Je unajua "hili" kuhusu Tume ya Warioba?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Je Unajua: Tume ya "kukusanya" maoni ya Katiba Mpya inayoongozwa na Jaji Warioba haikulazimishwa na sheria kukubali maoni ya wananchi wengi? Yaani, hata kama wananchi wengi zaidi wangependekeza kitu fulani tume haikutakiwa kukikubali? Kimsingi SIYO tume ya KUKUSANYA maoni bali ya KUSIKILIZA MAONI. Sivyo?

Swali la kujiuliza basi ni hili: Kama Tume haikulazimishwa kuchukua maoni ya wananchi wengi na kuyafanya sehemu ya Katiba je tunaweza kusema kwa haki na dhamira safi kuwa "Katiba imetokana na Wananchi" hasa kama maoni ya Wananchi hayakuingizwa kwenye Katiba hiyo?
 
Tume ya warioba kichefuchefu,ma Dc ma rc ded hatuwataki,mawaziri tunataka wa4 tu wizara ziongozwe na makatibu ambao wawe profnal.
 
ndiyo maana tunasema hii rasimu hatuitaki tutaishi na hii katiba ya leo mpaka tutakapokuwa na nia ya dhati ya kurekebisha au kutengeneza katiba bora. haiwezekani Warioba ajifungie ndani na mkewe halafu atuletee rasimu ya katiba ambayo ilitakiwa iishie kwa familia yake tu.
 
Kwanza kabisa tume yenyewe ingeamua kwa dhati kabisa kutupatia katiba ya maana kama wangekuwa na nia dhabiti.
Hao walionufaishwa kwanza hawawezi kutoa au kutatua kero za muda mrefu zilizopo hapa nchini.
 
mmk mie kuna jambo ambalo huwa silielewi kabisa??
hivi kwani nia ya kuwa na tume ya kukusanya maoni ya katiba je ilikuwa ni kupata katiba mpya ama kupata yatakayokuwemo kwenye katiba mpya.
namanisha kwamba ni ili kujua kama wananchi wanakubali uwepo ama kutokuwepo kwa katiba mpya??
 
Asante MMM, valid and legitimate article by you.
Well, euphoria aside, it's an utter waste of national resources. You know I'm amazed with the fact it was presented with such a fuss! While it was nakedly a mere piece of drama ushered before our wet eyes by CCM [again].

Toka awali kabisa sio Kikwete wala CCM waliokuwa na nia ya dhati wala utashi wa kuandaa mchakato wa Katiba Mpya nchini. Ndio maana hata wazo la Katiba Mpya hata halikupenya ktk manifesto yao ya uchaguzi 2010. Dr. Slaa na CHADEMA walitangaza nia ya wazi kwenye Ilani yao kuwa ndani ya siku 100 mchakato wa Katiba Mpya ungeanza kama CHADEMA wangeshika dola mwaka 2010.

Kasoro kubwa (tena nyingi za kimsingi & kisheria na nyingine za makusudi) ziliwekwa/zilifanywa na CCM ili kuvuruga kitu ambacho kwa unafiki walijidai kukiamini. Huu mchakato na tunda lake LOTE ni BATILI; na utabaki batili mpaka hapo tutakapotengeneza utaratibu makini na wa dhati wa kupata Katiba Mpya ya Tanzania.
 
Je Unajua: Tume ya "kukusanya" maoni ya Katiba Mpya inayoongozwa na Jaji Warioba haikulazimishwa na sheria kukubali maoni ya wananchi wengi? Yaani, hata kama wananchi wengi zaidi wangependekeza kitu fulani tume haikutakiwa kukikubali? Kimsingi SIYO tume ya KUKUSANYA maoni bali ya KUSIKILIZA MAONI. Sivyo?

Swali la kujiuliza basi ni hili: Kama Tume haikulazimishwa kuchukua maoni ya wananchi wengi na kuyafanya sehemu ya Katiba je tunaweza kusema kwa haki na dhamira safi kuwa "Katiba imetokana na Wananchi" hasa kama maoni ya Wananchi hayakuingizwa kwenye Katiba hiyo?

Kweli, sheria haikuwalazimisha, hivyo inawezekana wamechambua waliyoona inafaa zaidi.

Ili kupima Je wananchi sasa wanajisikiaje? Imetoka kama walivyotaka? Kama wengi wana hisi hivyo basi ni maoni ya wananchi.

Pia katika kipindi hiki hatutegemei perfect contstitution
 
Pia pale ktk ukumbi wa diamond, Jk alisema suala la muungano lisijadiliwe ktk katiba mpya!
 
Kama ni hivyo hata maana yenyewe ya neno KATIBA watakuwa wameiacha.ni lazima kuwe na makubaliano ya wote watakaofungwa na katiba hiyo.sasa kama maoni si ya kwetu basi katiba hizi zote mbili hazituhusu sie,ni za Warioba na wenzie.tungeanzisha mgomo kwa kuenenda kinyume na katiba ili kufikisha ujumbe.Zanzibar waende zao,mikoa ya bara na makundi yote ya jamii kila mtu achukue chake maana hatuna kitu kinaitwa Tanzania,hakipo!ndio nasema tena Tanzania hamna kwa sababu hatujakubaliana bado kuanzisha taifa moja!si hamna katiba?basi hakuna taifa la Tanzania maana hata hii katiba ya sasa ni hao hao kina Warioba walikusanyana wenyewe Diamond Jubilee hall pale,baadae tukaambiwa kuna katiba!uhuni mtupu!
 
Kweli, sheria haikuwalazimisha, hivyo inawezekana wamechambua waliyoona inafaa zaidi.

Ili kupima Je wananchi sasa wanajisikiaje? Imetoka kama walivyotaka? Kama wengi wana hisi hivyo basi ni maoni ya wananchi.

Pia katika kipindi hiki hatutegemei perfect contstitution
Sasa walitumia fedha nyingi kupita kusikiliza maoni kwa nini kama wangeweza tu kuandika rasimu yao __halafu waone mwitikio wa wananchi ni nini?
 
Je Unajua: Tume ya "kukusanya" maoni ya Katiba Mpya inayoongozwa na Jaji Warioba haikulazimishwa na sheria kukubali maoni ya wananchi wengi? Yaani, hata kama wananchi wengi zaidi wangependekeza kitu fulani tume haikutakiwa kukikubali? Kimsingi SIYO tume ya KUKUSANYA maoni bali ya KUSIKILIZA MAONI. Sivyo?

Swali la kujiuliza basi ni hili: Kama Tume haikulazimishwa kuchukua maoni ya wananchi wengi na kuyafanya sehemu ya Katiba je tunaweza kusema kwa haki na dhamira safi kuwa "Katiba imetokana na Wananchi" hasa kama maoni ya Wananchi hayakuingizwa kwenye Katiba hiyo?
Katiba hii itakuwa haijatoka kwa wananchi.Hakuna kigezo chochote kinacho onyensha kwamba katiba hii imetoka kwa wananchi.Nothing!

This won't be a constituiton for the people and by the people.
 
mmk mie kuna jambo ambalo huwa silielewi kabisa??
hivi kwani nia ya kuwa na tume ya kukusanya maoni ya katiba je ilikuwa ni kupata katiba mpya ama kupata yatakayokuwemo kwenye katiba mpya.
namanisha kwamba ni ili kujua kama wananchi wanakubali uwepo ama kutokuwepo kwa katiba mpya??

Soma sheria ya mabadiliko ya katiba.
 
mmk mie kuna jambo ambalo huwa silielewi kabisa??
hivi kwani nia ya kuwa na tume ya kukusanya maoni ya katiba je ilikuwa ni kupata katiba mpya ama kupata yatakayokuwemo kwenye katiba mpya.
namanisha kwamba ni ili kujua kama wananchi wanakubali uwepo ama kutokuwepo kwa katiba mpya??

Swali zuri; lakini labda swali lingekuwa pia ni nani anapaswa kuandika Katiba Mpya na hiyo Katiba inatoka kwa nani? Ukifuatilia sheria inayoongoza mchakato huu utaona kuwa TUme ya Warioba ndio itaandika Katiba hii - haijalishi maoni ya wananchi. Kwa mfano, asilimia 90 ya wananchi wakisema hawataki Muungano Tume haiwezi kuliweka hilo kama pendekezo? Kwa sababu mtu mmoja (Rais) kasema hatutakiwi kujadili kuhusu uwepo wa Muungano!
 
Mzee Mwenzangu Mzee Mwanakiji swali lako ni la msingi sana, tuseme ukweli unaouma kuwa, tumezoea na kujengeka katika msingi wa kufanya mambo kwakua tu hakuna mtu atakayetuhoji. Mfano mzuri ni ule wa akina fulani waliowahi kusema kuwa hata kama tutakula Nyasi but ni Lazima Ndege ya Rais inunuliwe.....Why, simply becuase hakuna atakayeuliza na kusikilizwa na kutenda.

Imagine leo hii mambo ya msingi kabisa yanaibuliwa na Upinzani (CDM) bungeni but kwakua kwao si priority kuyachukua na wala hakuna sheria ya kuwalazimisha kuyachukua basi huyaacha hewani na kuukumbatia UPUUZI....mifano ipo mingio sana hapa lakini ndio huo UTAMADUNI-MFU wetu tuliojijengea.
 
Last edited by a moderator:
Je Unajua: Tume ya "kukusanya" maoni ya Katiba Mpya inayoongozwa na Jaji Warioba haikulazimishwa na sheria kukubali maoni ya wananchi wengi? Yaani, hata kama wananchi wengi zaidi wangependekeza kitu fulani tume haikutakiwa kukikubali? Kimsingi SIYO tume ya KUKUSANYA maoni bali ya KUSIKILIZA MAONI. Sivyo?

Swali la kujiuliza basi ni hili: Kama Tume haikulazimishwa kuchukua maoni ya wananchi wengi na kuyafanya sehemu ya Katiba je tunaweza kusema kwa haki na dhamira safi kuwa "Katiba imetokana na Wananchi" hasa kama maoni ya Wananchi hayakuingizwa kwenye Katiba hiyo?

