Je Unamfahamu Adam Nditi Mzanzibar wa Chelsea?

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Hizi ni taarifa zilizopo katika tovuti ya Chelsea

0,,10268%7E11272385,00.jpg

Adam Nditi,

Born on 18 September 1994 in Zanzibar, Tanzania, Adam arrived at Chelsea as an Under-13 and can play either left-back or left-wing. It was the more defensive of those roles he filled as the FA Youth Cup was captured in 2012. He was joint-highest youth league appearance maker and played four games for the reserves in 2011/12, his first full-time season which led to a professional contract.

As a schoolboy he amassed 27 youth team appearances, and featured regularly during the 2011 FA Youth Cup run to the semi-final.
Adam Nditi | Standard Article | Official Site | Chelsea Football Club

Hii imekuwa kasumba kwa Watz wengi kwenda nje na kujichimbia huko. Je we kama mdau wa michezo tufanyeje ili kupata wachezaji hao?
 
Uzalendo hauji vivi hivi tu, unajengwa from the root. Na kuna uhusiano na hali ya siasa ya nchi, we unafikiri kama ungekuwa wewe ungerudi kutumikia nchi inayoliwa na wachache?
 
Shirikisho la mpira nchini linayo fursa na wajibu wa kufuatilia wachezaji wa Tz wanaocheza nchi za kigeni, ona kama tulvyowakosa akina Patrick Mtiliga na wengine
 
Shirikisho la mpira nchini linayo fursa na wajibu wa kufuatilia wachezaji wa Tz wanaocheza nchi za kigeni, ona kama tulvyowakosa akina Patrick Mtiliga na wengine

Ali Hafif wa Qatar, yuko on fire ajabu, ana mguu wa kushoto ambao uko powerful ajabu na anaweza kufunga kutokea point ngumu ya uwanja.
Tumemkosa hivyo, tuko na uongozi hopeless kwenye soka, halafu Ashford Mamelodi anakuja kutuambia kuwa tuna bonge la rais.
 
hivi angelikuwa bado yupo bongo angeliweza cheza kama alivyo? Huyo wala harudi kuja kucheza viwanja vya visivyokuwa na standard ukiondoa uwanja wa Taifa wapi kwengine ataweza uki slide unapata majeraha, kama mimi sirudi hata kuja tembea
 
Wabongo kwa kupenda sifa, kwani amefanya nini mpaka atambulike sasa? Chapeni kazi kwanza.
 
Shirikisho la mpira nchini linayo fursa na wajibu wa kufuatilia wachezaji wa Tz wanaocheza nchi za kigeni, ona kama tulvyowakosa akina Patrick Mtiliga na wengine

Mtiliga garasa 2 labda hafif na nditi.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
huyu akija tu huku kapoteza kazi yake halafu chengine mbona kina samatta wakuja cecafa na hamja lalama huyu dogo muacheni ajinafasi ndio zali lake hilo..
 
Wanatami aje wampige juju wafanane kiumaskini kama wao

wabongo roho mbaya sana
 
"Mzanzibari" anayekipiga Chelsea kwa nini sio "Mtanzania" anayekipiga Chelsea?

Nami mkuu niliwaza hilo sikupata jibu la haraka. Kwa hiyo Haffif naye tumuite Mdar es salaam anayekipiga uarabuni,au Sammata uLIMWENGU na Mgosi nao tuwaite Wadar es salaam wanaokipiga Congo..1 ina swihi hii kweli...?
 
Zanzibar ni nchi mkuu, ina bendera, wimbo wa taifa na mamlaka yake kamili. Huwezi kuifananisha na Dar...
 
Abaki hukohuko... asijifanye mzalendo sana.. bongo atapoteza tu!
 
Back
Top Bottom