Je unakumbuka ulipokua shule ulikua na cheo gani? Na faida ya hicho cheo ni ipi?

Primary nilikuwa monitor na kiranja nikiwa darasa la tatu,faida ni kuwa exempted kwenye kazi za shuleni hasa kilimo na usafi,pia nilibahatika kuwa mjumbe wa kamati ya shule kuwakilisha wanafunzi wenzetu tukawa tunapokea posho ya vikao kama wajumbe wengine,hasara ni kupigana au kupigwa ngumi na wababe waliokuwa wananizidi ngumi huo ndio ulikuwa ugumu wa kazi unapokuja.
 
Primary nilikuwa monitor darasa la 3 kwa kuteuliwa. Huwezi amini nilikuwa nachapa wapiga kelele na nilikuwa naona ni sahihi kabisa. Kuna muda nilikuwa naamuru walale wakikosa la kusoma (shule ya vidumu na mifagio)

Darasa la 4 nikawa kiranja nikapelekesha wasumbufu vilevile. La 5 mwishoni nikawa HP

Form 1 nikawa monitor kwa vile nilisoma vizuri sana pre-form one na nilikuwa najua. Form 2 nikawa store keeper, ni kazi inataka uaminifu na record keeping, then nikawa environmental prefect. Form 3 HP

A Level kiongozi flani hivi badge ya rank ya mwisho. Chuo nachezea kamati ya uchaguzi. Kwanza uku wanapitishwa watu kabla ya kupiga kura. Mimi ni adui wa siasa

Dini nimeshika nafasi kadhaa na kuwa kaka wa madogo kibao, nina vyeti vya dini kuliko kwingine. Viongozi wengi wa dini wanafeli au huwa wanasoma Edu
duh hongera bhana
 
'O' level sikuwa na cheo chochote ila Advance nilikua health prefect Kilinisaidia sana sababu nilikua mhusika pekee wa kusindikiza wagonjwa hospitali na shule ilikua ni boarding so ilikua haipiti wiki mimi niko mjini... napeleka mgonjwa hospitali afu naenda mjini kukata mitaa.
aaaah hiyo ilikua chance
 
Tangu chekechea nilikuwa kiongozi primary school nikawa monitor secondary school nikawa kiongozi wa chakula na baadae nikamalizia kuwa kiranja mkuu(HP).
 
Nilkua Monitor wa darasa kwa miaka miwili o-lever....3" 4

Bhas tu darasa lilinipenda sikua mkudaa sanaa wala msongo sanaa

Kwanza wahuni wote nilikua nawamudu!!!!
Japo totoz!! Nilizila"" siunajua tena Usmart!!!!!

Lakin nadhan hii nyota huwa haifi ni karibia kila sehem...napata kaupepo ka kua kiongoz fulan hiv!!
 
Nilichaguliwa umonitor na mwalimu wa darasa kwa sababu ya kufanya vizuri somo lake.

Noma ikaja nilikuwa ndo naongoza kwa kupiga kelele darasani, kwa hiyo nikawa na mimi najiandika kwenye majina baadhi ya siku.

Nikaondolewa.

Faida siikumbuki.

Hasara: watu wakigombana class monitor pia unachapwa eti hukuwaamua.
Hahaha! Kujiandika noma!
Ulitisha kulipa fadhila za wapigaji kelele
 
Nilkua Monter wa darasa kwa miaka miwili o-lever....3" 4

Bhas tu darasa lilinipenda sikua mkudaa sanaa wala msongo sanaa

Kwanza wahuni wote nilikua nawamudu!!!!
Japo totoz!! Nilizila"" siunajua tena Usmart!!!!!

Lakin nadhan hii nyota huwa haifi ni karibia kila sehem...napata kaupepo ka kua kiongoz fulan hiv!!
hicho ni kibali ulichonacho toka kwa Mungu
 
Nakumbuka uboyizini tulikua na monitor na msaidizi wake ambaye tulimuita Monitress japo alikuwa me
 
Back
Top Bottom