Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Oh, ulikuwa Coy Eagle! Ruvu, au Buhemba? Ruvu: Uliwakuta maafande Lyimo, Medadi, Zuberi, ...? CO alikuwa nani? Maafande wengi wamefariki, akiwemo Dr Omari, adjutant Jalala (km sijakosea jina).

Nilianzia Ruvu, Service Buhemba, kisha tukapelekwa detach Rwamkoma!

Brother majina sikumbuki sana. Lakini huyu Medadi kama namkumbuka vile . . .

Kuna jamaa alikuwa anaitwa Raymond alikataa kuanzisha disco, basi jamaa akampandishia saaaana. Akamwambia . . .

WEWE UNAJIFANYA EDUCATION SIYO? KUNA WATU WANA MADIPLOMA HAPA ITAKUWA DEGREE?

Akimaanisha unajifanya msomi? Na akidhani kuwa Diploma ni higher qualification kuliko degree. Nadhani alikuwa mfupi mweupe.

Alikuwa na wimbo anaupenda saana . . .. KIJOGORO CHAWIKA KOKOOO . . . HAIYOOO HIYOOO KOKOWEEEE . . . nk.

Jamani raha sana enzi hizo.
 
Wakati wa usiku kwenye disco, tukaona kundi la ma Mp linakuja usawa wa kombania. Tukajua, leeo tumepatikana. Wakaongea na kamanda wa kombania, halafu muda si mfupi wakaondoka. Baada ya wao kuondoka,kamanda akasoma majina yetu na kutuita tutoke mbele. Akautuuliza, nyie mlikuwa kwa kuku leo? Tukamuambia ndio. Akasema safi sana, nyie askari wazuri sana, mmekamatwa, lakini mkaweza kutoroka, pamoja na mayai yenu. Huo ndio uaskari. Hatukupewa adhabu, disco likaendelea!

Du! Mkuu Kitia, hii True Story ni kali saaana. Ama kweli Jeshini wote tulikuwa level moja.

Nakumbuka pia tulikuwa na watoto wa Vigogo wa zamani akina Nyota Kimario (Sijui yuko wapi siku hizi na Binti wa Malima). Wote kwata mtindo moja.
 
88/89 Nakumbuka Mafinga kulikuwa na bendi ya Kimulimuli na waimbaji mmoja alikuwa amepanga pale JC kwa jina aka Bichuka na mwingine simkumbuki jina alikuwa anapenda kuigiza nyimbo za regae -jerusalem mmojawapo. Mlay akiwa CO na major Miludi we acha tu walikuwa wanaweza kazi ikitokea kuna master parade ya CO.
siku moja Mlay akaja kukagua usafi wa maaskari hasa soski unavua viatu, we volunteers (volvo) walikuwa wachafu jamani! siku nyingine kibao kikawageukia maafande acha warushwe vichura!

Haaa haaa Mkuu, Ruvu ilikuwa ni mwendo wa King Kick na nyimbo zake za Kesi ya Kanga na Kitoto Chaanza Tambaa nk. Weekend Msasani Beach kwa akina Choggy Sly!

Mabreak Dance ndo ilikuwa kipindi chake. So, unapiga black trouser na White Shirt Long Sleeve na Bow Tie Nyeusi na Glove walau moja Nyeupe huku umekata Sheggy. Hapo ni mwendo wa kuteleza kwa kwenda mbele au kuzunguka kama Pia.

Raymond uko wapi Kiongozi? Boogie za mchana pale Mbowe Clubs kama kawa!
 
Lole Gwakisa,
Yaani Jamaa walikuwa na Mikwala kweli . . . Mara Oooh . . . .

NITAKUPIGA NIKUUE NA KUCHIMBA KABURI KWA MIKONO NA KUKUZIKA BILA MAITI YAKO KUONEKANA. WEWE NI KURUTA WA JESHI TU.

Ukimwona jamaa mwenyewe unatamani umvuruge lakini ndo hivyo tena.
 
Naona hapa sio mahala pake,tuna matatizo mengi sana kama taifa,tuachaneni na mtindo huu wa kukumbushana yaliyopita kama hayatusaidii.We do not need the past if can not contribute on our future.
 
Hebrew said:
Mmenikumbusha mbali sana.. Mimi nilukuwa Ruvu, halafu Mgulani (kwata la uhuru) halafu Mlalakuwa, miaka ya mwanzoni mwa 1990. Ruvu nilikuwa Fcoy (makondeko) na kina Afande kesi, simba, mohamed na salehe. CO alikuwa ni kanali urio (nasikia ni marehemu). Nakumbuka kulikuwa nafande mmoja alikuwa anaitwa Mizani na alikuwa mpenzi sana wa mabinti (alikuwa anawasubiri vichakani wakati wanatoroka).

Nyimbo ninazokumbuka ni kama !moto wayaka mama ..moto wayaka..wayaka wayaka", Zaina zaina..zainabu wangu usiku silali" na "canadia ee canadian ee.. (nimesahau maneno hapa). Nilifurahi sana jeshini kuliko hata shuleni (boarding).

Hebrew,

ha! ha! ha! ulikuwa RUVU combania F, kombania ya Mahepe, kombania ya Wajanja!! basi F kulikuwa na OC Luteni Mwakatumbula, Sir Major Babwetega "Mwiba", Staff Surgent Kinyaruhama "Kibuyu", Surgent Salamba, Volunteer Koplo Mwamasangula "Kamanda Mizinga", Afande Monica. pia alikuwepo Surgent mmoja Mhaya nimemsahau jina. Surgent Mwambingu pia alikuwa anakuja kubangaiza.

F COY ilikuwa na watukutu wote na wasichana wote wazuri. Maafande waliamua kukomoa makuruta wa F COY lakini badala yake makuruta wakawa wagumu. lilikuwa linapigwa kwata la mfano na kufa mtu. Maafande walikuwa wanatoka maofisini kuja kuangalia kwata. Baadaye F COY ilihamishiwa Mgulani kupiga gwaride la miaka 30 ya uhuru. Afande Kitomari RSM wa Mgulani alitukoma makuruta toka Ruvu kwasababu ya utoro.

CO alikuwa Luteni Kanali Kanaeli Urio, 2IC Major Chotta, CI Major Nakuchema, Adjutant Captain Balala, RSM Warrant Officer II Situke.

JESHI LILIKUWA NI KUPOTEZA MUDA TU. SIKUONA FAIDA YAKE.
 
Du! Mkuu Kitia, hii True Story ni kali saaana. Ama kweli Jeshini wote tulikuwa level moja.

Nakumbuka pia tulikuwa na watoto wa Vigogo wa zamani akina Nyota Kimario (Sijui yuko wapi siku hizi na Binti wa Malima). Wote kwata mtindo moja.

Kwenye platoon yangu alikuwepo mke wa CO, wakati huo Major Makame. Tulikuwa tunahenya wote mtindo mmoja, tena alikuwa hataki shushi.
 
Naona hapa sio mahala pake,tuna matatizo mengi sana kama taifa,tuachaneni na mtindo huu wa kukumbushana yaliyopita kama hayatusaidii.We do not need the past if can not contribute on our future.

LoL. Unajua tena usipokumbuka good old days utapata depression tu.
 
Wewe Sikonge wacha uhuni wako!

Mntanzania,
Siyo uhini. Unajua tulipokuwa kwa mama, tukawa tunapiga story za kwaya na walimu wake hasa huyu Mbajo. Ndipo akasema kuwa na yeye alikuwa akiimba kwaya. Aliponiambia kwaya gani na kumwuuliza juu ya mwalimu wao akasema naam ndiyo sisi. Katika nyie nafikiri mwenye tabia hiyo ni Abas tu.

Ukija kwenye uimbaji wa DISCO la JKT, nakumbuka hiki kituko ambacho nilicheka sana siku hiyo. Jamaa yangu huyo Manara. Huyu alikuwa mpinzani mkubwa wa Disco na kuimba. Baada ya kuimba kwa muda wa miezi miwili, siku moja aliporudi kwenye hanga, akasema "Lohhh, kama kuimba ni kazi ngumu namna hii, basi sitaki KWENDA MBINGUNI..." Watu tukapigwa na butwaa, vipi tena? Jamaa akasema "...... kama hapa JKT, Disco ni masaa mawili na ninachoka namna hii, je ukienda mbinguni itakuwaje? Kwenye biblia imeandikwa kuwa WATAMWIMBIA MUNGU, USIKU NA MCHANA..."
 
kweli nilisahau siku tliyozima moto wa msitu wa sao hill,siku nimeisahau ingawa nilirekodi kwenye diary yangu ambayo nimeisahau bongo (sasa hivi nipo saudi arabia kikazi),wengi tulikuwa tunajitayarisha kwenda jc,kiasi cha saa tano asbhi hvi bigula la hatari likalia wengine walipuuza waliamua kuondoka lakini afande co mlay aliamuru liende kupgwa hadi huko jc na yye mwenyewe akiwa msimamizi,alisimamisha gari lolote la jeshi na kulielekeza kikosini kuwachukua service men/women na askari wengine,kwenda kuzima moto.

tulianza kuzima kuanzia saa 6 mchana hadi 9 alfajiri na aliamrisha turudi kikosini moja kwa moja tulifikia canteen kule kilikuwepo chakula cha mchana na cha jioni,alisema kila mtu atachukua share zake zote kama hali aweke kwenye sehemu nyingine iliyotengwa maalum kwa ajili ya nguruwe wake.

kwa wale wasioitikia mwito wa kuzima moto walipata adhabu kali sana,walitakiwa kuamka asbhi kutmbea umbli wa km kama 50 na kurudi kwa muda waliopangiwa na kuchukua majembe kwenda kulima nakumaliza sehemu waliyopangiwa kwa muda maalumu,hiyo kama kwa mwezi mzima.Mengine nakubali kweli jkt wanawake bure,uongo,fitina,kujikweza,ujuaji
 
Nakumba green kwanjwa mmoja pale mafinga ilikuwa 88/89 baada ya kupata share jioni, tena siku hiyo nadhani pororo lilizidi, chakula kikawa kidogo, green kwanja akaamua kugawa yeye huku amevuta kofia nakufunika uso. tukiwa tunakula huku tunasikitikia pororo lilivyozidi. basi green kwanja akamsikia mwenzetu mmoja alikuwa akiitwa 'Double P' akamua kumuita nafikiri ili ampe adhabu; basi akaanza ;
green kwanja- Double P
Double P - Afandee
green kwanja - Carry on (akiwa na maana njoo hapa) sisi pamoja na Double P tukawa tunaondoka
green kwanja- Double P
Double P - Afandee
green kwanja - Carry on
sisi tukaendelea na safariyetuya usawa wa kombania. Basi acha green kwanja achachamae! we double P mimi nakuita uje hapa unajifanya unakibri siyo?

Double P - hapana afande si umeniambia carry on?!
green kwanja - Kutura - waken up (wake up)
 
Duuuh ama kweli nimekumbuka mbali sana. Mimi nilikuwa RUVU operation vyama vingi kama sikosei. Nilikwenda mapema tarehe za mwanzo wa mwezi wa sita. Wakati ule kulikuwa na baadhi wa service men wanalipia siku zao. Tuliingia na costa mpaka getini mida ya saa 11 jioni. Nilijulikana mimi mgeni.
Baadae tukaenda mesini kula, duuuh huo msosi nikashindwa kula maana yalikuwa maharage ya jana au asubuhi na ugali ambao umekauka ukipigwa nao unaweza kutoka nundu kama sio kuzimia. Nikamuuliza service man mmoja kuwa wapi naweza kumwaga ule msosi, basi jamaa akasema hapa chakula hakimwagwi lazima nikile nikimalize.

Wakati kama huo hao service men wanaolipia huwa wanajifanya maafande kwa hiyo wanatumia muda huo kuwatesa kuruta. Mimi kuangalia nikashtukia kuwa wale sio maafande maana walikuwa wamekaa na jamaa fulani nilikuwa nasoma nao walikuwa wamenitangulia darasa. Basi mimi nikamwaga pembeni kwenye mtaro nikampiga jamaa mkwara, nikampaka sana na nikamwambia kama ana uwezo anifanye anachoweza.

Niliyasema hayo lakini nilikuwa naogopa moyoni maana nikawa nawaza kuwa jamaa anaweza kunilengesha kwa maafande ukizingatia wakati huo kuruta walikuwa wachache sana. Basi usiku wakati tupo kombania, akaja afande akatuchagua kama watu sita hivi akasema tumfuate. Salaleeee, pale mess kulikuwa na lori lile Nissan Diesel nalikumbuka sana. Tukaambiwa tupande tukafuate mablanketi. Kucheki lori limejaa mahindi mpaka juu. Kumbe mablanketi ilikuwa danganya toto.

Tukapanda tukaenda tusikokujua, kumbuka hiyo ni siku ya kwanza kabisa. Mara tupo maghala, tunaambiwa tushushe lori zima maana linatakiwa kesho yake likachuke magunia ya unga phase 2. Ilikuwa shughuli si ndogo. Baadaye nikawasikia wanasema inabidi kesho hayo mahindi yapakizwe tena kwenye lori yapelekwe kusaga phase 2.

Nimetoka pale mweupeeeeee. Kwenda kujimwagia maji site nikasikia makuruta wenzangu wanasema kuwa kuna kuruta mmoja amemtukana afande wamempania ile mbaya. Hawakujua kuwa ndio mimi wenyewe walikuwa wanatia stori. Nikaenda kulala hoi bin taabani.

Kesho yake nimeamka asubuhi kupiga mswaki akaja afande akatunyakuwa watu kama 3 kwenda kushusha magunia ya unga, yalikuwa kama 10 au 12. Nikaona sasa hii ishakuwa shughuli. Siku hiyo hiyo mwenge ulikuwa unakuja kikosini kwa hiyo ikabidi tukapewe pit shot na green vest za kijani. Nikachukua na nikatumia kipindi cha shamra shamra za mwenge kuingia mitini baada ya kumuuliza mshikaji mmoja aliyekuwa analipia, nikachukua usawa wa njia ya vibwende. Hiyo ilikuwa experience ya siku ya kjwanza kabisa jeshini.

Nikakaa home kama wiki 2 duuh siku narudi tuu kama kawaida tukaja na jamaa wachache wanaolipia ndani ya costa. Sasa ukiwa mgeni unaambiwa kaa pembeni ukiwa na fomu yako. Sasa mimi nilitoa fomu ile siku ya kwanza kabisa kwa hiyo ikanibidi nijifanye mimi ni kati ya wanaolipia. Lahaula kumbe kuna afande mmoja anaitwa Samson slikuwa mweupe hivi anacheza handball, alikuwa ananikumbuka. Nilikuwa nimesharuhusiwa kabisa jamaa akaja akasema mimi ndio nilikuwa natafutwa nilikuja leo kesho yake nikaingia mitini. Ikabidi nipandishwe mahabusu.

Ila baadaye C1 Major Nakuchema akapita nikampa salamu zake (barua) mara nikaachiwa. Shughuli ilkawa huo kombania. Yaani mizengwe mtindo mmoja. Nikapoangwa kombania B. Huku afande Nyundo, na tukasikia kuna mtu anaitwa Basekana huyo kawaida anachukuaga likizo kabla kuruta wapywa hawajaja. Akirudi anajifanya kama pimbia kumbe anawasoma nani anajifanya mjanja nani yupo poa. Basi jamaa ana tabia ya kutembea na daftari lake limeandikwa kumbukumbu za utoro haliachi nyumbani wala ofisini maana watu walishawahi kumlaghai mke wake wakachukua dafatari wakalitumbukiza chooni.

Jamaa alikuwa na roho mbaya sana. Maana anakusainishwa hata zile siku ulizochukua pass. Kuna jamaa mmoja alishawahi kumpiga Afande Basekana mkwara akamwambia kama wewe unajiona mwanajeshi kweli nifuate kama sijakutumbua tumbo lako na hili panga, maana jamaa alikuwa ameshika panga. Afande akafyata.

Kombania A kuna afande Matata na Sahani. Huyu Sahani wanasema alikwenda vitani akarudi na silaha yake ile ile haijapotea. Alikuwa kama fyatu fulani sometimes. C coy kuna afande kibuyu. Alikuwa anapigishwa kwata huyu. Utamsikia hakikisha **** na **** vinaachana (wakati wa kwata).

