Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Bubu Msemaovyo,
Bubu Msema Hovyo, kisa chako ni kizito na kimenigusa sana . . .

I am starting to think sijui tuandike kitabu cha "VISA VYA JKT" . . . very interesting
 
umenikumbusha mlimbila huyu sisi tulikuwa tunamwita muuza sumu,kwani anaweza kukuzushia taarifa za uongo.Kusema kweli jkt ni experience nzuri sana sijui kwa nini serikali imefuta mpango huu
 
mkuu waled, umenena sana.

Hebu tupatie kidigo kumbukumbu zako . . .

mgambo nilikaa mwezi tu; kwani nilichangamkia bogi la maramba; ticket ilikuwa packet moja ya sigara-sm.

Maramba nilikuwa ikulu, kila week end tanga nyumbani; nikirudi mkate, sukari na sigara quater gurd ilikuwa kwa wengine wasikuwa na 'mm' kama hizo
 
Jamani JKT nakumbuka waliokuwa wanajifanya maselule, kina dada walikuwa wanapata C za matron, kulikuwepo pia zamu za kilinda mahanga, terms kama pororo.
 
Oh, ulikuwa Coy Eagle! Ruvu, au Buhemba? Ruvu: Uliwakuta maafande Lyimo, Medadi, Zuberi, ...? CO alikuwa nani? Maafande wengi wamefariki, akiwemo Dr Omari, adjutant Jalala (km sijakosea jina).
 
umenikumbusha mlimbila huyu sisi tulikuwa tunamwita muuza sumu,kwani anaweza kukuzushia taarifa za uongo.Kusema kweli jkt ni experience nzuri sana sijui kwa nini serikali imefuta mpango huu

Kunahitajika marekebisho mengi, hasa kudhibiti uonevu kwa wasichana/wanawake, kwani ufuska JKT ndiko kwao; na huu UKIMWI!! Sijuiii!!
 
Mmenikumbusha mbali sana.. Mimi nilukuwa Ruvu, halafu Mgulani (kwata la uhuru) halafu Mlalakuwa, miaka ya mwanzoni mwa 1990. Ruvu nilikuwa Fcoy (makondeko) na kina Afande kesi, simba, mohamed na salehe. CO alikuwa ni kanali urio (nasikia ni marehemu). Nakumbuka kulikuwa nafande mmoja alikuwa anaitwa Mizani na alikuwa mpenzi sana wa mabinti (alikuwa anawasubiri vichakani wakati wanatoroka).

Nyimbo ninazokumbuka ni kama !moto wayaka mama ..moto wayaka..wayaka wayaka", Zaina zaina..zainabu wangu usiku silali" na "canadia ee canadian ee.. (nimesahau maneno hapa). Nilifurahi sana jeshini kuliko hata shuleni (boarding).

Lidumu Jeshi La Kujenga Taifa!!
 
JF ni kiboko kwa kuibua kumbukumbu zenye mvuto. Natamani kama leo ningekutana na watu wote niliokuwa nao jeshini tungekumbushana mengi.

JKT niliipenda sana maana kruta hukulazimika kuwa na ratiba yako kichwani, hukuwa na haja ya kuwaza kwamba kesho nitafanya nini, kila kitu unaamuriwa.

Nilianzia Makutopora nikamalizia Buhemba (operation miaka 30 ya uhuru). Kwa buhemba nilikuwa c - coy. Nakumbuka baadhi ya Maafande pale Buhemba kama Lichonjo (huyu alikuwa na baiskeli ameiandika cha mtu mavi), Makarius, Mbanusi, Kabadi, Kaburu, Chacha na wengine wengi.

Vituko:

Nakumbuka siku ya ku - pass out kuna kulifanyika sherehe kikosini na kulikuwa na jamaa mmoja (kruta) alikuwa ametoka Lwamukoma, siku hiyo alikunywa mataputapu akalewa kisha alianza kutapika kiasi kwamba aliishiwa maji mwilini mpaka akawekewa drip za kuongeza maji.

Nakumbuka wakati wa musimu wa mavuno ya mahindi tulipelekwa Lwamukoma ili kusaidia, kule nilishangaa sana maji waliyokuwa wanapikia ugali, yaani maji machafu kama vile ya dimbwi na yametuama hadi yana viruwiruwi, lakini unakula ugali hadi unaenda kuburst.

Nawamiss sana rafiki zangu akina Shija, Adolf Nzihangana, Rose Kaguo, Burreta, Yasintha Rwechungura na wengine kibao.
 
Hebrew,

RUVU C-Coy NA Mgulani! - viwandani
CO Makame Rashid - Ruvu
CO Mgulani Kanali Kabiru
Nyimbo - Canadien eeeehh kapanda mlima! ( Hiyo canadien ni raba zilizokuwa imported from Canada!)
Jeshini jamani usiombe ukiwemo.Uisikie tu na usimulie ukishatoka! Kupalilia mpunga, kutunza kuku, gwaride.

Mgulani shu shi tu - kujongo jumamosi na kurudi jumapili jioni na kupenya kwenye michongoma.
 
Dr Omari nakumbuka alishushwa cheo toka Meja kuwa luteni kwa sababu ya binti mmoja hivi. Mimi nilukuwa Ruvu kipindi hiki. Jeshi lilikuwa na utamu wake!! Mgulani poa nilipiga sana kwata kwa ajili ya sherehe ya uhuru halafu Mlalakuwa freshi ila tatizo ni ku guard mara tatu kwa wiki kwa sababu ile ilikuwa ni kambi ya wagonjwa!! Wazima tulivunwa sana pale!!
 
Oljoro 85/86, watoto wa askofu Msilu mpo?

Bogi la kwenda kwa Mtono Tanga kidogo watu tufungwe baada ya kulikimbia.

Mtanzania,
Kumbe ulipangiwa Tabora? Mwaka huo mie nilikuwa nasubiri matokeo ya form 4 huku kwetu Sikonge na kaka yangu (aliyekuwa Urusi) alikuwa anasota hapo JKT Msange (Masange)- Tabora. Yeye kwa sababu alikuwa kamaliza masomo ya Automotive Engineer. pale Arusha Tech. Basi kufika pale akasema yeye ni fundi wa mashine. Wakampa kuwa msimamizi wa mashine ya kusaga mahindi. Jamaa alipomaliza akawa kashatengeneza visenti vyake, acha raha alizopata kwani ilikuwa mara kwa mara akija nyumbani kwa kisingizio cha "kaja kutengeneza chekecheo za mashine ...."

Umeandika juu ya kaka yako aliyekuwa Arusha. Pana wakati tulienda kuangalia mashindano ya kuimba kwaya za kanisa la Lutheran mkoa wa Arusha. Sisi watu wa Arusha Tech tulienda kama waangaliaji maana pamoja na kuwa na Mbanjo mdogo, hatukufua kitu. Kumbuka Mbanjo Mkubwa alikuwa ni tishio kwenye mashindano ya Taifa.

Basi ilipokuja kwaya sijui ya Monduli, akaja Mwalimu wao ambaye alikuwa anatoa macho na kuyaweka kama yana Kengeza. Watu tulicheka sana. Mtu mwingine niliyemkumbuka alikuwa ni jamaa aliyekuwa akiangalia chini kama ana aibu na ku-smile. Hiki kitendo kilifanya baada ya miaka kibao, kuja kujua kuwa kumbe alikuwa kaka yako.
 
Jamaa akaendelea ".. huyu afande alishasababisha mgomo kumbaini B watu wakakataa kula. Huyu alifanya ..... na afande unajua kuwa sisi wanaume tukilala, asubuhi tunapoamka huwa tunakuwa na MIGOGORO........" Lohhh, watu walicheka hadi wakalala na mkutano ukawa umefia hapohapo maana hata afande mwenyewe machozi yalikuwa yakitoka kwa kucheka. Mkutano ulifungwa na Sajenti Manyilizu na luteni Mohamed alijikaza kwa shida kupigiwa saluti. Alipovua tu kofia akaangua tena kicheko.

Mkuu sijakupata, unatunyima raha, kama ni blue print fafanua kwa lugha ya uungwana tuelewe.

Mtuimbe,
Duu, hii mbona inajulikana? Mwanaume wa kawaida wakati akiamka, kama damu bado inafanya kazi kawaida na yupo feet basi asubuhi akiamka mashine huwa inakuwa IMESIMAMA. Mashine hiyo wanawake hawana au niseme wanayo ila imekaa vingine.

Sasa jamaa alichokuwa akilalamika ni kuwa "mtu unaamka, na mbele yako yupo Matron, na 9 inches imesimama", unahangaika kuipoza na kuifanya ikae vizuri ndani ya chupi, kwa kweli ni STRESS kubwa sana. Hapo kumbuka kuwa kama una chupi ya VIP, unaweza kushangaa umeamka na yenyewe iko kifuani kama sindiria. Unaanza kuhaha kuitafuta ile kaptura yako na hapa Matron kakukalia kooni.
 
