enzi zile makamanda hawakuwa na shule kabisa na walijitahidi kukariri maneno machache ya kingereza na kuyatumia kila mara.....nakumbuka ile adhabu ya push up!!!!!afande atakwambia ....haya...chini!down!chini!down....akimaanisha juu ..chini sasa ujifanye hujamuelewa!!!cha moto utakiona kwa kujifanya msomi!!!
ypte tisa kumi matumiz ya mustin lol!!
yaani mboga moto, ugal moto bakuli moto utakulaje utajiua wewe
kutandika kitanda jeeee....................unatandika afu usiku una opt kulala chin manake kukipatia kutandika asbh ni shidaa........
Waliita mustin ila ni mess tin, yale yale. Unakumbuka mambo ya green vest ya njano au nyekundu?
lol!!.................green vest af nyekundu
ila ukweli ukakamavu tulijifunza sana ivi wa siku hizi bado zile staili za zaman zipo?
ivi yale amteso tuliyopata bado wa siku hizi wanayapata?
Duh!! Umenikumbusha mbali, Ruvu JKT, 832KJ, 91/92 Combania C kwa sir major Chenge
Mafinga JKT 1981 sitasahau tulipopewa ng'ombe mimi na bw. Hezron Kigondo (sasa ni SACP wa Polisi Makao Makuu), kufika malishoni tukalala usingizi kwenye mti mmoja wa kivuli. Tulipoamshana hatukukuta ng'ombe hata mmoja, walitutoroka. TULIULIZANA TUTAEALEAZA NINI KIKOSINI? tuliamua twende liwalo na liwe tukiamini kwamba tutasaidiwa na kikosi kuwatafuta walipo.
Tulipowaeleza maafande acha watuhenyeshe kwa kwata mpaka tukawa mbendembende. KUMBE NG'OMBE WALIRUDI WENYEWE NA WALIKUWA KWENYE ZIZI LAO SALAMA KABISA.
Kuna jamaa alikuwa lindo na SAR, akaamua kwenda Disco na bunduki akaificha angani. Aliporudi bunduki haipo ! :confused2:
Jamaa akachukua Begi lake usiku huo huo, akaishi mpaka leo !
View attachment 247745
Daaa ezi hizo mafinga jkt tulienda kuzima moto msitu wa saohilli saa kumi tulitoka kikosini mpaka kesho yake saa 6mchana bila ya kula chochote pata picha na baridi la mufindi