Je, unakumbuka "Scaba-Scuba, Scaba Line", basi dogo lililokuwa ikifanya safari zake Dar es Salaam - Morogoro?

JBourne59

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
941
8,525
Je, unaikumbuka?

(Kwa waliozaliwa kuanzia enzi za utawala wa Mzee Mwinyi (Mzee wa Rukhsa si rahisi kukumbuka hili basi)

Ni lililokuwa basi dogo, ilikuwa ikifanya safari zake Dar Es Salaam - Morogoro.

Ni basi lililokuwa linaweza kufanya safari tatu kwa sita kwa siku moja Dar - Moro licha ya changamoto za barabara wakati huo.

Je, unakumbuka iliishia wapi?

Ni miongoni mwa mabasi machache ya abiria yaliyokuwa na radio / cassette player ndani ya gari, Safari na Muziki.

Stendi/Kituo chake kwa Dar wakati huo ilikuwa na Magomeni Mapipa (sikumbuki vizuri kama pia waliwahi kuwa pale Manzese baada ya kutoka Magomeni mapipa)

Ewe Mhenga mwenzangu, umekumbuka nini zaidi?

Karibuni.
 
Huyo SCUBA mwenyewe yuko wapi siku hizi? Hili jina linafanana na "Shkuba" yule muuza mihadharati aliye kuwa extradicted to USA!!
 
Scaba scuba, ilikuwa ni Mitsubishi Rosa nyekundu six cylinder. Enzi zile gari nyingi zikikuwa zikifanya safari 3 x 2. Kulikuwa na Camp Safari, Jongwe, El Sakran, Sansui, Accountant, Red Rooster, Cheetah, Uvikiuku, Selungwi, Wagala, Balhabou niishie tu hapo.
 
Shkuba hayo majina mbona yana element za utapeli? Si ndio huyo aliyekuwa anauza Ngada? Scuba na magari wapi na wapi? Scuba si Hardware na Fremu tu?
 
Scaba scuba, ilikuwa ni Mitsubishi Rosa nyekundu six cylinder. Enzi zile gari nyingi zikikuwa zikifanya safari 3 x 2. Kulikuwa na Camp Safari, Jongwe, El Sakran, Sansui, Accountant, Red Rooster, Cheetah, Uvikiuku, Selungwi, Wagala, Balhabou niishie tu hapo.
Balhabou wamepoteaaaaa kabisa!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
1620021748209.png
 
Scaba scuba, ilikuwa ni Mitsubishi Rosa nyekundu six cylinder. Enzi zile gari nyingi zikikuwa zikifanya safari 3 x 2. Kulikuwa na Camp Safari, Jongwe, El Sakran, Sansui, Accountant, Red Rooster, Cheetah, Uvikiuku, Selungwi, Wagala, Balhabou niishie tu hapo.
Nyingine zilikuwa Pop Juice, Master Top nk. Hizi zilikuwa zinapaki Magomeni Mapipa opposite CRDB Morogoro Road.

Nyingi zilikuwa ni Coaster za 3B engine ndo zikafuata Coaster Box Body.
El Sakaran ilipata ajali mbaya mno maeneo ya Mwidu 1991 au 2
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom