Je, unajua kwa nini ajali nyingi zinatokea mwisho wa mwaka hasa Desemba?

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,312
10,492
Hii imekuwa ni kawaida sasa. Ukiangalia nyingi ya post za ajali humu jukwaani zinatokea mwisho wa mwaka. Hebu tujaribu kujiuliza kwa nini hii inatokea.
WAZO LANGU
1.Mwisho wa mwaka, watu wengi huenda likizo na wengine hupenda tu kwenda kwa mapumziko au sababu za kimila/kiimani (mfano wachaga). Hivyo kipindi hiki ndipo makampuni mengi hufanya biashara sana na kujaza mno abiria, si ajabu kukosa tiketi ya safari kisa gari limejaa hasa sikukuu za Noeli na mwaka mpya zinapokaribia. Hivyo madereva wengi hujaza abiria, huendesha kwa kasi kuwahi biashara, hufanya kazi usiku na mchana (mf ajali ya Gari la Simiyu yetu iliyowapita askari na kusafiri mda uliozuiliwa) hivyo kupelekea ajali.
2. Kuna uhusiano unaosemwa pia, wengi wa wamiliki wa magari (na wengine) mwisho wa mwaka ndio muda wa kutoa makafara mengi.
Je, wewe una maoni gani?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
1. magari kukimbizana kuwah abiria nayo ni sababu,

2. mwisho wa mwaka huibuka magari mengi mabovu yasiyokuwa na vigezo sababu ya tamaa ya pesa ya wingi wa abiria, sababu kipindi hichi usafiri huwa unakuwa ni mgumu hivyo abiria nao kupanda tu kwa kukosa jinsi

3. trafiki nao hugeuza mwisho wa mwaka ni kipindi cha mavuno, magari yaliyojaza kupita kiasi na magari mabovu kuachwa yapite sababu ya sheflu10 tu.

uchawi na kafara ni mazoea yetu tu kila zikitokea ajali pasipo kuzama kwenye tatizo.
 
Maoni yangu ni kuwa: mwisho wa mwaka ni maandalizi ya kuanza mwaka mwingine,hivyo ni ngumu sana kuufikia mwaka mpya,turudi kwenye kauli ya MUNGU,anasema-mwanadamu ni nani hata ashindane na mimi? Na siku zake za kuishi hazitazidi miaka 120,na ndo maana tunaambiwa tukae tayari,maana hatuijui siku wala saa! kwa hiyo uwepo wa ajali mwisho wa mwaka ni kutimiza agano la Mungu kwa maisha ya wanawadamu,maana tumemuasi,tumejaa kiburi,pumzi inatupa viburi,kiasi cha wengine kusema hakuna MUNGU,laiti kama wanadamu tungekuwa ktk mstari ulionyoka,na kutii amri za MUNGU,sidhani kama tungekuwa watu wa kulia lia kila siku,dhambi zetu zilimfanya Mungu apunguze umri wetu wa kuishi duniani,tazama Nuhu aliishi miaka 900,ghadhabu ya MUNGU i juu yetu wanadamu,kwa ajili ya dhambi zetu,ktk biblia tena kitabu cha isaya,Mungu anasema,ole wako Damascus maana mji wako utakuwa magofu,leo tunaona yaliyopo syria,hebu kila mtu akasome Ayubu 14:1.na mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi ni chache,nazo hujaa tabu!
 
Mwisho wa mwaka pia hesabu nyingi hufungwa...so pia na hesabu za
1. Wamiliki wa mabasi
2. Wachawi
3. Wamiliki wa makanisa
4. Wanasiasa
Kada hizi huwa zibachangia sana kutoa kafara.
 
hivyo Mungu wetu akasema watu watakufa mwisho wa mwaka? Kwa maandiko gani duuhh
 
Mwisho wa mwaka pia hesabu nyingi hufungwa...so pia na hesabu za
1. Wamiliki wa mabasi
2. Wachawi
3. Wamiliki wa makanisa
4. Wanasiasa
Kada hizi huwa zibachangia sana kutoa kafara.
Hakuna mmiliki wa Kanisa, kanisa likisha anzishwa lina Board of Trustees ambao ndio wanashikilia kwa niaba ya Waumini.Jielimishe mjomba.
 
Hii imekuwa ni kawaida sasa. Ukiangalia nyingi ya post za ajali humu jukwaani zinatokea mwisho wa mwaka. Hebu tujaribu kujiuliza kwa nini hii inatokea.
WAZO LANGU
1.Mwisho wa mwaka, watu wengi huenda likizo na wengine hupenda tu kwenda kwa mapumziko au sababu za kimila/kiimani (mfano wachaga). Hivyo kipindi hiki ndipo makampuni mengi hufanya biashara sana na kujaza mno abiria, si ajabu kukosa tiketi ya safari kisa gari limejaa hasa sikukuu za Noeli na mwaka mpya zinapokaribia. Hivyo madereva wengi hujaza abiria, huendesha kwa kasi kuwahi biashara, hufanya kazi usiku na mchana (mf ajali ya Gari la Simiyu yetu iliyowapita askari na kusafiri mda uliozuiliwa) hivyo kupelekea ajali.
2. Kuna uhusiano unaosemwa pia, wengi wa wamiliki wa magari (na wengine) mwisho wa mwaka ndio muda wa kutoa makafara mengi.
Je, wewe una maoni gani?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Nadhani tukipiti takwimu, uwiano wa ajali na wingi wa vyombo vya usafiri barabarani unaweza kuwa sawa tuu na nyakati nyingine..au inaweza kukawa na ongezeko dogo.

Mwisho wa mwaka wasafiri ni wengi kuliko nyakati nyingine zote za mwaka. Hii inachangia ongezeko kubwa la vyombo vya usafiri na waendeshaji wake pia. Kwa kuzingatia Hilo pekee inaweza kuonesha chimbuko la ongezeko la ajali ukilinganisha ni nyakati nyingine za mwaka.

Lakini pia tamaa yafedha, ubakita hata magari mabovu au yenye Hitilafu yanaweza kuwekwa barabarani ambayo inaongeza hatari zaidi. Pia madereva wazuri na wazoefu nao Wanapungua kulingana na mahitaji unakuta aidha wasio wazuri au wasio na uzoefu na wanaingia barabarani. Matokeo yake ni ongezeko katika ajali.
 
Back
Top Bottom