Je Unajua Kwamba Kundi la Taarabu la Malindi lina Miaka 104 na Limetoa Nyimbo 3,000 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Unajua Kwamba Kundi la Taarabu la Malindi lina Miaka 104 na Limetoa Nyimbo 3,000

Discussion in 'Entertainment' started by MziziMkavu, Jun 6, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280

  [​IMG]WAHENGA walisema 'visima vya kale havifukiwi', bali ni hazina muhimu kwa jamii.

  Msemo huo unamaanisha kuwa kuwepo kwa kumbukumbu za kale kunasaidia maendeleo katika jamii, hasa kwa wanajamii kujifunza ni wapi walipotoka, walipo na wapi wanaelekea.

  Miongoni mwa mambo ya kale ambayo Tanzania haina budi kujivunia ni kundi kongwe la muziki wa taarabu la Malindi... lililoanzishwa mwaka 1905.

  Kundi hili lenye maskani yake katika visiwa vya Zanzibar lilianzishwa katika mwaka huo likijulikana kama Nadi ikwaan Safaa.

  Nassor Amour (Cholo Ganuor) ni katibu wa kundi hilo ambaye alifanya mahojiano na Nifahamishe jijini Dar es Salaam wakati kundi hilo lilipokuja kufanya onyesho moja lilokuwa limeandaliwa na kampuni ya Abbas Chezntemba Entertaiment.

  Cholo alisema kwamba kundi hilo ambalo kwa sasa lina miaka 104 limeweza kuimba taarabu halisi kwa miaka yake yote jambo ambalo wanaliona kama moja ya mafanikio yake.

  Cholo alisema kundi la Malindi katika kipindi chote cha uhai wake limeweza kutoa ajira kwa vijana wengi wa visiwani Zanzibar ambao wengine wamezeekea hapo.

  Anasema mziki huo wa taarabu asilia umeweza kukubalika pia katika nchi nyingi za Ulaya hali ambayo inachangia wao kufanya maonyesho katika nchi za mbalimbali za Bara hilo.

  Katibu huyo alisema kundi hilo limefanikiwa kutawanyika katika maeneo mengi ya Ulaya na Asia lengo likiwa ni kutoa burudani ambayo imekuwa ikikubalika zaidi.

  Cholo anasema taarabu asilia imeweza kuendelea kuheshimika hasa katika Visiwa vya Zanzibar ambapo ndipo palipoasisiwa muziki huo.

  Anaendelea kuelezea kuwa muziki wa taarabu asilia umefanikiwa katika nchi nyingi za Ulaya kutokana na ukweli kwamba upigaji wake umeweza kugusa nyoyo za wapenzi wake.

  Kiongozi huyo wa kundi alisema kundi hilo lina waimbaji nchini Ufaransa zaidi ya 50 ambao wamekuwa wakifanya maonyesho mbalimbali.

  Anasema maonyesho katika nchi hiyo yamekuwa na mafanikio kutoka na wingi watu ambao wanajitokeza kuingia bila kuhofia kiingilio.

  "Sisi tunaweza kusema kwamba soko letu lipo kubwa katika nchi za Ulaya kwani tunauza na viingilio vya kule ni vikubwa lakini wanaingia," alisema.

  Alisema katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka taarabu ambazo zinadai kuwa zinaenda na wakati jambo ambalo alilipinga kwa kusema kuwa mziki wa taarabu unaharibiwa na watu ambao amewataja kuwa wenye tamaa.

  Cholo alisema watu ambao wanajigamba kuimba taarabu hapa Tanzania kwa sasa wapo katika maslahi ya muda mfupi tofauti waimbaji wa zamani ambao walizingatia vigezo bora vya taarabu.

  Katibu huyo alisema katika kipindi cha miaka 104 wamefanikiwa kuanda zaidi ya albamu 200 ambazo zina nyimbo zaidi ya 3,000.

  Baadhi ya nyimbo ambazo zimeimbwa na kundi la Malindi ni pamoja na Raha ya Moyo wangu, Zabibu, Uwa, Cheo chako, Leo Tena na Usijigambe.

  Aidha aliwataja baadhi ya waimbaji wa kundi la Malindi kuwa Rukia Ramadhani Haji Mohamed, Yussuf Mohamed na Mwanahawa Ally.

  Alisema nyimbo hizo na albamu zimeweza kukubalika kwa kiwango cha hali ya juu hivyo kuwapa moyo wa kujiamini na kujituma zaidi.

  Akizungumzia changamoto ambazo wanakabiliana nazo ni katika kuhakikisha kuwa mziki huo wa taarabu asilia unakubalika hasa katika nchi za Afrika ambapo kunaonyesha kutawaliwa na mitindo ya kisasa.

  Cholo anasema taarabu ambayo inaimbwa kundi hilo inazingatia kuburudisha na kuelimisha jamii ambayo imewazunguka.

  Amour alisema kutokana na hali hiyo jamii ya watu wa pwani wanaposikia muziki wa taarabu asilia wanapata ujumbe ambao una manufaa kwao.

  Pia alibainisha kuwa katika nchi hii ya Tanzania yapo makundi mawili pekee ambayo yanajihusisha katika uimbaji wa taarabu asilia ambayo ni Malindi na Culture Music Club yote ya Zanzibar.

  Alisema ni vema Watanzania wakajaribu kubadilika ili kuendana na muziki ambao una ujumbe wa kutosha na kuachana na ushabiki kutoka kwa makundi mengine ambayo yanaonekana kupotosha kwa makusudi muziki huo taarabu kwa kigezo cha maslahi.

  Hilo ndilo kundi la Malindi Innardwan Safaa ambalo maskani yake yapo Zanzibar ambapo lengo lake ni kuhakikisha kuwa taarabu asilia inarudi Tanzania.

  Kundi hilo limeonyesha mfano wa kukuza na kuendeleza historia, kwani wameweza kupiga hatua kwa kujifunza na kuyaendeleza yale yote mazuri waliyoachiwa.

  Ukweli utaendelea kubakia kwamba watanzania wengi siku hizi wamekuwa wakikumbatia tamaduni za kigeni wakipuuzia utamaduni wetu.

  Hapa Tanzania suala la mambo ya kale huonekana kama ujinga na wengi wetu tunaelekeza nguvu zetu katika kuukumbatia utamaduni wa mataifa ya magharibi tukiamini huo ndio muafaka.

  Umefika wakati wa kuanza kuenzi tamaduni zetu na kuendeleza yale mazuri tuliyoachiwa.
   
Loading...