Hahahaha nimekumbuka mbali sana, I was in RUVU CTS enzi za Urio, Chota, jalala, nilikuwa mkuu wa kitengo cha Garage. niliwafufulia Scania lilokuwa limekufa fo so long time. Afande mmoja sebelo akanikumbuka kuwa nilikumfundisha kutengeneza magari sehemu ya Engine room Saab scania pale Pugu road. Akanidabua tukiwa tunarudi kutoka kulisha kuku. Just two days after I reported JKT. Tangu hapo Kombania wataniona wakati wa disco. Order ilitoka kwa CO. Niliyaona mengi. Mabaya na mazuri. Lakini yote yalilenga kumjenga na kumfanya mtu kuwa mkakamavu

Kama huna apetite basi jeshini unaweza kuazima apetite kutoka kwa kuruta mwenzio maana kulingana na maelekezo ya afande kukubha liyesoma Jangwani high school!! (mwanaume huyo!!) kulikuwa na kuruta wenye apetite mbilimbili.(He meang mess tin).

Kama vijana wa leo kitu walichokosa maishani ni experience ya JKT. kule kuna mizengwe, ulaghai, mbinde, uongo, kuzingiziwa, kuonewa, ujasiri,usawa,utii, amri, kejeli, uovu, mamlaka, upendeleo, ufuska, kila jema na baya unaloweza kufikiria utalikuta JKT. Hayo yote yalijiri ili kukuweka wewe kikuruti uwe mgumu! uone jinsi amabvyo ulimwengu ulivyo.

Ukiwa selule kama ni binti basi umechagua maafande wajipange ili wapate favor, Binti ukiwa mgumu basi Quater guard kila leo, adhabu zisizo na mpango haziishi. Lakini maafande wakishundwa basi wanakuacha na wanakuheshimu.. Au la Kama uko jikoni Basi PORORO kwa afande(Nakumbuka wakati mmoja master parade ya CO URIO--RIP)walidakwa maafande kibao na Vilambo!! mpka maofisa!

Nakumbuka tukiwa kuruta bado baada ya disco then MINAZI(Hapo vijana wa kiume huwasindikiza wasichana serengeti then they may kiss) Vijana wakirudi hangani basi kila mmoja anaeleza mekunywa denda lita ngapi!!

Mimi nilikuwa Danger coy( kwa Babu, mwambingu, na (kukubha-means craw)
mwambingu akiwania binti basi chakula cha jioni kula ni juhudi yako. Mtanyakua mpaka mkome!

Nakumbuka kulikuwa na jamaa waliweza kujongo kazi kwa muda wa miezi kadhaa bila afande yeyote kujua. ilitokea siku moja kukawa na kitengo 'kwa CO kutengeneza mlngo wa mbuzi' basi kila siku jamaa wana shoka , panga na msumeno kwa CO. Kumbe wanaishia Vibwende.

Kisa kingine binti mmoja alikwenda kulisha kuku, akeba mayai, basi kufika quater guard afande akaanza kukagua na kirungu akigongagonga mifukoni na katika kofia. huyo binti alipofikiwa agongwa kichwani wacha udelela wa mayai uanze kutririka kutoka kichwani!! Mie nilijifunza kunywa mayai mabichi JKT.
Another memorable ki kisa cha servicemen kutandika kitanda vizuri kumbe wamelegeza springs afande akija anadhani wako nje kumbe jamaa wanauturumua! no mchakamchaka!

Kisa cha kingine ni wapendwa tulikutana kwa muda mfupi tu kumuomba Mungu baada ya disco. badala ya kwenda Kula denda tuilkuwa tunakutana briefly kuomba. Afande mmoja alikuwa anmfuatilia mpendwa mwenzetu. Akaamua kula njama na Ma -MP wakaja wakatudaka na mashitaka ni kukutana nyakati za usiku mafichoni bila kibali kwa lengo la kupindua serikali. Mashahidi wakajitokeza wakiwa ni maafande. Mungu bariki Nilimconfront Urio na nikmweleza ukweli what happened. na alikuwa ananiamini kwani akitaka kwenda DAR basi nilikuwa naifanyia gari lake service. Akaamuru kufuta mashataka. Tukapona. JAMANI!!

It was funny and adventurous to be at Nationa service.
 
Kwa waliopita Mazengo, mnamkumbuka yule Mhindi SURI? Alikuwa na kiswahili chake cha DAKIKA TANO BAKIA. Mke wake makelele sana..... "Don't write singl, write dabl dabl..."

