Je unajua nini Kuhusu wanyonya damu -Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je unajua nini Kuhusu wanyonya damu -Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Waberoya, Jan 10, 2009.

 1. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #1
  Jan 10, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JF,

  Ni hadithi au ukweli ulioshamiri miaka fulani nyuma,Kuwa kuna watu maalumu wanaitwa wanyonya damu. Wanaua watu then wanachukua damu. Kipindi fulani nilijaribu kuuliza kwa watu wa rika langu la ujana, nikagundua kuwa hali hii ilisambaa karibu mikoa yote.Nikiwa Moshi kuna mzee mmoja akanieleza operation hii ilikuwa imepata kibali cha serikali, kwa watu wauawe ili damu ziongezeke mahospitalini na alienda mbali ya hapo kwa kusema hata ubongo ulikuwa unachukuliwa ili kutengenezea madawa!

  Inawezekana ni uongo au ni ukweli, NAOMBA mtu anisaidie mwenye kujua hili swala au aliyewahi kusikia same story, au zilikuwa story tu za vijiweni tu? natamani kujua pia.

  Na je wako mpaka nyakati hizi? kama walistop ni kwa nini?

  nawasilisha!

  Waberoya
   
 2. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Walikuwa wanaitwa Mumiani.
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hata mimi wakati wa utoto nakumbuka sana hizi habari, umenikumbusha jambo lililokuwa linatutia sana hofu tukiwa tunaenda shule. Nakumbuka siku moja tukiwa tumekusanyika shuleni asubuhi (shule ya msingi na huo uvumi ulienea wakati huo sana). Likatokea gari jekundu, tulikimbia siku hiyo, kuna wanafunzi walijeruhiwa kwa kukanyagana.

  Na hilo suala la ubongo, walikuwa wanasema eti unaenda kutengenezea dawa ya "Aspirin", wakati tukiwa watoto tuliamini.

  Lakini haya yote hutokea kwa tetesi, sasa ikitokea mtu akafa kifo cha kutatanisha wakati wa hizo tetesi, ndio inaunganishwa kanyonywa damu. Lakini sina uhakika wanyonya damu wapo ama hawapo. Lakini tukiunganisha na haya matatizo ya Albino, huenda walikuwepo kwa sababu za kishirikina kama vile wachuna ngozi na janga la sasa la viungo vya Albino.
   
 4. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hizi story zilikuwepo sana- kijijini kwetu akija mtu mgeni hasa wa kutoka mjini walikuwa wanaogopwa sana, siku moja karibia mwalimu mmoja adundwe pale shuleni kwetu kuwa kaleta mnyonya damu! Duh! Lakini sidhani kama kuna mtu aliwahi kushudia mtu kauawa, sembuse kunyonywa damu.
  Kitaalam, ubongo wala damu hazitumiki kutengeneza dawa 'kwa kawaida' na serikali haiwezi kuua watu ili kuongeza damu mahospitali, hiyo itakuwa akili, matope?
  Mimi nadhani ilikuwa story tu za kutiana hofu, ama sivyo itakuwa ni mambo ya imani potofu kama ilivyo kwenye mauaji ya albino.
   
 5. nukta77

  nukta77 Member

  #5
  Jan 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi imani potofu zina misingi na machimbuko tofauti. Huwa zinaanza kama utani na baadaye zinamea na kuchukuliwa kama jambo la kweli. Hili suala la albino limezidi kipimo cha utani huo. Nakumbuka maeneo ya kwetu tulipokuwa watoto wadogo tulikuwa waoga sana kupita kwenye bonde la mto hivyo wazazi/walezi wetu walituaminisha kuwa kuwepo mbali na nyumbani nyakati za jioni ni hatari. Wakatuambia njia rahisi ya kukwepa hatari hizo ni kuhakikisha kuwa tunawahi kurejea nyumbani la sivyo tutanyonywa damu na 'Jinja' ama 'Joram' kwa ajili ya kutengeneza 'chloroquin' ama 'aspirin'. Ilitutia adabu (japo ya woga).
  I blog at nukta77
   
 6. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Waberoya,

  Nafikiri huu uvumi ulitokana na Red Cross (au Bank ya damu ya dunia?) ilipoanzisha program(s) ya uchangiaji wa damu Tanzania kwa mara ya kwanza. Kilichotokea ni kwamba, wakati hii program ilipoanza, kuna wazungu kibao wa Red cross walikuja nchini kwa ajili ya kukusanya huo mchango wa damu. Na zoezi zima lilikuwa ni la hiari. Sasa wananchi kwa kutokuelewa, wakadhani ni zoezi la lazima. Matokeo yake wazushi wakaingiza uoga miongoni mwa wanachi kwa huo msemo wa "wanyonya damu." Hivyo basi, kila gari la Red Cross lilipokuwa linapita mitaani, wananchi walikuwa wanatoka mkuki..

  Disclaimer: Huu ufafanuzi nimeuweka pamoja mwenyewe. Hakuna mahali popote niliposoma hivyo. Nilikuja kufikiria hivyo baada ya kuunganisha dots kati ya zoezi zima la uchangiaji wa damu linaloendeshwa na Red Cross na huo uvumi wa 'wanyonya damu."
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Jan 11, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280

  Nashukuru wengi kumbe mlizipata au kuwagusa moja kwa moja, hata mii naamini kuwa ni uvumi tu amabao baadaye ulipata baraka za jamii husika kuwa ni serikali. Cha ajabu ukiwauliza wazee siku hizi wanasema eti haiendelei kwa sababu ya magonjwa hususan Ukimwi!

  Inawezekana ilikuwepo lakini kishirikina zaidi. kama kuchuna ngozi, najua mbeya ilikuwepo tangu miaka mingi mpakani mwa mbeya na malawi.

  Mungu atuepushie haya mabaya nchini mwetu
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Pamoja na maelezo ya waliotangulia, nafikiri uvumi huu ulienea katika harakati ya kutafuta majibu ya kile ambacho hakikueleweka vizuri.Nakumbuka huko Lushoto kulikuwa na mzungu mmoja akiitwa Bonzon ( kitu kama hicho) nyumba yake ilionekana tofauti na za wengine, ikiwa na uwa na maua/majani ( creepers) yaliyotambaa na ukuta.Huyu na hata wengine waliokuwa na nyumba zilizozungushiwa ukuta hivyo kufanya watu wasiweze kujua kinachoendelea ndani waliitwa machinjachinja ama mumiani.Miaka ya nyuma, mauaji yasioeleweka yalipewa majibu rahisi kwa kuhusisha na wanyonya damu.
   
 9. S

  Shamu JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nilizisikia hizo habari wakati nilikuwa mdogo. Zinaweza kuwa ni habari za kweli, kwasababu wakati ule tulikuwa na serikali ya ujamaa. Hali ilikuwa mbaya sana kimaisha, kiuchumi. Inawezakana watu walikuwa wanawanyonya watu damu halafu wanawauzia red cross au wagonjwa wenye hela. Agalia sasa watu wanaua Albino ili watimize mahitaji yao. Bongo inawezakana ilitokea, True Story.
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Dada Subi KARIBU sana jamvini tupate kuhabarishana, Blogu yako inasaidia katika masuala ya Shule (Scholarships nk). Kaza buti tupate habari zaidi na Hongera. Samahaniu kwa kutoka nje ya mada...
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ndugu,
  Damu haigemwi kama tembo! Red Cross hawangeweza kununua damu kama hiyo.Elewa kuwa zoezi zima la kuchukua damu ili iweze kutumiwa na mtu mwingine si jepesi.Kuna kutambua aina/kundi la damu na pia uhifadhi wake ili isigande.
   
 12. nukta77

  nukta77 Member

  #12
  Jan 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfumwa,
  Asante kwa kunikaribisha.
  Asante pia kwa kufurahia nafasi za shule na masoko ya juu. Nitaendelea kujitahidi kuzituma kadiri nitakavyozipata.
  Shukran!
   
 13. k

  kakamiye Member

  #13
  Jan 12, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wajameni, kwa wale wa Dar-es-salaam,je mlishawahi kusikia lile la MTU KUGEUKA CHATU.Nafikiri hili lilikuwa sehemu za buguruni na lilivuma sana.
  wasalaam.
   
Loading...