Je Unakumbuka Ulimpataje/Mlikutanaje na Mpenzi/mke/mme wako?

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,145
13,216
Watu hukutana na kufahamiana kutokana na viunganishi mbalimbali, yaweza kuwa matukio, kupitia marafiki n.k

Hili la wapenzi/wanandoa kukutana nalo limekuwa na msisimko wa aina yake kutokana na simulizi mbalimbali, wapo wanaosema walikutana ofisini, shuleni, kwenye harusi, daladala nk, na wachache husimulia walianza anzanaje.

Je wewe unakumbuka ulikutana vipi na mpenzi/mwanandoa wako? pengine si bibaya ukatujuza zaidi ilikuwaje na mkaishiaje au mnaendeleaje hadi sasa....... hii itasaidia katika kujenga ujasiri kwa wengine humu.

Binafsi mpenzi wangu wa kwanza nilikutana naye nilipoenda kumuona bibi yangu aliyekuwa mgonjwa. Naye alikua amemsindikiza rafiki yake.

Ilitokea tu tukawa tunaangaliana sana na kwa bahati mbaya yule bibi alifariki na ikasaidia kuimarisha mahusiano kwani yule dada straight away aliniletea kadi.

Tulidumu miaka 4 kama marafiki tu mwishowe akaamua kufunga ndoa na mtu mwingine lakini bado tunawasiliana.
 
Ngoja nijaribu....

Shuleni ..primary.
Nje barabarani..
Studio..
Sokoni..
Kwenye party...
Hi5
Myspace
JF..
Kwenye daladala
Facebook
Kwenye pantoni...
Club..
JF

Skype? Whatsaap? MSN Messenger? Yahoo Messenger? Tagged? IKEA?
 
Timu ya Mpira na Risevu
Ngoja nijaribu....

Shuleni ..primary.
Nje barabarani..
Studio..
Sokoni..
Kwenye party...
Hi5
Myspace
JF..
Kwenye daladala
Facebook
Kwenye pantoni...
Club..
JF
 
Kwahiyo nia yako ni kuhukumu wenzio?! Hongera we ambae hata timu ya kucheza chess hujafikisha!
Ahhhhhh, Pole Lizzy....ni wazo tu lilinijia baada ya kufanya hesabu za haraka.............mimi nadhani najaza Hiace
 
Inaonekana umchangia bila kusoam thread?? changia mkuu usijali....hapa ni jukwaa la kubadilishana mawazo na kuliwazana....hebu fikiria unasishi naye na hili swali linakukumbusha historia...bila shaka hata kama mlikuwa na mikwaruzo usiku wa leo utajirudi kwa kutafakari jinsi mlivyokutana....hata kama ilikuwa ni NDOA YA JAMVI
Acha umbea. Nikikwambia itakusaidia nini?
 
Inaonekana umchangia bila kusoam thread?? changia mkuu usijali....hapa ni jukwaa la kubadilishana mawazo na kuliwazana....hebu fikiria unasishi naye na hili swali linakukumbusha historia...bila shaka hata kama mlikuwa na mikwaruzo usiku wa leo utajirudi kwa kutafakari jinsi mlivyokutana....hata kama ilikuwa ni NDOA YA JAMVI

Wengine waliwapora rafiki/shoga zao hao wenza walio nao.. Kwa hiyo kumbukumbu hiyo inawa-haunt hadi wanakuwa na wivu kupitiliza...
 
Hili nalo neno...

Kabisa Mwali...

Hataweza kusema tulikutana kwenye party.. Maana kwenye party alitambulishwa tu,na akaambiwa amkeep company maana yeye yuko busy...

Watu wa aina hii wanakuja kutake advantage kwenye scenario za namna hiyo..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom