Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Hebrew,

Hata nami nilisikia kuwa col. Urio alifariki. Huyu alitukuta, nasi tulimkuta col. Meena.

Mnaukumbuka wimbo wa "Malela, Malela, Malelaaa, ... Malela, Malela, Male nakutafuta!!"? Tuliambiwa kuwa Huyu Malela alikuwa ni kuruta (msichana, nadhani). Siku moja alitoka yeye na kuruta mwenzake (naye ni msichana, nikumbukavyo) kwenda kwa "Babu". Njiani walikutana na kibibi kizee ambacho kilikuwa kinauza miwa. Malela na rafikie walikuwa wanataka kununua miwa.

Kwa kuwa miwa ilikuwa michache, yule bibi akamwambia Malela akachukue miwa ndani ya kibanda cha bibi ambacho kilikuwa jirani. Malela akaenda, na akakawia sana kurudi. Baada ya yule rafikiye kumsubiri kwa muda mrefu, ikabidi amuulize yule bibi. Bibi akamwambia : "Mbona rafiki yako alishaondoka muda mrefu sana! Hukumuona! Aliondokea kule kule kibandani".

Ilipofika jioni yule rafikie Malela hakumuona Malela. Alipoulizia kwa kuruta wengine, wakamwambia kuwa walikuwa hawajamuona kwa muda mrefu. Wasiwasi ulipomzidi, aliripoti suala la kutoweka kwa Malela kwa Sir Major. Walitumwa wanajeshi wakiongozwa na rafikie Malela kwenda ktk tukio. Walipofika, walishangaa kutokuta kibanda, kinyume na alivyosimulia rafikie Malela.

Mara kwa mara, inasemekana kuwa, rafikie Malela alikuwa akimuona Malela, lkn alipowaonesha wengine, hawakumuona! Hiki ndicho kisa cha kuzuka wimbo huu.

Mmh! Sijui km ni cha kweli au la.
 
Wanataaluma mnanikumbusha mbali sana tena . . .

Nakumbuka wakati wa kwata na kunyakua, kuna afande alikuwa analala chini kabisa akidai anataka kuhakikisha kuwa miguu yote inaenda na kushuka pamoja bila kupinda.

Ilikuwa balaa . . . Kunywa uji mwendo wa kunyakua, kula mwendo wa kunyakua nk.

Jamani tunatoka mbaaaaali kweli kweli. Sijui kama watoto wetu watakuja kupata hii experience . . . .
 
Inaelekea hii mada imewakuna wengi!! Mnakumbuka afande akisema "kazi magoti, kanyagia kisigino na angalia mbele" hii ni wakati wa kwata!! Mnakumbuka mwendo wa pole!!
 
Mwanzo wa kwenda JKT:

Ni mwaka wa 1975, Jumapili. Naamka nikiwa na hangover kali baada ya kukesha Disco la Sansui pale Sea View Hotel. Nakumbuka kuwa leo ni siku ya kwenda jeshini baada ya kumaliza Mkwawa, kidato cha sita. Nachukua mfuko wangu, na kwenda Makao Makuu ya JKT, Upanga. Hapo tunapakizwa kwenye malori na kupelekwa Mgulani. Kufika tu Mgulani, foleni. Naulizwa,'Askari, kwa nini hujanyoa nywele?' Nashangaa kwa vile mimi sio askari na sijapata muda wa kunyoa Afro langu. Tunapelekwa mess, chakula ni mkate na maharage. Najaribu kula, nashindwa.

Tunapakizwa kwenye malori tena, usawa wa Ruvu. Kabla ya kuingia kambini, kuna kilima, tunashushiwa hapo. Foleni. Tunaambiwatuimbe wimbo, mchakamchaka. Mie ulimi nje. Baadae tunagawwiwa kombania, yangu F Coy. Tunapewa green vest za kijani na bukta. Wasichana wanakazana kushusha bukta zao, kwani mapaja yako wazi. Usiku disco, tunaamshwa saa tisa usiku. Unazinduka, unaamka huku bado umelala. Maisha gani haya jamani?

Baadae mchana namuuliza rafiki yangu ambaye ni service anipe mbinu za ku jongo. Ananieleza kuwa huwezi kumfundisha mtu mbinu.Unajifunza mwenyewe kutokana na mazingira yako. Baadae nagundua kuwa alisema kweli tupu.

Mikasa na matukio baada ya kujifunza mbinu za ku survive jeshini baadae.
 
