Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

bokassa,
Wewe ulikuwa selule.

Anyway. Unanikumbusha C za matroni. Kuna jamaa aliona mademu wamekaa chini hawafanyi kazi na yeye akajiunga nao.

Afande aliyekuwa anatafuta watu waliojongo akaanza kuuliza wanafanya nini. Mademu wakajibu wana C za matroni. Afande akawaachia kiulaini na alipomuuliza jamaa. Jamaa naye akatia ana C ya matroni.
 
Sanctus Mtsimbe:

Uite mpera mpera na wala sio mchungwa. Wanajeshi watakufundisha jeshi tu na sio ujasiliamali.

Kama kuna nia ya kufundisha watu ujasiliamali, sehemu zitafutwe zingine na sio jeshi.

Mzalendo Zakumi; maoni yako ni ya kweli kwa mfumo uliokuwapo.

Wazo langu mimi ni kuwa JKT kama ikirudi ingeweza kuwa Transformed kwa namna fulani ili kuwasaidia Watanzania wanaopitia hapo. Asilia Watanzania wengi hawana uthubutu wala ujasiliamali. Shurti ingetafutwa namna ya kuangalia namna gani wanaoptitia wangepatiwa pia mafunzo ya Ujsasilimali na Uzalishaji, basi Watanzania waliopitia wangekuwa wabunufu na wachapakazi sana.
 
Bulombora kwa Kanali Kikoti enzi hizo mpoooo?

Mkuu tupo, Unajua Kikoti aliishatangulia kwenye hukumu ya haki (RIP). Baadaye wakaja akina Afande mzena na Afande Mtekele. Kulikuwa na yule RSM na ndevu za ajabu sana moustache umesimama......nakumbuka zile kazi za kukata magogo ya chokaa kwa kutumia jembe shoka...yale majembe shoka yalikuwa ni multipurpose kulimia, kukata kuni, kuchonga mawe kule ziwani.....

nakumbuka kipindi cha kupalilia migazi ama kufyatua tofari ilikuwa shughuli pevu, niliamua kujongo kwa kuwa nakimbia na shoka begani, nikiulizwa nipo wapi nikawa najibu special assignment kwa afande CO. Jamaa wakajiunga na mimi ikajulikana sisi ni kitengo maalumu kwa CO.

Siku ya siku ilikuja julikana ni waongo tulipelekwa uwanja wa damu tulipigwa drill na afande Mayunga will never forget...jamaa alitupiga na ule mwendo wa kukwepa ndege ulitumaliza kwa kweli nilisikia damu puani.

A lot of memories Bulombola, Week ends Kaseke na myomboz kupata pombe za kienyeji hahahahah
 
Wewe ulikuwa selule.

Anyway. Unanikumbusha C za matroni. Kuna jamaa aliona mademu wamekaa chini hawafanyi kazi na yeye akajiunga nao.

Afande aliyekuwa anatafuta watu waliojongo akaanza kuuliza wanafanya nini. Mademu wakajibu wana C za matroni. Afande akawaachia kiulaini na alipomuuliza jamaa. Jamaa naye akatia ana C ya matroni.

Du! Mkuu, hiyo kali sana! Jamaa akadai ana C ya Matron? Nadhani hakuwa ameelewa. Maana kule wala huwezi kudanganya wote mnakuwa kwenye Green Vest za Kijani na Blue Bukta za Bluu.

Vipi, hakupata Dirill?
 
Ushirombo,
Nilikuwa Bingwa Coy kwa luteni mmoja jina limenitoka alikuwa na mkwala anakusogezea bega lake anakuonyesha nyota zake mbili halafu anasema, "unaona hizi, hupigiwi kura kupata hizi!" duh na koplo Omari jamaa mwili mdogo sauti kubwa, mkwala mwingi kwenye kwata anapita nyuma yetu akisema "ukisikia uzito sehemu yoyote ya mwili wako, ujue simba ametua" eti yeye simba wakati hata buti zake anashindana nazo uzito, maafande kwa mikwala mbuzi...
 
Mama, Makutupora ni kule kwenye kilimo cha mizabibu? Hebu tupe visa vya huko.
...Nilikuwa Makutupora mzee mzima operation Kambarage...Mkuu kupalilia mashamba ya zabibu na kumwagilia bustani ya mboga za majani unapiga ndoo mpaka mikonoo inaota viazi utadhani unafanya mazoezi gym. Nilikuwa kombania C...Mwanawane kuna afande mmoja anaitwa Mwiba kifaa kwa kwata hicho ni noma. Nakumbuka siku moja tunapiga kwata mchana wa saa 8 baada ya chakula mchana kuruta mmoja alianguka mpaka akatapika spinachi na ilikuwa hakuna ruhusa kumsaidia wala nini...

Ah! Makutu mwanangu nakumbuka kuvunja mawe mlima kitunda saa 10 alfajiri kwa ajili ya kujengea nyumba za maafande na safari za Dodoma mjini kwa miguu 21 km kwenda na kurudi kaka nilikuwa fiti kinoma.Kichele ilikuwa Sh. 350 kwa mwezi na unaipigia bajeti kama kawa, mafuta ya Ray, Colgate ndogo kama kidole, sabuni ya mawingu kwa ajili ya kuogea na kufua si unajua Dom maji ya chumvi.....Tumetoka mbali sana...
 
Kwa wale tuliokuwa nao Mlale JKT, Operation Azimio la Arusha, 1987/1988. nadhani mnawakumbuka afande Pilato, Nguvu ya Nyani, Mtono(RIP) na vijiwe kama Lusonga, Magagula, Mlandizi, Chipole
 
Kwa jinsi Jeshi lilivyonikolea siku moja nilikuwa Posta Dodoma mjini kuchukua tujisenti twa kujikimu si nikaitwa jina, kwa nini nisiitike "Afande!!" watu wote waliangua kicheko..Kwa wale waliopitia Makutupora nadhani majina haya ya Maafande yatakuwa yanawakumbusha mengi...Afande Zimwi, Mduba,Gwalanda,Singira,Mwashambwa,Mwanaidi, PEO (Haka kajamaa ndio kalikuwa katalaamu ka siasa pale Makutu)...

Kombania C ile biashara ya kutengeneza Miradi pembezoni mwa Mahanga then usiku Tembo anapita. Sir Major Gwalanda akitunyung'unya vijana kwa kutukalisha kwenye baridi usiku mkubwa kwa kututaka tuvue vest....Masuala ya kusimamisha minazi usiku kwenye kwenye chai ya sh.10 canteen na vitumbua wanavyopika wake za mafaande kwa unga wa mahindi vitumbua vigumu kama kitennis...

Kwenda guard usiku unatakiwa ulinde nguruwe hata kama itikadi yako haikuruhusu jeshi haijui hiyo.... Kwenda kukata magogo MayaMaya....Ni brudani fulani na lugha za mafaande eti kuruta umevaa green vest ya njano, au unajifanya msomi una degree kuna watu wamepita hapo wana diploma!!!!Teh! teh! Tehhhhhh!!!!! Kibwengo usiku serengeti....
 
Hivi kuna watu huku walikwenda JKT CHITA? Maana nasikia huku ndipo kulikuwa na jeshi haswa!! Tungependa kujua kulikuaje huko. Nasikia makuruta walikuwa wanavunwa sana na huwezi kutoroka (simba n.k).
 
Hivi kuna watu huku walikwenda JKT CHITA? Maana nasikia huku ndipo kulikuwa na jeshi haswa!! Tungependa kujua kulikuaje huko. Nasikia makuruta walikuwa wanavunwa sana na huwezi kutoroka (simba n.k).
....Hebrew, usiambiwe kitu huko Chita si kwamba ndio kwenye jeshi ni JKT kama zilivyo kambi nyingine tatizo la Chita ni kuwa porini sana kiasi kwamba hata kuruta aki-attemp kutoroka ndio hivyo risk wanyama, majoka ndio tatizo. Otherwise kama ni kilimo hata kambi nyingine wanapiga jembe kama kawaida. Kwani Chita mtu akitaka kusafiri kwenda maeneo mengine usafiri uliopo ni treni ya Tazara tu.
 
Nilipangiwa kwenda kambi ya Masange Tabora, kuna watu walinipa taarifa kwamba kambi ile siku ya kwanza ukiingia lazima mtu upewe mawe fulani kwa ajili ya kunyonya sumu ya nyoka. Nilitishika nikaamua nikaripoti JKT Mafinga. Kufika pale Mafinga JKT nilimuona afande Mlay nikajieleza kwamba ilikuwa niende Masange Tabora lakini napenda nibaki Mafinga. Afande Mlay akasema hii ni manpower safi kabisa. Baki hapa.

Nilipangiwa Coy F kwa OC Afande Rweikaza, Mlimbila au Master Followup na Afande Mwakyosi. Siku ya pili tuliamka kama kawaida saa kumi alfajiri. Tukafanya usafi na baadaye foleni kwa ajili ya kupangiwa kazi kwa utaratibu wa kikosi. Sote tukiwa kwenye green vest za kijani. Afande Rweikaza akawauliza maafande wenzake kama tumesahaulishwa shule, wakajibu BADO.

Tukaambiwa kila mmoja awe na jembe. Tukapanga foleni, nyuma geuka tukageuka tukaelekea porini karibu na eneo la kombania yetu. Kufika kule wakatuamuru kupanga mstari mmoja mrefu (single file) kama walivyoita wao. Kila mmoja akiwa na jembe tukaambiwa kila mmoja achimbe kishimo kidogo. Sote tukawa tumechimba kila mmoja kishimo chake, tukaambiwa kila mmoja ainamie kile kishimo akikumbuka kuanzia tarehe yake ya kuzaliwa, jinsi alivyosoma mambo yote aliyokabiliana nayo hadi pale alipo. Baada ya hapo tukaambiwa tufukie yale mashimo.

Tukafukia. Afande Mwakyosi akaamriwa kuanza mafunzo rasmi. Mwakyosi akasema wewe kama kuruti hapo ulipo huna elimu. Hujui kusoma wala kuandika. Akauliza "...kati yenu nani anajua kuhesabu tukanyosha mikono akamuamuru kuruta mwenzetu mmoja ahesabu akamuacha hadi akafika kumi, mwingine akafika tano tu, kisha akasema kuna hesabu za kijeshi na za kiraia. Hapa ni kuhesabu kijeshi. Akaanza kijeshi tuna namba zifuatazo.....1...23...1. Akaamuru akisema kushoto geuka tuzirudie namba hizo sambamba na kukanyaga mguu chini kwa nguvu.

Ndiyo maana hadi leo hakuna namba inayozidi hiyo kwenye amri za jeshi. ...1....23.....1.

Jeshi hilo.
 
Last edited:
Bubu Msemaovyo,
Oh man, kipindupindu kilipigwa kwata kikakimbia, Oh ugali kwa uji usio na sukari ni mtaja ajabu tena basi saa tatu asubuhi. We bwana, ni saa kumi alfajiri, ugali kwa maharage wa jana jioni uko chini ya kitanda vumbini, kuruti kumi na moja mnagombania.

Uti umejitahidi mwenyewe kuleta kuni, unashitakiwa kwa kuiba viota vya ndege. Siku moja tumeshikilia landrover juu juu mpaka tairi lililokuwa na pancha likabadilisha eti uraiani tunasema haiwezekani!!

Saa kumi na nusu alfajiri wagonjwa 20 wamefoleni, Afande anaandika wagonjwa 4 tu, sasa akili kichwani baadaye wote mmepona sasa sijui wangapi walikuwa wagonjwa kweli
 
Fikiria wanaume wote mmenyoa vipara, wote wake kwa waume mmevaa bukta za Buu (wakati huo wasichana wanazivutia chini kuficha mapaja yanyongara, kumbe baada ya wiki tu wote watakuwa wanavutia hizo bukuta juu!!!!!!!!!) na green vest za "kijani" viatu sampuli mbalimbali (wakati huo hakuna buti) hapo ndio unaona kweli binadamu wote ni sawa. Wasichana wanpokuwa sambamba na wavulana kuiba ugali (sio kosa kule)...... yaani unajifunza maisha ya kumthamini kila mtu maana hujui ni nani atakae kuokoa wakati gani!
 
Mzalendo Zakumi; maoni yako ni ya kweli kwa mfumo uliokuwapo.

Wazo langu mimi ni kuwa JKT kama ikirudi ingeweza kuwa Transformed kwa namna fulani ili kuwasaidia Watanzania wanaopitia hapo. Asilia Watanzania wengi hawana uthubutu wala ujasiliamali. Shurti ingetafutwa namna ya kuangalia namna gani wanaoptitia wangepatiwa pia mafunzo ya Ujsasilimali na Uzalishaji, basi Watanzania waliopitia wangekuwa wabunufu na wachapakazi sana.

Haya ni maoni yangu. Vipaji ni lazima uviendeleze watu wakiwa na umri mdogo. Kama hukucheza soccer mapema basi soccer la uzeeni uliwezi.

Likewise, ujasiliamali unatakiwa kuanza mapema kama sehemu ya mafunzo mashuleni.

Sehemu kubwa katika ujasiliamali ni matumizi ya Instincts kama vile mwanamichezo. Hivyo mitaala ya mashule yetu ambayo kwa sehemu kubwa inamuandaa mwanafunzi kushindania nafasi chache za elimu ya juu inabidi iangaliwe upya kama tunataka watu wawe wajasiliamali.

Kwa maoni yangu haya sioni sababu mwanajeshi ambaye maisha yake yako Institutionalized na utamaduni wa kujongo, mbinu za medani, kutafuta pororo awe mwalimu wa ujasiliamali.
 
Zakumi,

Zakumi, tunaweza tukawa hatutofautiani sana.

JKT hapakuwa mahali pa kujifunza mambo ya Kijeshi tu. Nadhani kama sikosei 25% ya Muda ndiyo hasa ilitumika kwa mafunzo ya Kijeshi. Ukuruta ni Miezi sita na katika hiyo si wakati wote mnasoma au kufanya mambo ya kijeshi. Service ni Miezi 6 na ni mchanganyiko wa Guards na shughuli nyingine.

Kwa experience yangu, Ujasiliamali wa kusoma unaweza usilete matunda yanayokusudia. Kuna wengi nawafahamu waliosomea elimu ya Ujasiliamali lakini bado hawajafanikiwa katika kujiwezesha.

Wafundishwe Mashuleni? Sawa, lakini hata Elimu ya sasa ya vijana wetu na ubora wake ni mgogoro. Wataweza Ujasiliamali kwa ubora wa kuwawezesha?

Ninachosema mimi JKT inaweza kuwa transformed kiaina ika-accomodate mafunzo ya Kijeshi na Ujasiliamali wa Kimaadili lakini wenye msukumo wa LAZIMA UWE MJASILAMALI kiakili na hata vinginevyo. Hili ni suala ambalo linaweza likawa linahitaji concepts mpya mfano wa Makambi ya Ujasiliamali.
 
bangusule,

Bangusule, umenichanganya kidogo. Maelezo yako yote yanaelezea kila kitu kilicho tokea G Coy mwaka huo pale Ruvu. Labda originally wewe ulitoka F Coy na kuhamishiwa G Coy. Kwa sababu G Coy ilianzishwa specifically kuwanyosha wajanja wajanja na watoro wote wakutoka kombania zote pale kambini.

Na kweli, watoto wote wazuri walikua huko G Coy na watu tulikula jeshi pale G Coy thanks to Mwakatumbula na maafande wake mpaka adhabu ikabadirika naikageuka kujenga wanajeshi kabambe. Mpaka G Coy ikachaguliwa kuwakilisha JKT kwenda kupiga gwaride la miaka 30 ya uhuru uwanja wa taifa.

Da hii topic imenikumbusa mbali na JKT ilikua experience moja ambayo kweli sita sahau na faida zake kwangu ni nyingi sana na kubwa mojawapo ni kukutana na watu wengi wa kila aina kutoka Tanzania nzima kwa wakati mmoja. Am having major nostalgic feelings kukumbuka matukio ya kila aina na kusoma yote haya na vituko vyote, mazuri na mabaya yaliotokea and will ever be grateful for the experience.
 
Sanctus Mtsimbe,
Mtsimbe:

Haya ni maoni yangu tu. Kama nilivyosema kuwa ujasiliamali ni instincts na sio elimu ya maarifa. Huwezi kuwafundisha watu instincts. Instincts unazi-build.

Kilichomfanya Bill Gates, Kijana wa Facebook.com kuacha masomo na kujiingiza kwenye biashara ni instincts.

Unapochukua masomo ya biashara, unachukua elimu ya maarifa lakini sio instincs.

Kama vile hatutegemei mtu kuanza kucheza soccer akiwa na miaka 20, vilevile tusitegemee elimu ya biashara au uhasibu kumfanya mtu kuwa mjasiliamali.

Kwa mtaji huu sikatahi kuwa JKT inaweza kutumika. Lakini vijana wengi wanakwenda wakiwa na umri wa miaka zaidi ya 18. That's too late kwa maoni yangu.
 
Ndo maana JF tunaiita jungu kuu, mmenikumbusha mengi na mbali sana. Kwa wale wa Oljoro mnaikumbuka ROSHEROOO umasaini?

Afande Dauda keshatajwa, je, Mnamkumbuka Afande John Matondo?, yeye akiamsha watu kwa kurusha changarawe au kijiwe kidogo juu ya bati!, sasa ole wako usiamke! Wakati mwingine anaingia hangani halafu anatoa kikohozi cha kebehi halafu anatoka anasuburi, dakika mbili baadaye anakata bogi la wachelewaji! Afande Bosco yeye sifa yake kubwa ilikuwa alishaua kuruta kwa kusulubu!-Akikutazama tu unaweza kuanguka!

Nawakumbuka na ningependa kuwasiliana na wengi kama akina Justin Majengo, Mbutolwe Kabeta (alinifundisha kusonga ugali wa kombania, kwani mara ya kwanza mwiko wa ugali nusura unirushilie mbali!), Erasto Mkumbo, Peter Mhina, Hadi Katunzi, Chausiku (Butote?), (Lindarose?) Mushi, Wallace Arthur-Hamisi Bakari (Dr), Kapinga, Davi Mwamakula, Abdul Tajiri, Costantine Mkama, Costa, Joseph Mbelwa, Sauka (Stanley?) Ndaro, Eva Nziku, (Mary?) Shule, (Grace?) Magoti, Joseph Masanja, Yohana Mgonja, na wengineo wengi tu ambao majina hayajanijia kichwani sasa hivi.

Nilijifunza mengi na nilifunguka macho kwa mengi niliyoona, nilipata marafiki na wengi wao tukawa kama ndugu.
 
Kiongozi Zakumi;

Uko sahihi in a way hasa unapozungumzia Wajasiliamali ambao ni wa kuzaliwa.

Kama ilivyo kwa viongozi, kuna Wajasiliamali wa namna mbili, kuna wale ambao ni wa Kuzaliwa ambao nadhani wanaingia kwenye kundi ulilitaja hapo juu.

Lakini wako Wajasiliamali ambao ni wa Kujifunza baada ya kwenda shule, au kuishi katika mazingira fulani hivi, na hao wako wengi hata hapa Tanzania. Nawafahamu baadhi yao.

Wakati nakubaliana na wewe kuwa ni vema Elimu ya Ujasiliamali itolewwe Mashuleni, bado kuna muhimu kuwa na PRACTICAL ENTREPRENEURSHIP CENTRES. Hizi kwa mawazo yangu zinaweza kuwa kama INCUBATORS za Wajasiliamali. Wazo langu ni kuwa, kama kukiwa na Waalimu wazuri JKT na hili somo likawa enforced, basi Watanzania wengi watabadilika. Asilia Watanzania wengi ni wavivu.
 
Back
Top Bottom