Huyu mzee alikuwa na watoto wawili, wa kike na wa kiume. Wahindi walivyo mafisi, nasikia mzee siku imekuja barua ikimtaka BINTI yake (aliyekuwa kasoma Mazengo High school - nafikiri ni msichana wa kwanza kuanza kusoma na wanaume huku akikaa nyumbani) aende JKT, basi mzee alipata ugonjwa wa moyo, akaanguka na AKAFA.

Binti alienda Oljoro JKT na kwa sababu alikuwa selule wa kutupwa, Maafande wakawa wanambeba huyu binti. Siku kamaliza na wakampa cheti, nasikia alilia sana na akasema, "baba uliogopa tu, mambo si magumu kiasi hicho".

Nashukuru hii story ya kuuwa mtu maana tulipokuwa JKT, tulikuwa tunasikia tu kuwa maafande walikamatana ugoni na wakauwana. Pia huyu afande Nusu Mungu. Nasikia alikuwa akijiita nusu Mungu kwa sababu anaweza kutoa uhai ila hawezi KULETA uhai. Hii inamfanya awe NUSU na si KAMILI.
Nilizosikia JKT:

- Kwa nini ST anakupa amri na wewe una-OBEY??
- Mnaenda mwagilia bustani, bustani ikikauka nyie mtakuwa IMPOSIBLE kujibu.
 
.. Au la Kama uko jikoni Basi PORORO kwa afande(Nakumbuka wakati mmoja master parade ya CO URIO--RIP)walidakwa maafande kibao na Vilambo!! mpka maofisa!

Mimi nilikuwa Danger coy( kwa Babu, mwambingu, na (kukubha-means craw)
mwambingu akiwania binti basi chakula cha jioni kula ni juhudi yako. Mtanyakua mpaka mkome!

Kumbe wanaishia Vibwende.

Maarifa,
Umenikumbusha mbali aisee. Nilikaa Mlandizi kama mwaka mmoja niki-pump maji kwenda Dar (Siku hizo NUWA). Nilipofika hapo siku moja boss wetu Mhandisi Kasiga, alikuja akatuambia tuvalie vizuri na twende kwenye sherehe ya WAFANYAKAZI wasomi kwenda kumuaga URIO. Basi sherehe ilifanyika Ruvu Secondary kwa mwalimu mkuu. Ndiyo siku nilikuja kumuona Urio. Jamaa likuwa charming wala huwezi amini kuwa ndiyo huyu mtu huwa nasikia kuwa mkorofi. Nasikia walikuwa hawapikiki na Makame. Wakati Makame anahamishiwa Mbeya na kumuacha Urio Ruvu, akasema mbele yake "... sintafuata chochote alichokuwa akifanya huyu Raia mla panya - Makonde...".

Baada ya miaka kadhaa, Makame akaitwa Dar. Wakati akienda, akaamua kwenda Ruvu kuomba mayai. Urio kuona gari zuri akauliza nani huyo, wakamwambia Makame. Akaagiza MP waende wamtimue Raia aliyevamia Kambi ya Jeshi. Kumbe kufika Dar ndiyo anapewa cheo cha Mkuu wa JKT Tanzania. Nasikia cha kwanza kufanya ni kumpigia Urio simu kuwa "nakuhamishia hapa makao makuu..." Urio nasikia akacombine haraka sana na akarudi TPDF.

Unamkumbuka yule afande (Mtu wa Mbeya) aliyekuwa akishughulikia fedha pale Ruvu? Nasikia alikuwa akizika sana makuruta fedha. Watu wakizamia pale, anawapa form wajaze kuomba fedha za nauli. Mkikatwa bogi basi fedha anatia ndani. Ukimaliza JKT na kwenda kudai fedha, anakuitia MP wakutimue kwani wee ni raia.

Huyu jamaa alikuwa TAJIRI baadaye na nasikia alikuja pata ajali na kufa kama sikosei Visiga? kama waenda Dar, akiwa ndani ya Pajero. Alikuwa akitamba kuwa kazika hadi fedha za marehemu waliokufa vitani Uganda, itakuwa nyie makuruta?
 
Kuna mwana JF yeyote aliyesoma Kigurunyembe Seconadary 1981-1984? Ningependa sana kukumbuka enzi zetu za shule, wakati Head Master akiwa Mr. Magere na Second Master Mr. Betelo!!!
 
Back
Top Bottom