Sanctus Mtsimbe,
Asante kwa kutukumbusha mbali. Kwa kweli vituko vya JKT havisahauliki hata ipite miaka kibao.
Nilikuwa Mafinga. Nakumbuka tulikuwa tunaambiwa kufanya mazoezi ya vita porini - usiku, eti kwa kuwa vita hupiganwa usiku. Tunapelekwa porini na hapo tunatahadharishwa kwamba kuna watu wanaweza kutekwa na adui. Mtu akitekwa hata kama unaona, huna ruhusa kumtetea, ila ni kusonga mbele kukabiliana na adui. Ajabu ni kwamba wanaotekwa ni wasichana tu. Wavulana hawatekwi - maajabu ya vita ya JKT!

Vita inapopamba moto tunaingia kwenye mahandaki. Raha ni pale wavulana na wasichana wanapoingia kwenye handaki moja lakini hakuna anayekumbuka mambo machafu (you know what). Unasahau kabisa kwamba uliye naye ni wa opposite sex.

Tulikuwa tunasaidia kazi mbalimbali za kambini kutegemea na profession yako. Nakumbuka watu walikuwa wanabadilisha profession kila siku. Jana alikuwa daktari wa mifugo (ng'ombe anachomwa sindano popote), leo mwalimu wa chekechea (anafundisha watoto wa maafande kwa kuwaimbisha nyimbo za disko), kesho ni seremala (ubao unarandwa hadi unaisha na kusingizia kwamba hayo ndio mahesabu aliyopanga), n.k. ili mradi siku zinapita.

All in all, JKT ilikuwa na uzuri wake. Ukitoka JKT unakuwa na uthubutu mkubwa. Unakuwa tayari kukabiliana na maisha ya aina yoyote popote! Wakati ule tuliona ni mateso makubwa lakini sasa hivi zimebaki simulizi - ni raha tupu!
 
I went to Ruvu, then Mbweni. Ruvu was tough, Mbweni shusi. Favorite Songs '' Kule kule kwa Chinova, Kule kwa Chinova...." and I really liked Sisi Tunataka kuwasha mwenge tunataka kuwasha mwenge. It is among my favorite Patriotic songs, the first one being Tanzania Tanzania nakupenda kwa Moyo wote, folowed by Tazama Ramani utaona nchi nzuri. Naupenda ubeti unaonaza na chem chem ya furaha ama nipe tumaini.
 
Jamaa mmoja alikuwa mwoga sana, anaogopa sana adhabu. Kama kawaida ya jeshi. ilikuwa ni lazima utandike kitanda vizuri kwa style ya jeshi, kila kitu, shuka, blanketi, kitanda mess tin, kwa dressing. Haya yote unatakiwa ufanye kabla hujapurukushwa kwa wito wa 'FOLEN'! Basi huyu jamaa alikuwa anatandika kitanda chake vizuri usiku tukitoka disco, halafu alikuwa analala chini! Tulikuwa tunamcheka sana, lakini baadae tukawa tunamuonea huruma.

Njemba moja alikuwa akizurura kutwa na sururu. Akiulizwa, askari unakwenda wapi, anasema ametumwa kazi na afande fulani. Tulikuwa tunamuonea huruma maana alikuwa anazurura kutwa na sururu baada ya kulala porini kama sie wengine wajongomeaji.

Tulijifunza kutomaliza kazi mapema, maana ukiripoti umemaliza kazi uliyopewa, unabambikiziwa nyingine. Tulikuwa na midomo yenye fridge, maana kama jamaa yako alikuwa zamu jikoni, akikuchotea nyama au wali kwenye mess tin, unatakiwa umeze haraka, hata kama ni vya moto kiasi gani. Ulitakiwa uwe mwizi sana, hasa wa kofia, maana kama umeibiwa kofia na hukuvaa, unapewa adhabu. Mimi nilizoea kuwaibia maafande kofia zao, maana ilikuwa ni rahisi kwao kupata nyingine.

Katika kombania yetu tulikuwa na wahindi wawili. Siku moja kwenye disco, baada ya wiki kadhaa za kukaa jeshini, mhindi mmoja akawa anatufundisha wimbo wa kihindi. Tulijifunza, lakini yule mwingine akawa anacheka sana,. Sisi tukadhani kuwa maneno ya wimbo ule yanachekesha. Kesho yake ilibainika kuwa yule Mhindi aliyetufundisha ule wimbo ametoroka. Yule mhindi aliyebaki akatuambia alikuwa anacheka sana maana maneno ya wimbo ni: Kwaherini, mimi kesho natoroka!

Siku moja kombania yetu ilikuwa zamu. Platoon yetu ikapelekwa kwa kuku. Kama kawaida, ukishafika huko unakazana kubugia kwa wingi mayai mabichi kiasi utakachoweza. Baada ya kumaliza kazi, tukachukua mengine, tukajaza kwenye mifuko ya combat. Rafiki yetu mmoja akachukua mengine akayaweka kwenye jungle hat yake, halafu akaivaa.

