Je unaishi kwenye ndoa au uhusiano wenye kukutesa? Sababu ni hii hapa..........! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je unaishi kwenye ndoa au uhusiano wenye kukutesa? Sababu ni hii hapa..........!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 23, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu ya kanuni ya mvuto, ni kwamba huwa tunavuta wenyewe kila kitu kizuri ama kibaya katika maisha yetu. Hivyo, hatuna namna ya kuukimbia ukweli huo wa kwamba sisi ndiyo tuliozisababisha hali zote tulizonazo. Kila mtu ana namna yake ambavyo suala hili limejitokeza katika maisha yake, lakini ifuatayo ni mifano ya kuelezea jambo hili.
  [​IMG]
  Uhusiano: Hili ni eneo ambapo mara nyingi watu huvuta kile wasichokihitaji, ingawa huwa hawajui kama wanafanya hivyo. Ni ngumu kukubaliana na hili hasa kama uko kwenye uhusiano usio na amani. Ni ngumu mtu kukubali kwamba aliuhitaji uhusiano huu. Ni ngumu mtu kukubali kwamba huwezi kumpata ‘mtu sahihi' kwa sababu au humhitaji ama labda hata hujui namna anavyopaswa kufanana.

  Siku zote kwa kufikiri kwetu, tunawavuta wapenzi wenye tabia tusizozipenda kuja kwetu. Tunafikiri mara nyingi kuhusu wapenzi wakorofi, kuhusu wapenzi malaya, kuhusu wapenzi wasiojiamini. Tunafikiri hivyo, kwa maana kwamba, hatuwataki. Lakini, tusichojua ni kwamba, kwa kuwapa nafasi akilini mwetu, ndiyo tunawavutia kwetu.
  [​IMG]
  Kazi: Watu wengi wamo katika kazi wasizozifurahia au hawapati kila kitu walichokitarajia. Inawezekana ni suala la kutokuipenda kazi, kutokupata pesa ya kutosha au labda kutopatana na wafanyakazi wenzake. Ukweli ni kwamba, unavuta vitu vingi ambavyo huvihitaji katika maisha yako ya kazi.

  Kwa kadiri usivyoifurahia kazi, ndivyo ambavyo unafikiria mambo mabaya kuhusu kazi hiyo. Mambo hayo mabaya maana yake unayavutia kwako na utapambana nayo, iwe unayataka au huyataki. Kumbuka, tunavuta yale tusiyotaka kuja kwetu kwa kuyafikiria sana.
  [​IMG]
  Afya: Suala hili liko wazi ingawa wengi wetu huwa hatulioni. Kama una afya njema au uzito wa ziada (kitambi), hiyo ni kwa sababu, kwa kiasi fulani unaamini kabisa kwamba unapaswa kuwa hivyo. Kitaalamu ni kwamba, unatoa mtikisiko unaoonesha kwamba una ugonjwa au wewe ni dhaifu. Hii inawezekana ni kwa sababu huamini kuwa unaweza kuishi maisha marefu na yenye afya njema. Inawezekana pia kujikubali kwako (kujiamini) ni kwa kiasi cha chini sana ingawa kwa juu wewe unajiona kuwa sawa.

  Masuala yote haya-mahusiano, kazi na afya yana namna zake za kuyasimamia ili kuepusha uvutaji wa vitu usivyovihitaji. Lakini kitu kikubwa hapa ni kwamba ni lazima ukubali kuwa unavuta vitu usivyovihitaji jambo ambalo kwa wengi ni gumu kulikubali. Fanya uchunguzi wa kina (jitafute) uone ni mambo yapi maishani mwako ambayo hayako kama wewe utakavyo, na jiulize mwenyewe maswali ukiwa na hamu pia ya kupata majibu ya kweli:
  [​IMG]
  Je, unaamini kuwa pamoja na kujiamini kwako, hustahili kupata 'mwenzi sahihi?'Unafikiri kwamba pamoja ya kuwa na maadili mazuri ya kazi, huna uwezo ama kipaji cha kupata kazi yenye mshahara mzuri au kazi ya ndoto zako? Je, unaamini kuwa unavuta uwepo wa afya njema, siha, kujiamini na kujikubali? Kumbuka, tunavuta mambo yatupatayo maishani kwa kufikiri, siyo kwa njia nyingine. Haya maswali ni mfano tu, na unaweza kujenga fikra zaidi juu ya masuala hayo.

