Je, unajua utaratibu wa kutekeleza hukumu ya kifo? Inaweza kubadilishwa kwa Wajawazito

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
26.-(1) Pale mtu yeyote amehukumiwa kifo, hukumu hiyo itaelekeza kwamba mtu huyo anyongwe kwa kitanzi mpaka afe:

Isipokuwa kwamba, endapo mwanamke aliyehukumiwa adhabu ya kifo atakuwa mjamzito, mahakama itachunguza ukweli huo na, endapo mahakama itajiridhisha kuwa ni mjamzito adhabu itakayotolewa dhidi yake itakuwa ni kifungo cha maisha badala ya adhabu ya kifo.

(2) Adhabu ya kifo haitatamkwa au kuandikwa dhidi ya mtu yeyote ambaye, wakati wa kufanya kosa mtu huyo alikuwa chini ya umri wa miaka kumi na nane, lakini badala ya hukumu ya kifo, mahakama itamhukumu mtu huyo kuwekwa kizuizini wakati wa msamaha wa Rais, na ikiwa atahukumiwa hivyo atawajibika kuzuiwa katika sehemu hiyo na chini ya masharti ambayo Waziri mwenye dhamana juu ya mambo ya sheria atakavyoamuru, na wakati akiwa katika kizuizi hicho atahesabiwa kuwa katika uangalizi halali.

(3) Pale ambapo mtu amehukumiwa kuwekwa kizuizini wakati wa msamaha wa Rais kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2), jaji anayesimamia kesi hiyo atapeleka kwa Waziri mwenye dhamana juu ya mambo ya sheria nakala ya maandishi ya ushahidi uliochukuliwa katika mwenendo wa kesi, ikiwa na ripoti ya maandishi yaliyosainiwa na yeye na yenye mapendekezo au maoni juu ya jambo hilo kama atakavyoona inayafaa kufanya.

(4) Msimamizi Mkuu wa gereza au sehemu yoyote ambayo mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na nane amewekwa kizuizini kwa maagizo ya Waziri chini ya kifungu kidogo cha

(2), atalazimika kutayarisha ripoti ya maandishi kwa Waziri kuhusu hali, historia na tabia ya mtu huyo baada ya kumalizika kwa muda wa miaka kumi baada ya maagizo ya Waziri.

(5) Baada ya kupokea taarifa na kuifanyia kazi kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (4), Waziri anaweza kuamuru mtu huyo aliye chini ya miaka kumi na nane kuachiliwa huru au vinginevyo kushughulikiwa kwa kwa masharti ya kubakia chini ya uangalizi mahali popote au mtu yeyote na kwa kuzingatia masharti mengine yoyote kwa ajili ya kuhakikisha usalama na hali ya maisha ya mtu huyo na umma kama Waziri atakavyoona inafaa.
 
Back
Top Bottom