Tukawa tunaondoka kutoka kwa kuku, tukiwa na dhamira ya kwenda kwenye jongomeo letu msituni. Mara tukakutana na ma MP. Kitu kilichotuponza siku hiyo ni kutokuvaa vizuri. Hatukufunga kamba boot, mashati hayakufungwa vifungo nk. MP mmoja akasema, 'Askari, simama. Mbona mmevaa kama askari wa kukodiwa?' Akamuita yule jamaa aliyevaa jungle hat yenye mayai. 'We, kuja hapa, mbona umening'iniza kofia?

Njoo hapa nikuonyeshe namna ya kuvaa'!! Akashika kofia, akaishusha kwa nguvu ili aizingushe zungushe kwa nguvu kichwani. Lo, si mayai yakavunjika! Yakaanza kumwagika usoni mwa jamaa. Basi tukazingirwa tusikimbie. Tukasachiwa likapatikana karai zima la mayai. Tukapigishwa fang fang usawa wa Quarter Guard, tayari kwa kufungwa na kuwa court marshalled.

Muda huo ulikuwa mchana na chakula cha ma MP kilikuwa kimeletwa. Basi ma MPwote, isipokuwa mmoja, wakaenda kula. Ikatokea kuwa kitabu cha kuandikisha mahabusu kimejaa, MP akaenda kuchukua kingine. Wakati huo tupo kwenye baraza la Quarter Guard, bado hatujawekwa ndani. Kuona upenyo huo, tukaamua tutoroke. Mmoja wetu akakumbuka kuwa tumesahau karai letu la mayai, akalirudia, tukatokomea nalo msituni. Mchana ule tulikula vizuri sana mayai ya kuchemsha .

Wakati wa usiku kwenye disco, tukaona kundi la ma Mp linakuja usawa wa kombania. Tukajua, leeo tumepatikana. Wakaongea na kamanda wa kombania, halafu muda si mfupi wakaondoka. Baada ya wao kuondoka,kamanda akasoma majina yetu na kutuita tutoke mbele. Akautuuliza, nyie mlikuwa kwa kuku leo? Tukamuambia ndio. Akasema safi sana, nyie askari wazuri sana, mmekamatwa, lakini mkaweza kutoroka, pamoja na mayai yenu. Huo ndio uaskari. Hatukupewa adhabu, disco likaendelea!
 
Bw. Mtsimbe kwa post hii ambaya kwa kijana wa kiaka 19-25 ilikuwa mizuri sana. Miaka ya JKT ilikuwa ya viyuko vingi sana na vijana wa leo hawajui wanakosa nini.

Mimi nilikuwa Makutu pale Makao Makuu na tulikula gwaride na zoezi kali sana la kijeshi , kumbe yalikuwa maandalizi ya kumkabili Nduli.

Hata hivyo alikuwepo kijana mdogo aliitwa afande Mwiba, kijana wa darasa la saba machachari sana sijui yuko wapi sasa.

Siku moja kaniita, "Kuruta wewe mwenye green vesti ya kijani kuja hapa!"
Kabla sijajibu akaniambia ,"nipigie pushap ishirini"
Akaanza
"UP"(akimaanisha chini)
"JUU"(akimaanisha kwenda juu)
"UP"
"JUU"
Push up ya tatu nikaanza kucheka , na hapo nikapelekwa qarter guard kwa hatua zaidi.
Walah mpaka leo sijui nilikosa nini ukiacha kicheko
 
Sanctus Mtsimbe,
Sanctus,

Hii hata kule Oljoro ilikuwepo, tulikuwa tunapigishwa kwata, zoezi likanoga. Jamaa akalala kwenye vumbi kichwa juu kuhakikisha miguu yote iko sawa na inaenda juu vyakutosha. Akiamka kajaa vumbi mwili mzima.

Sijui kama hata sasa hao maafande wanajituma kwenye kazi zao kama enzi hizo.
 
Wakuu wa kaya,

Mnajua mnanivunja mbavu sana. Toka asubuhi nacheka mpaka machozi yanatoka.

I am enjoying reading every bit. I think hii Thread haitakuwa na mwisho . . . . We need to write a book.

Du, Wakuu ngoja nikanawe uso, machozi yamekuwa mengi na handkerchef haifai tena . . .
 
88/89 Nakumbuka Mafinga kulikuwa na bendi ya Kimulimuli na waimbaji mmoja alikuwa amepanga pale JC kwa jina aka Bichuka na mwingine simkumbuki jina alikuwa anapenda kuigiza nyimbo za regae -jerusalem mmojawapo. Mlay akiwa CO na major Miludi we acha tu walikuwa wanaweza kazi ikitokea kuna master parade ya CO.

siku moja Mlay akaja kukagua usafi wa maaskari hasa soksi unavua viatu, we volunteers (volvo) walikuwa wachafu jamani! siku nyingine kibao kikawageukia maafande acha warushwe vichura!
 