Nimeligundua hili kutokana na msimamo wa tume kuhusu Muungano. Siamini kama kweli Watanganyika na Wazanzibar tulipendekeza Serikali tatu!!
 
Je Unajua: Tume ya "kukusanya" maoni ya Katiba Mpya inayoongozwa na Jaji Warioba haikulazimishwa na sheria kukubali maoni ya wananchi wengi? Yaani, hata kama wananchi wengi zaidi wangependekeza kitu fulani tume haikutakiwa kukikubali? Kimsingi SIYO tume ya KUKUSANYA maoni bali ya KUSIKILIZA MAONI. Sivyo?

Swali la kujiuliza basi ni hili: Kama Tume haikulazimishwa kuchukua maoni ya wananchi wengi na kuyafanya sehemu ya Katiba je tunaweza kusema kwa haki na dhamira safi kuwa "Katiba imetokana na Wananchi" hasa kama maoni ya Wananchi hayakuingizwa kwenye Katiba hiyo?

Mzee Mwanakijiji hoja gani hii tena? we ulitaka wakubali kutokana na wingi na siyo kutokana na hoja!!

Hata hivyo hapo kwa red siyo kweli, unatafuta sababu ya kuikosoa tume bure. Tunajua hii rasimu imekaba watu wengi sana, hasa waliokuwa na hidden agenda/personal interest. Sasa kila kukicha wanawaza wataanzia wapi kuikosoa tume ili kutimiza ambitions zao.

Nakutalia hapo kwa red kwa sababu mimi binafsi, nikiwa mwananchi wa kawaida nilitoa nilipendekeza mambo 9. Katika hayo ni moja tu ndo lilipigwa chini (la wakuu wa mikoa na wilaya), the rest were taken on-board. Of course, simaanishi ni mimi tu ndo niliyapendeza, ila nataka kuonyesha kuwa walikuwa wanaangalia uzito wa hoja na impact yake kwa taifa. Na hivi vingezo vinatakiwa kuzingatiwa hata huko kwenye mabaraza na kwenye bunge la katiba. Tukienda kwa idadi ya watu utashangaa hoja ya ndugai khs spika na naibu wake inapita!!!
 
Mkuu MMKJJ, maoni ni maoni tuu, mkusanyaji wa maoni, halazimishwi kufuata maoni ya wengi bali huongozwa na reasonableness ya maoni husika!.

Tume ya Nyalali, ilipokusanya maoni ile 1992, asilimia 80% ya wananchi walitaka chama kimoja kiendelee na ni asilimia less than 20% ndio waliotaka vyama vingi!. Kama tume zingefuata maoni ya wengi, where would we have been!?. Hivyo vyama vingi tulilazimisha tuu ndio wale asilimia 80% ya wakati huo wameendelea kuchagua chama kile kile!.

Kilichotoka sio katiba ni rasimu ya katiba tuu, hivyo there is ample room, tutoe maoni kuiboresha tupate japo "bora katiba!" japo tulitaka katiba nzuri, tunacholetewa ndicho hiki, lets make the best of what we get!.

Mimi msimamo wangu ni ule ule juzi, jana na leo!, "if you can't get what you want, just take what you get!", "moja shika sii kumi nenda rudi!", hii moja ndio fimbo iliyoko mkononi, ndiyo uiawayo nyoka!". Shika fimbo, uwa nyoka, shika hii moja iliyopo, ukishaimiliki, ndipo zifuate zile kumi za nenda rudi!".

Tutoe maoni, tupate katiba!, vinginevyo we'll be back to squire one!.

Pasco.
 
Mzee Mwanakijiji hoja gani hii tena? we ulitaka wakubali kutokana na wingi na siyo kutokana na hoja!!

Hata hivyo hapo kwa red siyo kweli, unatafuta sababu ya kuikosoa tume bure. Tunajua hii rasimu imekaba watu wengi sana, hasa waliokuwa na hidden agenda/personal interest. Sasa kila kukicha wanawaza wataanzia wapi kuikosoa tume ili kutimiza ambitions zao.

Nakutalia hapo kwa red kwa sababu mimi binafsi, nikiwa mwananchi wa kawaida nilitoa nilipendekeza mambo 9. Katika hayo ni moja tu ndo lilipigwa chini (la wakuu wa mikoa na wilaya), the rest were taken on-board. Of course, simaanishi ni mimi tu ndo niliyapendeza, ila nataka kuonyesha kuwa walikuwa wanaangalia uzito wa hoja na impact yake kwa taifa. Na hivi vingezo vinatakiwa kuzingatiwa hata huko kwenye mabaraza na kwenye bunge la katiba. Tukienda kwa idadi ya watu utashangaa hoja ya ndugai khs spika na naibu wake inapita!!!

sasa huoni wameacha maoni mengi ya wananchi hasa ya wakuu wa mikoa na wilaya, bado wananchi tunalia na wakuu wa mikoa na wilaya!
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom