Jumong S
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 7,312
- 10,492
Hii imekuwa ni kawaida sasa. Ukiangalia nyingi ya post za ajali humu jukwaani zinatokea mwisho wa mwaka. Hebu tujaribu kujiuliza kwa nini hii inatokea.
WAZO LANGU
1.Mwisho wa mwaka, watu wengi huenda likizo na wengine hupenda tu kwenda kwa mapumziko au sababu za kimila/kiimani (mfano wachaga). Hivyo kipindi hiki ndipo makampuni mengi hufanya biashara sana na kujaza mno abiria, si ajabu kukosa tiketi ya safari kisa gari limejaa hasa sikukuu za Noeli na mwaka mpya zinapokaribia. Hivyo madereva wengi hujaza abiria, huendesha kwa kasi kuwahi biashara, hufanya kazi usiku na mchana (mf ajali ya Gari la Simiyu yetu iliyowapita askari na kusafiri mda uliozuiliwa) hivyo kupelekea ajali.
2. Kuna uhusiano unaosemwa pia, wengi wa wamiliki wa magari (na wengine) mwisho wa mwaka ndio muda wa kutoa makafara mengi.
Je, wewe una maoni gani?
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums