Je unajua kinachompata mwanao kwenye School Bus?

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,674
9,994
Ni mengi mno. Wale uncles (kondaktaz) huwa wana tabia chafu sana. Vile vitoto vinavyo anza kuota matiti vimekuwa vikichezewa na kushikwashikwa maziwa na makonda hao, haswa wanapokuwa ni wa kwanza kuchukuliwa kabla ya wenzake au ni wa mwisho kurudishwa nyumbani.
Pia wavulana nao wamekuwa wakipata wakati mgumu sana kutoka kwa wahuni hao wanao jiita uncle.
Ni bora mwanao umpeleke shule mwenyewe na ukamchukue (kama una uwezo)
 
Unaweza muokoa na kondaz,ila kuna walimu shuleni na hata ndugu zako hapo nyumbani.
Bado majirani nao wamo.
OTIS.
 
Ni tatizo la kupeleka watoto kusoma shule za mbali!!
ila hili halisaidii, Ni maombi tuu na kuwa karibu na watoto wetu.

maana kote kote hakuaminiki!!
 
Ni mengi mno. Wale uncles (kondaktaz) huwa wana tabia chafu sana. Vile vitoto vinavyo anza kuota matiti vimekuwa vikichezewa na kushikwashikwa maziwa na makonda hao, haswa wanapokuwa ni wa kwanza kuchukuliwa kabla ya wenzake au ni wa mwisho kurudishwa nyumbani.
Pia wavulana nao wamekuwa wakipata wakati mgumu sana kutoka kwa wahuni hao wanao jiita uncle.
Ni bora mwanao umpeleke shule mwenyewe na ukamchukue (kama una uwezo)
aisee,hi nlikuwa siijui alafu nahisi kuna ukweli hata kama sijaudhibitisha!!sina mtoto wa hivyo ila umewapa wadau hoja nzuri sanaaa
 
katoto kamoja shuleni kila siku hana rana mwalimu akauliza - kila mwanafunzi aseme kiitu hapendi hapa duniani, katoto kakasema sipendi school bus, mwalimu kufuatilia kumbe ni wakwanza kuchukuliwa na wa mwisho kurudishwa, na ni lazima kila day koda/dereva wamfanyie mambo mabaya kale kamalaika, jamani huu ni ukweli, hivyo kila abiria achunge mzigo wake. nawasilisha.
 
Jamii inayokosa mwelekeo inakimbilia kwenye suluhisho la kufikirika zaid. Yaani suala la mmomonyoko wa maadili kwenye jamii kwa kukosa meno kwemnye sheria zetu mnakimbilia kwenye maombi>? Ndio yale yale ya mtoto hataki kula unampeleka kanisani kwenda kuombewa. Maombi hayana mipaka hatukai lakini pia tutumie na busara zetu pia. Hata busara na hekima nazo zinatoka kwa Mungu.

Mtoto kuamka saa 11 kwenda shule na kurudi saa 10 jioni wakati ana miaka chini ya kumi ni mateso makubwa! Pia jamii yetu inatakiwa kujenga utamaduni wa kukemea maovu, sheria zetu kufanya kazi zaidi (hapa suala la rushwa linaingia) na jamii ibadilike. Kasi ya mmomonyoko wa maadili kwenye jamii yetu inatisha sana!
 
Kwa hiyo unataka kusemaje? Angalizo kuhusu makonda wa school buses lipuuzwe kwavile wapo mabazazi wengi?
Ukiwa kenge huwezi kubadilika ukawa kitu kingine.
Unaweza muokoa na kondaz,ila kuna walimu shuleni na hata ndugu zako hapo nyumbani.
Bado majirani nao wamo.
OTIS.
 
jamani watoto wetu,huyo konda akigundulika apigwe kama mwizi na jambazi!
 
My gooosh!
Hili jambo lina ukweli fulani!
Nilipata kuona dalili za hii michezo kwenye gari fulani la wanafunzi!...Yaani wako tayari kumchelewesha mtoto wanayemtaka ili wabakie nae peke yake na wamtende jeuri!
Ndio maana wahindi wanaajiri madereva vibabu!...Lakini hawa barobaro ni hatari kwa afya ya mtoto!
 
inasikitisha kwa kweli
 
Kwanini wacweke konda wanawake?!,,,,

Upo kwenye mawazo yangu!
Cha msingi ni wazazi kupropose kwaumoja kwamba tunataka maskul bus yote pawepo na konda na konda wa kike, basi tatzo linakwisha,
Halafu sisi wazazi hatujui tu, wanetu wanaanza shule wakiwa na umri mdogo sana so is better wakawa chini ya uangalizi na mhudumu wa kike frm/to shule/hom coz wanawake siku zote ni caring kuliko sie midume tamaa mbele!
 
Heeee!jamani hao makonda hawaoni watu wa saizi yao mitaani mbona wapo wengi tu,kwa hao malaika wasiojua kitu wanapata raha gani kama si ushetani tu nakuharibu watoto wa watu, wenye watoto wa shule kuweni makini na kuwauliza watoto kama wanasumbuliwa na hayo mabazazi na kuchukua hatua mapema.
 
Kwanini wacweke konda wanawake?!,,,,

Angalau kuna skuli moja maeneo ya mbezi bichi, skuli basi yao inakaa na mwl mmoja wa kike mwanzo mwisho, na ada yao nafuu sana, 1.2m kwa mwaka pamoja na usafiri. Kwa maelezo zaidi ni-PM, icje kuwa natangaza biashara bure!
 
Pia wazazi tunatakiwa kuongea kwa marefu na mapana na watoto wetu na kuwaeleza kwa uwazi kabisa ulimwengu na walimwengu ndani yake jinsi vinavyokwenda na vilipofikia na pindi tupatapo taarifa za uhalifu hatua za kisheria zichukuliwe!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom