Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Me nakumbuka alinilipia ada ya mitihani ya kumaliza sec huku akiwa anaumwa hoi na akihitaji wa pesa pia ili aendelee na matibabu
Masikini Baba yangu saa chache baada ya kumaliza mitihani furaha yangu ikakatizwa baada ya kurudi home na kukuta msiba
Alitekeleza wajibu wake mpaka mwisho wa maisha yake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAOMBA UMAKINI WENU NA PIA TOENI PREJUDICES

Dada angu alivoolewa hakubahatika kupata mtoto mapema. nikiwa nakaribia kuanza darasa la kwanza, Shem akaja home kwa baba na mama akawaomba niende kuishi nae. Mzee alimsisitiza kuwa huyu mkorofi kama kuchapa chapa kweli.

Nimelewa na shem kama baba angu mzazi .Kanifundisha vingi kilimo na tabia njema .Sijawahai maliza tamka neno lolote kinywani kuhusu mahitaji yangu asinitimizie.lAinidekeza na kunionya sana.
Ladha ya viboko vyake haifanani na mtu mwingine aliyewahi kunichapa.

Yeye hunifundisha kimyakimya sio muongeaji. Kaniambukiza u introvertHata leo hii nikipata nafasi huwa naenda kumsaidiankazi zozote iwe nyumbani au hata shamba.Huku akinipa a to z kuhusu hiyo kazi tunayoifanya kiti ambcho nimepata maarifa mengi sana.
Hapendi uchafu ,Utotoni nimekula sana stick kisa nilikuwa sijui kufua.Aikuwa anaaka maji nayosuuzia nguoxmara mwisho yawe masafi masafi kama nilivyochota.

Anapenda niwe smart muda wote.Ana sikuxyake special ya kupiga pasi huo upanga wake nzi akijipitisha tu tu lazima akatike tu
Anapenda niwe sharp muda wote .Kanifanya nipende sana baiskeli mpk leo .Asa enzi hizo uende na baiskeli shamba afu irudi bila hata mzigo wa kuokoteza.

Kuna siku nikiwa likizo kipindi o level basi alini mind sana kwa kuwa nilikiwa tu kufanya kazi nachill geto basi akafoka eti wenzako wanafanya mazoezi ya mpira wewe umekaa hovyo tu.

Baba angu mzazi sijaishi nae sana ila na miss alikuwa akitupikia akipata time na malezi vile vile.

KiUFUPI NAJIVUNIA HAWA WARU WAWILI
Walijaliwa watoto baadae?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana Mushi hupaswi kuendelea na kazi kutokana na hali uliyo nayo..yafaa uwe nyumbani na familia ...Jibu la mzee Wanangu hawastahili shida labda niwe nimekufa...
Hapo ni baada ya kupata ajali na kupata hitilafu kwenye uti wa mgongo...nachokumbuka ..ilifika hatua hawezi kutembea still alitaka kwenda kupambana..
Tulikuwa hatununuliwi pipi ila mifuko ya pipi, Kama ni sikukuu Atanunua kila kitu in bulk, crates za soda mavazi, chakula, nk, , , Alikuwa na moyo wa kutoa ... Vitu hivyo havikuw vyetu peke yetu...Akifika utasikia Mama juma njoo chukua hivi ,mama fulani, , , , Then Wewe J chukua hizi wapelekee marafiki zako.......
KIZURI HAKIDUMU
Moment ambayo naipenda Alikuwa ananuka sana miguu so kazi Yangu kama sijalala akija Tuuu naanza kumwambia baba vua viatu hapo mlangoni unawe ...atacheka ataniita mwanangu J njoo univue viatu then ataninusisha...😅
....Nina mengi juu ya mshua ila alipendwa zaidi...
Rest in peace father

Nimepitia mengi sana ila nilipo afadhali...Ipo siku nitashusha nondo za life langu humu.😭😭😭
Dada kabaki kusema KAMA BABA ANGEKUWEPO
Dah,umenikumbusha mbali sana,mshua alikua smart sana.
Tabu yake anachepuka balaa.
Siku kalala nje siku 2 anakuja home maza alikua mwalimu, kuna bwege mmoja skuli kanisingizia nimeandika barua ya mapenzi kile kipigo siku ile sisahau, mdingi alipiga nikaflot alafu kakunja taulo kanininginiza juu ya dari nilivyopata upenyo mama ndo alifungua kitanzi.
Ila baada ya hapo nikawa chuma namimi tunabishana tu na pale dah akawa respect mpaka anavuta.
RIP baba😭😭😭
 
Nakumbuka mimi nikiwa form one na mdogo wangu grade 2 tumeshuka kwenye school bus tunatembea kuelekea nyumbani. Ghafla njiani akatokea mkaka jirani yetu akaanza niambia kwanini unanikataa huku ananipiga akinituhumu najisikia sababu sisi tunapelekwa shule na gari.

Mdogo wangu akakimbia hadi nyumbani kumwambia baba na mimi nilifanikiwa kumchomoka yule kijana nikakimbilia nyumbani kufika nalia baba akinichukua hadi nyumbani kwao yule kijana, ile tunaingia tu na yule kijana kafika kwao aiseeeeee alipigwa makofi na mshua nikajua yameisha tunaenda nyumbani.

Mara baba akasema tunaenda polisi kufika polisi nikaandika maelekezo na hivi nilikua underage ikachukuliwa defender pale kuja kumkamata yule kijana yeye alikua mkubwa tukaenda polisi alichapwa fimbo na polisi jamani baadae wakanipa fimbo na mimi nijirudishie hehehehe. Tangu siku ile hakuna kijana mtaani kwetu alitusogelea kuongea ujinga.

Nakupenda sana baba Mungu akupe maisha marefu.
Mi siku hiyo kuna madogo wababe kichizi mtaani,ila asubuhi utawakuta pembeni home pale wanaota jua.
Nikamwambia mdingi jana nimetandikwa vibaya, na nani?fulani na fulani aah jamaa hakulaza damu,asubuhi tu huwa anawapita pale na pilipili wanaota jua,siku hiyo katokea upande wa pili na mkanda wa jeshi walipigwa mikanda wale jamaa asubuhi ile mpaka nikajuta kwanini nimewashtaki.
 
Nakumbuka alikuja nichukua uwanjani nacheza chandimu. Nilikula viboko mpaka skuli, Sitaisahau siku hiyo. Mzee amerudi anaambiwa na mother kwamba nipo skuli, anapita uwanjani anakuta mechi kali.
Ndo siku ndoto za kua sadio mane zilipofifia maana sikudeal tena na mapira
 
mimi baba amejitahidi kusimamia yale yanayomhusu kama baba mpaka kufika hapa nilipo.

hakuwa na mkono wa kupiga piga,ila ni mfokaji hasa akipata maji.halafu mimi ndiye nimefanana naye kuliko ndugu zangu wengine.

nimelelewa na watu baki (shangazi)mpaka nikafikisha umri wa miaka 15 ndio narudi home kuishi na baba yangu ndugu zangu,na mama wa kambo.kule nilipotoka walezi wangu walikuwa wakali sana kuliko baba,nilivyofika kwa baba eti ndugu wanamhanya,mimi nikawa nacheka kwa dharau kwamba hamjui wandava nyinyi.cha ajabu mimi pekee ndiye nikawa na msuli wa kumjibu akiwa anaongea na kueleza masaibu ya familia na yangi binafsi bila kupepesa macho.mpaka akawa mtani jembe.ulikuwa ukikuta league isiyo rasmi mimi na faza unaweza cheka sana.

bado ni mzima namuombea aendelee kuishi zaidi,mpaka leo mimi ni kama mshikaji kwake.ila mama mzazi aliishatangulia toka nikiwa mdogo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba yangu alinibeba kwa baiskeli kunipeleka Dar ul Muslimeen primary school Dodoma..kwakweli tulikua tunatembea mwendo mrefu kidogo.

Baadae nikawa kibonge Akawa anasema nimekuwa mzito Sana....Baadae alihamishiwa Arusha hivyo nilibidi nitembee kwa.mguu kwenda shule. Rip my father...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah,umenikumbusha mbali sana,mshua alikua smart sana.
Tabu yake anachepuka balaa.
Siku kalala nje siku 2 anakuja home maza alikua mwalimu, kuna bwege mmoja skuli kanisingizia nimeandika barua ya mapenzi kile kipigo siku ile sisahau, mdingi alipiga nikaflot alafu kakunja taulo kanininginiza juu ya dari nilivyopata upenyo mama ndo alifungua kitanzi.
Ila baada ya hapo nikawa chuma namimi tunabishana tu na pale dah akawa respect mpaka anavuta.
RIP baba😭😭😭
yule mze dah. Nilikuwa mdogo kinoma 4 yrs lakini namkumbuka nakumbuka hustle zake ...kila nikipiga stories na maza haachi kuniambia kuhusu yeye... ..Napopitia matatizo ananiambia Hayupo angekuwepo Msingepitia Haya....Na ni kweli nimekula msoto.....nimeishi miaka 16 nikijua maza kafa ila ila ila Ndugu Wengine siyo powa...

Miss you dad....
 
Nakumbuka mimi nikiwa form one na mdogo wangu grade 2 tumeshuka kwenye school bus tunatembea kuelekea nyumbani. Ghafla njiani akatokea mkaka jirani yetu akaanza niambia kwanini unanikataa huku ananipiga akinituhumu najisikia sababu sisi tunapelekwa shule na gari.

Mdogo wangu akakimbia hadi nyumbani kumwambia baba na mimi nilifanikiwa kumchomoka yule kijana nikakimbilia nyumbani kufika nalia baba akinichukua hadi nyumbani kwao yule kijana, ile tunaingia tu na yule kijana kafika kwao aiseeeeee alipigwa makofi na mshua nikajua yameisha tunaenda nyumbani.

Mara baba akasema tunaenda polisi kufika polisi nikaandika maelekezo na hivi nilikua underage ikachukuliwa defender pale kuja kumkamata yule kijana yeye alikua mkubwa tukaenda polisi alichapwa fimbo na polisi jamani baadae wakanipa fimbo na mimi nijirudishie hehehehe. Tangu siku ile hakuna kijana mtaani kwetu alitusogelea kuongea ujinga.

Nakupenda sana baba Mungu akupe maisha marefu.
Alikosea, alitakiwa kuacha ecological cycle to take place
Hata mbugani ukikuta simba anafukuza swala sharti umuache

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namkumbuka kwa mengi hasa jinsi alivyokua ananihamasisha kusoma, japo alikua mkali, viboko kwa sana ila nashkuru kwa hayo sasa naona matunda yake.

Pia ni mtu poa sana na yuko social, hii imetusaidia kumzoea na kuongea nae mengi. Mungu ambariki sana na amlinde.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mgawanyo wangu wa trust mzee nampa 50%, mama yangu nampa 25% wajomba na baba zangu nawapa 20%, shangazi zangu nawapa 10% na mama zangu nawapa 5%
Based on my perception

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wangu bado upo naomba mwenyezi mungu akuweke zaidi ushuhudie mafanikio yangu kidogo na pengine nifanye utabasamu katika kipindi chako ulichobakiza hapa Duniani!!!


Tangu utotoni nilikuwa na matatizo ya kiafya sana tu niliwasumbua sana wewe na mama angu ambao bahati nzuri mpaka Sasa bado mpo hai!! Kuanzia 2003 hadi 2012 umekuwa ukinipeleka Clinic pale Muhimbili kuanzia nimelazwa Hadi nimetoka hospitali ulitake care kila kitu kuanzia kuniogesha kunifulia Hadi kunilisha japo nilikuwa mdogo sana ila nakumbuka kila kitu kizuri katika hicho kipindi chote, nakumbuka ile tupo mapokezi pale MNH tunaambiwa natakiwa nilazwe nikaanza kulia namtaka mama ulinibembeleza sana kuwa kila kitu kitakuwa sawa tunafika MWAISELA unaambiwa uniache utakuwa unakuja tu kuniona uligomba sana hadi ukataka upigane na yule Nurse yote ni kwasababu ya upendo wako mkuu kwangu!!!


Licha ya kuwa Askari wa cheo Cha chini kabisa na kipindi hicho hata BIMA hazijaanza kutumika kwa askari ulinigharamia matibabu yangu yote na hatukuacha clinic hata moja pale MNH tulitoka Mwanza hadi Dar kwa treni na baadae tukahamia Bus nilikulalia sana mapajani mwako na wala hata hukuwahi sema nakusumbua!!!


Siku zote ulikuwa Unapenda kuniita na kuniambia taratibu MWANANGU BAHATI MBAYA SANA MWENYEZI MUNGU KAKUNYIMA AFYA NJEMA SANA, HUWEZI HATA KULIMA ILA TAMBUA JEMBE LAKO NI AKILI YAKO JITAHIDI USOME SANA NDIO KULIKO NA MAVUNO YAKO!!


Nakumbuka siku nachanguliwa kidato Cha Tano ukaniletea Tranka Yale ya bati ulijaza kila mahitaji yangu ya msingi na Mzigo ukawa mzito haswa ila ulinipeleka wewe Hadi shule (kutoka mkoa mmoja hadi mwingine) ukalibeba begani mwako ukasimamia registration yote hadi nakabidhiwa bweni JITEGEMEE CUBIC L ulibeba Hadi bwenini!!!


Mwisho tena hili la juzi tu hapa Chuo nilkula Ada ya semester ya pili yote kama 600K nikawa Naogopa sana kukueleza na ninajua ni mstaafu kwa sasa huwezi kutoa kiasi kikubwa hicho kwa mara moja!! Nikawa nimemueleza ukweli Dada angu nae akamueleza Mama angu na Mama nae akakueleza wewe hukuniambia chochote mpk siku moja asubuhi umenifata chumbani kwangu ukaniambia tu amka ujiandae twende mjini tumefika town naona unanipeleka CRDB NYANZA BRANCH unasema chukua hii laki 7 weka kwenye account yako afu jiandae week ijayo nenda Chuo ukalipe deni na uchukue vyeti aseeeh nilifurahi Hadi nikalengwa lengwa machozi kwa mbalii hivi!!


Nakupenda sana Baba angu japo ulijua kabisa nilikuwa na afya mgogoro Ila ulinipa stick sana sana, nikizingua nakumbuka kipigo chako mujarabu ushanitia bakora nikiwa darasa la 5!! Kwa kuonyesha dharau kwa mama angu mdogo mbele yako Hadi nikajikojolea kile kipigo sitakisahau maishani mwangu!!! Niko O'level kdato Cha 2 na 3 ukagundua sipendi shule na ukiwa unaingia kazini asubuhi basi siendi shule Ila ukaanzisha Operation ukienda job sa4 unarudi kupiga tea lazima uulizie Mhuri 25 akenda shule wasipokupatia majibu ya kuridhisha sana unakuja chumbani ukinikuta utaniamsha na stick juu nioge ma muda huo huo niende shule nishaonekana sana darasani kuanzia sa5 hadi sa9 wakati asubuhi sikuepo!!



Nimeshindwa hata kuandika vizuri maana sio muandishi mzuri kabisa ila leo nimeona angalau niseme haya kwa Baba angu nawakubali sana Baba wote mnaojitambua na kujali familia zenu naomba mwenyezi Mungu nami Nije niwe baba Bora na mume mwema kwa mke wangu!!!






Typed Using KIDOLE
 
Kila mtu anasema their father ni best ever!!! Sababu kila mmoja kaonja ladha ya babake pekee na si ya baba wa mtu mwingine.Mimi naona kama best dad ever hatutamjua,Au nakosea?
Huyo baba mwingine ambaye hajakuzaa hawezi kuwa na ladha ya baba yako mkuu

Huyo n best dad ever kwa mtoto/watoto wake kama ambavyo baba yako ni best dad kwako wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu kwa hayo uliyopitia
Asante. Ilinifunza sana. Mama alikuwa kila siku akikonda, bahati mbaya sana mama yangu alikuwa ni mpole sana, na mtiifu kupita kiasi. Nikaja jua kuwa ni mzee ndiye chanzo baada ya kuwa mtu mzima. Nilizoea kuwaambia wadogo zangu, mkiolewa msiwe kama mam, kuweni na heshima kwa waume zenu ila msiwe watumwa. All in all, namshukuru pia sababu kila kitu nilichofanikiwa maishani mwangu, msingi ni wake.
 
Back
Top Bottom