  Jiulize kama katika mambo hayo unavuta maisha unayoyahitaji, au kama unafikiria kitu hiki lakini kinakuja kingine. Ukweli ni kwamba huwa tunavuta maisha tunayoyaishi leo. Hakuna kulogwa au njama. Ukitaka kuacha kuvuta mambo usiyoyahitaji unapaswa kuwaza kile unachotaka kuvuta. Ukitaka kuwa na uhusiano utakaodumu, uliojaa upendo, huruma na wema, unapaswa kutafuta namna ya kuzionesha hisia hizo kwa watu wengine, hata wale usiohitaji kutengeneza nao uhusiano.
  [​IMG]
  Ukitaka kazi yenye mshahara mzuri, anza kutenda kama mwajiriwa anayesitahili kazi hiyo. Usiwe tu mfanyakazi mzuri bali kuwa mtu mwenye fikra safi na mwenye ndoto halisi. Kama huna afya njema, basi anza kufanya mazoezi, kula vizuri na uanze kufikiri vizuri. Baadaye mwili wako utabadilika. Acha kulalamikia namna maisha yako yalivyo. Kuwa mtu anayestahili na avutaye aina ya maisha anayoyahitaji, na maisha hayo utayapata.

  Kumbuka sijasema kwamba, hutaugua, sijasema kwamba, hutapata matatizo kazini kwako au kwenye uhusiano. Ninachosema ni kwamba, je, hayo yanayoendelea kwenye maisha yako ndiyo unayoyahitaji? Kama siyo, mbona bado yanakuja kwako tu? Ukweli ni kwamba, kama huyahitaji, hayatakuja kwako. Siku zote utakuwa unakutana na yale unayoyahitaji kwa kuyavutia kwako kwa hiari yako mwenyewe. Bahati mbaya ni kwamba, inawezekana unayavuta ikiwa ni juhudi yako ya kuyachukia au kuyakataa. Kwa hiyo kuanzia leo, badili namna yako ya kufikiri. Anza kufikiri kuhusu yale au kile unachokitaka tu. Kama jambo hulitaki usilipe nafasi wala muda kwenye fikra zako. Kama mzaha, maisha yako yatabadilika kabisa.

  Kwani unaweza, kinachotakiwa ni kuamini na kufanya uamuzi wa kutenda hivyo.
   
 2. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Ngoja ntafakari huku naangali picha nichangia baadae
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi kaangalie hiyo movie uliyoweka hapo juu ya huyo dada aliyeshika kitabu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mr Rocky, yaani ulichoona ni picha tu ya huyo dada alioyeshika kitabu na siyo maudhui ya huu uzi.......LOL
  Ngoja naiondoa sasa hivi.......
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mtambuzi maudhui ya uzi wako wote yamo katika hiyo movie Think Like a Man na sio kwamba nimeona tuu hiyo movie mkuu nimepata na ujumbe kabisa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Michelle, njoo uone, wamekuweka kwenye picha !
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. N

  Neylu JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Baba Ngina, ujumbe wako wa leo umenigusa sana... Ubarikiwe sana kwa somo zuri...
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  unanivuta? lol
   
 9. N

  Neylu JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hahaha..... Kuna mahali popote nimesema namvuta The Boss??
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  basi hujaelewa
  usiponivuta
  utajikuta unavuta 'matatizo' shauri yako lol
   
 11. N

  Neylu JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hahahaaa.... Weye sema tuu kama mwenyewe unataka kujivutia kwangu!
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mimi huwa ninavuta vitu vizuri na vinavyonukia kwangu
  so kama una sifa hizo usishangae ukajikuta kwangu lol
   
 13. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0

  Mwali,st Ivuga hajambo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  We baba canta leo umekunywa nini,kimpumu? Unaota tu malavidavi.
   
 15. N

  Neylu JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hahahaaaaaa.... Kumbe ndio kazi yako hiyo kuvuta vuta...! Basi ndio maana najihisi kuvutwa vutwa kumbe ni wewe ndio wanivuta!!
   
 16. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Kuna watu nahisi wanatongozana hapa.
   
 17. N

  Neylu JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hivyooooo eeeh??? Hebu niambie ni kina nani hao tuwajue haraka??
   
 18. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Neilu na ze bosi.
   
 19. N

  Neylu JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hahahaaaa....... Angalia vizuri hizo hisia zako zisije zikakupeleka pabaya Bishanga... Wengine tuna wachumba humu JF usije ukatumwagia vitumbua vyetu mchanga..! Hahahaaaaa..........!!!
   
 20. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  Haya ndo mambo Kiranga ameyakemea,shauri yenu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...