Jamani wale wa Buhemba Mpo?

Disco na Steel Band vipi? Wimbo kama Mario n.k.

CO alimpiga zengwe jamaa aliyetoka Ruvu na kimwana super na kila wakati anaonekana naye. Jamaa akapigwa Transfer Lwamkoma kulima pamba (EMBAKASI), binti akawekwa ofisi ya CO shughuli maalumu. Ukawa mwisho wa showdown!

Vipi some benefits? Nilienjoy sana mafunzo ya Kijeshi, Mbinu za Medani nk. Na akina dada wenye NIDO kubwa walikuwa hodari sana kwa shabahi.

Oooh, How I miss JKT! Thanks Mwl. JK Nyerere.
 
Tanzania 1,
Taarifa yako hapo yawezekana ni kweli kwasababu huko huko Ruvu JKT kulikuwa na afande mmoja aliyekuwa katoka JKT Mafinga akiwa na cheo cha Staff Sgt jina lake Afande Stuke. Huyu afande alikuwa na sauti kali sana akitoa amri mfano pale JKT Mafinga sauti yake ilisikika hadi Mafinga Seminari kiasi cha kilometa kama tano au sita hivi. Kutokana na umahili huu alihamishiwa JKT Ruvu. Na kama kawaida wakaona huyu Afande apandishwe cheo kuwa Afisa Mteule Daraja la Kwanza.

Ndipo hapo wivu wa wenzake ulipojitokeza. Inasemekana siku moja akiwa tayari na cheo chake alikuwa akikagua mahanga toka A Coy hadi mwisho sijui ni Coy gani pale Ruvu ni ya mwisho. Inasemekana alipotokea mlango wa pili ikawa moja kwa moja hadi msituni na baada ya hapo moja kwa moja kwenye magofu ya kaole akafichwa huko. Order ya kutoweka kwake ikatoka, kisha wakaona kimya Jeshi likaanza kumtafuta bila mafanikio. Baada ya miezi kama sita hivi ndugu zake wakahangaika wakapata taarifa kwamba wakienda magofu ya kaole watamkuta afande Stuke.

Wakapewa dawa wakaenda na bila ajizi wakamkuta Afande Stuke akiwa kakonda ile mbaya. Walimchukua hadi Tanga kwa mganga wao akatibiwa na kuhamishiwa kambi ya Maramba Tanga ama Mgambo JKT sina uhakika ni kambi ipi alihamishiwa kwa usalama wake. Uchawi upo sana huko majeshini. Hata huyo Malela wangekazana ndugu zake wanaweza kumuona.
 
waliokuwepo Mafinga mnakumbuka bisi zilizokuwa zinapatikana kule kwa wakata kuni na bigula la kuzima moto na la chungulia pipa?
Jibaba Bonge,
Bigula la moto kule Sao Hill ndugu yangu... yani we acha tu!
Basi Mlai alikuwe mshenzi kweli...tulikuwa tumezima moto siku 2..wakati tunaendelea mabasi ya abiria toka Songea na Mbeya yakasimamishwa..abiria wakapata kibano kuzima moto..yaani kuokoa raslimali za Taifa! walilalamika lakini wapi!

Nilijifunza, uvumilivu na uzalendo na nyimbo za kupenda Tz kuliko wakati wowote ktk maisha yangu!

Wale waliokuwa Danger Coy..1990 je mnamkumbuka Singano na Afande Sagaya?
 
RUVU C-Coy NA Mgulani! - viwandani
CO Makame Rashid - Ruvu
CO Mgulani Kanali Kabiru
Nyimbo - Canadien eeeehh kapanda mlima! ( Hiyo canadien ni raba zilizokuwa imported from Canada!)
Jeshini jamani usiombe ukiwemo.Uisikie tu na usimulie ukishatoka! Kupalilia mpunga, kutunza kuku, gwaride
Mgulani shu shi tu - kujongo jumamosi na kurudi jumapili jioni na kupenya kwenye michongoma.

kama sikosehi Cadanian vilikuwa ni vichwa vya Train vyenye speed nzuri. Hivyo mnaokimbia mchakachaka kwenye makundi inakuwa kama train inayovutwa na Canadian.
 
Jibaba Bonge,
Huyu afande Mlay alikuwa very technical kuna wakati alifanya ukaguzi wa usafi eneo la kambi hadi kwenye makazi ya askari akayakuta aliyoyakuta lakini alipokuja pale mesini akakuta mifupa kibao. Mlay akasema kuaznia cheo cha Luteni kushuka chini hadi Private kila niliyemtaja mifupa kumi na tano.

Akasema kila atakaye pata idadi hiyo foleni hapa. Basi maafande walikuja kwetu kusubiria mifupa tuliyokuwa tunamalizia kunyonya bone marrow ili aongeze idadi.
 
Back
Top Bottom