzee Aziz Ali alikuwa na nyumba nyingi sana Dar es salaam, na ndiyo zilikuwa moja ya utajiri wake, katika nyumba hizo nyumba ya mtaa wa mbaruku na Kongo, nyumba hii ilikuwa moja ya sehemu ambazo harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika zilianzia hapo, nyumba nyingine ilikuwa mtaa wa Kipata kwa Ally Sykes, hapo zamani lilipokuwa duka la baba yake na baraza la wazee.
Nyumba nyingine ilikuwa Stanley Street, kwa Abdul Sykes ,Nyumba hii ilikuwa pia ya Kleist na kulikuwa na duka la vifaa vya ujenzi katika uhai wake. Mzee Aziz Ali alitoa mchango mkubwa sana katika harakati za Uhuru wa nchi hii, kwa kujitolea mali zake na nguvu zake mfanyabiashara aliyemiliki kampuni ya ujenzi wa nyumba nyingi tu mjini mitaa ya kariakoo, yeye alikuwa amezijenga tena kwa kumlipa kidogo na baadaye kummalizia malipo yake kwa makubaliano maalum na wala hajawahi kuishtaki mtu kwa kumcheleweshea malipo yake.
Ndipo Kutokana na ukarimu wake mkubwa wakamwita "Aziz" yaani "kipenzi" ikawa wakimtaja jina wanatanguliza " Aziz" yaani *kipenzi chetu Ali" kiasi kwamba ikapelekea jina la kidonyo kufa kabisa kwa hakika Aziz Ali alikuwa ncha Mungu sana. Alipokufa mwaka 1951 miaka miwili baada ya kifo cha rafiki yake Kleist Gazeti la "Tanganyika Standard "liliandika kifo chake kwa Maneno haya " Aziz Ali the builder of mosques is dead; yaani Aziz Ali mjenzi wa misikiti amefariki".
Alipofariki mzee Aziz Ali, biashara zake ziliendelezwa na mmoja wa watoto zake Dossa Aziz Ali, na hata zile harakati za Uhuru alijihusisha nazo tena kwa undani zaidi, Hii ilikuwa mwanzoni mwa 1950, Mambo yalipamba moto sana kuanzia mwaka huo pale Vijana wazalendo walipoanza kufanya mipango ya kuunda chama cha siasa halisi kupambana na ukoloni wa Muingereza.
Nyumba zilizokuwa anamiliki Mzee Aziz Ali ndizo zikawa nyumba ambazo Nyerere alikuwa akifikia kuanzia mwaka 1952 kila anapokuja mjini kutokea Pugu alipokuwa akifundisha Dossa alikuwemo Katika kuasisi vyombo vyote vya mwanzo vinavyonasibishwa na harakati za kumng'oa mkoloni kama vike TAA na TANU akiwa Afisa na mjumbe mwandamizi aliye na sauti hili sawa hili Fanya, hili wacha, na mambo yakawa hivyo asemavyo.
Dossa kwa kushirikiana na mwanachama mwingine Alexander Tobias walichaguliwa na wenzao wakati fulani wawe makatibu wa pamoja wa muhtasari .harakati ziliposuasua alikuwa hachoki kuwapitia wenzake na kuwakumbusha majukumu waliyopewa akienda kwa mmoja mmoja nyumbani kwake kwa kutumia gari lake na kutaka kujua kulikoni mambo hayaendi ipasavyo.
Katika Sikuwa mwanzo harakati ,chama cha TAA na baadaye TANU havikuwa na uwezo wa kifedha wa kujiendesha mambo yote hata kidogo Tegemeo lao kubwa lilikuwa ni kwa watu kama akina Dossa Aziz, aliyekuwa Mkurugenzi na msimamizi Mkuu wa biashara na mali za babake ,wengine ni Mzee John Rupia ,na wale akina Sykes watatu, Abdul ,Ally na Abbas, ambao baba zao walikuwa na uwezo wa fedha ,wawapige jeki ,wachangie pakubwa.
Habari zinasema ilikuwa ni Dossa Aziz aliyemwomba Nyerere kuacha tena kuvaa kaptula mbele ya wazee, kwani sasa ameshakuwa kiongozi ambaye atakuwa akikutana na watu wazima na hivyo si vizuri kuonekana na Kaptula na Stockings ( zile soksi ndefu mpaka kwenye magoti). Mzee Dossa alifanikiwa katika hilo kwani alimnunulia pia Nyerere suti kadhaa, maridadi katika ile safari yake ya kibali.
UNO Umoja wa Mataifa (wakati ule) ili kupeleka kilimo cha Watanganyika kudai Uhuru.