Ajutant akipita na kifimbo chake anapiga blanket utasikia "vumbi" yaani anavyolipiga lazima vumbi litoke. Sometimes anasema vumbi hata kabla hajapiga blanketi. Kuna mtu alikuwa anaitwa Sakinoi jamaa alikuwa mmasai. Jamaa alikuwa na roho ngumu sana. Alishawahi kutaka kumchinja afande Matata.
Yaani jeshini kulikuwa hakuna kufikiria sana. Linalokujia fanya. Ukirudi ukisikia ulikuwa unatafutwa kwa utoro, solution ni kuingia mitini tena.

Deal ukiwa na washikaji wapishi au bakery basi either utapata pororo la nyama au utapata executive bread. Ila Ruvu kuna chatu wengi na malaria ya kumwaga. Maana wale mbu nao walikuwa kama wamajeshi. Watu kadhaa walipoteza maisha pale kwa ajili ya Malaria. Lakini tulisurvive, na sometimes tulikuwa tunatoroka usiku sijui vichwa vyetu vilikuwa vinawaza nini. Ila nilijifunza mengi sana ikiwa ni pamoja na kuwa kwenye jumuiya huwezi kujua mwenzako anawaza au anakusudia kufanya nini pia ukakamavu na kutokuwa mwoga.
 
Katika kombania yetu tulikuwa na wahindi wawili. Siku moja kwenye disco, baada ya wiki kadhaa za kukaa jeshini, mhindi mmoja akawa anatufundisha wimbo wa kihindi. Tulijifunza, lakini yule mwingine akawa anacheka sana,. Sisi tukadhani kuwa maneno ya wimbo ule yanachekesha. Kesho yake ilibainika kuwa yule Mhindi aliyetufundisha ule wimbo ametoroka. Yule mhindi aliyebaki akatuambia alikuwa anacheka sana maana maneno ya wimbo ni: Kwaherini, mimi kesho natoroka!

Hii imenifurahisha sana, Mkuu!

Wakati wa usiku kwenye disco, tukaona kundi la ma Mp linakuja usawa wa kombania. Tukajua, leeo tumepatikana. Wakaongea na kamanda wa kombania, halafu muda si mfupi wakaondoka. Baada ya wao kuondoka,kamanda akasoma majina yetu na kutuita tutoke mbele. Akautuuliza, nyie mlikuwa kwa kuku leo? Tukamuambia ndio.
Akasema safi sana, nyie askari wazuri sana, mmekamatwa, lakini mkaweza kutoroka, pamoja na mayai yenu. Huo ndio uaskari. Hatukupewa adhabu, disco likaendelea!

Huu ndio uzuri mmojawapo wa JKT.
 
Inasemekana siku moja akiwa tayari na cheo chake alikuwa akikagua mahanga toka A Coy hadi mwisho sijui ni Coy gani pale Ruvu ni ya mwisho.

Kwa kufuata mstari ulionyooka, Coy E ilikuwa ya mwisho. Mm nilikuwa Coy hiyo, ambayo ilikuwa imepakana na pori na njia ya kuelekea kwa "Babu".

Siku moja ilitoka order kuwa siku inayofuata, asubuhi, kutakuwa na Master Parade. Kuruta tulikuwa tunapata taabu sana wkt km huu. Km kawaida ya order, inatoka jioni, na wkt huo tunatoka kwenye fatigue, tumeshafuka km chokoraa! Unajitahidi kufanya usafi wa combat (jua limeshazama!) na mwili uwezavyo huku maafande wanakupa kazi km hizo - kuwapunguza nywele, kuwapigia polish buti zao, nk.

Siku ya Master Parade nilikuwa na pasi. Nikaona nikienda ktk parade, inaweza ikawa ni sbb ya kwenda mahabusa kwa kutokuwa smart. Alfajiri ya siku hiyo nikatokomea kichakani. Nilipokuwa nikienda mbele zaidi, nikakuta shimo lililokuwa linaonekana limechimbwa muda mfupi uliopita. Mara akapita babu mmoja ameshika panga, nadhani alikuwa anaelekea shambani. Nilipomuuliza khs lile shimo, akaniambia; "huyo ni nguruwe". Duuh! Nikasema moyoni: "sijui ingekuwaje ningelikutana naye?".

Wanajeshi wote walikuwa wamejiandaa walivyoweza. Walipofika ktk Master Parade, CO alisimama mbele, akaangaliaaa! Kisha akasema: "Ondokeni wote hamko smart!"
 
Kuna kruta mmoja (Msukuma) alikamatwa na Afande baada ya kuwa amejongo Disco akaletwa pale tulipokuwa tunaimba na akalazimishwa aimbe wimbo wa Taifa kwa kilugha (Kisukuma).......! Du mbona ilikuwa shughuli hadi raha, yaani tulipata burudani ya kutosha...........Wimbo wa Taifa kwa Kisukuma ni mzuri sana.

Kwa waliopita Makutopora, mnakumbuka jinsi Makruta wa kike walivyokuwa wanakuja kulala kwenye mahanga ya wanaume ili waweze kuwahi mchakamchaka alfajiri saa kumi. Hii ilikuwa ni kwa sababu Serengeti ilikuwa mbali sana, ila cha ajabu ni kwamba unashtuka usiku unaona kuna demu amelala pembeni yako wala huwazi hata swala la ngono.

For sure kilikuwa kipindi kizuri sana.
 
Wakuu nimecheka mpaka mbavu zinauma.

Jamani enzi zile haki za binadamu ilikuwa vipi? Pale Makutupora kuna makruta walikamatwa usiku wamesimamisha minazi...wakaswekwa lupango.Kesho yake, duh! MP aliwachukua akawa awakimbiza kila mahali wakiimba " sisi ni malaya wa kikosi". Kila kulipo na kundi la watu wanapitishwa wakitroti na kuimba kawimbo hako!. Baada ya hapo waliachiwa, lakini kweli walidhalilika.Likatokea bogi la kwenda Bulombora, hawakuwemo lakini wakaomba..wakaunganishwa haoooo...Bulombora.

Tulipofika tu, tulipewa tips za kuishi jeshi na maservice waliokuwa wamebaki. Mfano, mkiwa wengi na afande akaita mtu mmoja au wwawili waje...basi kauka tu...maana unweza jitolea ukakuta kuna anakuitieeni bonge la kazi. Siku moja pale combania A afande alikuwa kwenye hanga letu akachunguliwa akesema, 'watu waili waje hapa". Mimi nilikuwa tu karibu na mlango nikajua nikikauka ngoma inaweza ikawa nzito kwangu..nikaenda.

Nakumbuka jamaa mmoja aliitwa Mwinyijuma alikuwa mwisho kabisa wa hanga naye akaje..wengine wamekauka kauu! Tulipofika kwake akatumbia kachukueni mizigo yenu mnahamia kwenye kibanda cha shamba la zabibu nyeupe. Salaaaale! balaa yageuka bahati..maana tulishapewa dili hiyo kwamba huko ndiko raha zilikogunduliwa. Tuliporudi hangani jamaa wakatuuliza, vipi kwapa kazi gani? Tukajibu, kitengo cha zabibu nyeupe. Kila mtu alijilaumu kwa nini hakuenda wakati afande Hamis aliita. Walijua ni kushusha magunia ya maharage kwenye gari(maana ndi thadhari tuliyopewa).

Huko kwenye kitengo laifu ilikuwa bombaaaaaaa...kula zabibu nyeupe kwenda mbele.Kwa wasiozijua zabibu nyeupe...mmmh, ni tamu mpaka saa nyingingine vindege unaweza vikamta vinang'ang'ani.
Jamani kwa wale wa makutupora, kula nyanya mbichi mnakumbuka? Unamwagilia nyanya chini ya ulinzi mkali wa afande, akiangalia pembeni kidogo, unachokua nyanya na kupeleka direct mdomoni imeoshwa?

mmmh saa ingine unaweza lenga uliyoiona mbivu kumbe umechukua mbichi na ukaizamisha mdomoni. Kazi kuitema maana afande anaweza geuka akakuona...unameza tu.
Kombania A kulikuwa na kiafande kinaitwa Mwashamba..ebwana hiki kijamaa noma kweli. ati mchakamchaka kinakuja kutuamsha kwa kurusha mchanga kiduchu kwenye bati halafu nduki...wale watakosikia ndio haohao....kinahesabu namba na kuleta fadhaa.

Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, kwa wale wasienda JKT hawataelewa hiyo experience tuliopata....lakini ilikuwa na very exiting experience japo kwa sasa ingekuwa disaster hasa ukiangalia hili janga la Ukimwi.

Jambo afandeeee.
 
Back
Top Bottom