Je unaiwakilishaje Tanzania ktk uwanda wa kimataifa?

Himawari

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
2,609
1,698
Wana JF, baadhi au wengi wetu tumeshatoka nje ya mipaka ya nchi yetu either kwa matembezi, kishule, kikazi au hata ktk makongamano, warsha, mafunzo ya muda mfupi na semina mbalimbali. Je huwa unaiwakilisha vipi Tanzania mbele ya ugani wa kimataifa?

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuhudhuria mafunzo ya kimataifa nje ya Tanzania. Yalijumuisha wataalamu toka nchi 12 duniani. Kila nchi ilipewa nafasi ya kuitambulisha nchi yake ktk muktutadha au fani zetu husika.

Wengi walitambulisha nchi zao ktk namna ya kuelimisha, kusifia na kupendeza (na mimi vile vile).
Tatizo lilikuja pale mwenzangu toka Tanzania alipokuwa naitambulisha nchi yetu ktk muktadha au fani yake.
Presentation yake ilikuwa ni ya kuiponda Tanzania..,kuwa hakuna kinachofanyika, watu (wafanyakazi) ni wazembe wala rushwa, viongozi ni mafisadi, akaenda mbali zaidi kuonyesha picha za mazingira machafu sana ktk baadhi ya sehemu za nchi yetu.., na mengine mengi yasiyofurahisha. Hakuwa na jema hata moja!!

Baadae nikamuuliza ndg yangu ina maana Tz haina mazuri ya kuitambulisha kimataifa? Akajibu kwa ukali sana.., "hiyo ndio Tanzania"!!
Kwangu mimi ilikuwa ni aibu ya kupindukia na ndio iliyonifanya nije na hili swali kwenu wana JF.., je Tz haina mazuri zaidi ya kusifika nje ya mipaka yetu??

Je, wewe unaitambulisha vipi Tanzania nje ya mipaka yetu?
 
Back
Top Bottom