Je, unaishi Dar? Una mtoto wa umri kati ya miaka 3 na 15? Mlete kwa Jakaya M. Kikwete

Sema Tanzania

JF-Expert Member
May 18, 2016
251
466
Habari WanaJF,

Sema Tanzania kwa ushirikiano mkubwa na JamiiForums, tunapenda kuwaletea taarifa hii nzuri kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam.

[HASHTAG]#SikuYaMtoto[/HASHTAG] inafanyika tena kwa mara ya pili ikiwaleta pamoja watoto zaidi ya 1,000 toka viungani mwa jiji la Dar es salaam - kucheza, kufurahi na kushindana.

Kama ilivyokuwa kwa mwaka jana, watoto zaidi ya 700 walihudhuria - na washindi walipewa zawadi. Medali na zingine nyingi. Hii ni katika kuungana na watoto kote Afrika kumuenzi mtoto wa Afrika. Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka tarehe 16 Juni - USIMKOSESHE!

Ni pale pale ktk viwanja vya Jakaya M. Kikwete Youth Park, (zamani Kidongo Chekundu).

Watoto.jpg

Je, unaishi Dar es salaam? Una mtoto wa umri kati ya miaka 3 na 15? Usimkoseshe! Watakula. Watakunywa. Watavaa.

Mwaka jana ilikuwaje? Tazama video hii fupi uone kama unastahili kukosa mwaka huu!

Pia usiache kufuatilia updates kila wakati kupitia hapa JamiiForums na kwenye Ukarasa wetu wa;
Karibuni sana.
 
Hii event ingewapa kipaumbele watoto wa mitaani na mayatima badala ya kuruhusu watu wenye uwezo wao kuwapeleka watoto wao wakapate maakuli ya bure.
Point! Lakini nadhani vituo vya watoto yatima vinaweza kujiorganize vikapeleka watoto pia. Sidhani kama inashindikana hiyo. Wafuatilie tu!
 
Mama yupi huyo mkuu? Amesema hawezi malezi?

Mama mmoja nazani ni temeke au ilala Uzi wake ulipita apa jf...alilia sana siku anajifungua mapacha wanne hawez kuwalea,..wameweja namba yake ya simu, pia ukiicheki utaona,
 
Hii event ingewapa kipaumbele watoto wa mitaani na mayatima badala ya kuruhusu watu wenye uwezo wao kuwapeleka watoto wao wakapate maakuli ya bure.
Hii event inawapa kipaumbele watoto wote wenye wazazi/walezi wenye vipato vya chini, kati na juu. Tunajichangisha fedha kuwapa hadi usafiri wa kwenda na kurudi majumbani watoto wenye wazazi wa kipato cha chini. Kumbuka watoto hawana vipato na hivyo hatuna makusudi ya kuwabagua kutokana na machimbuko yao.
 
Ingekuwa vizuri hata mikoani hili tukio lingekuwa linafanywa, hata kama kusiwe na vyakula tutabeba mihogo yetu na maji lakini watoto wataweza kujumuika na wenzao na kuienzi siku ya mtoto wa Afrika.

Maana najua serikali ikiamia Dodoma utasikia maadhimisho ni Dar na Dodoma.. tuwajali na wengine hilo ni ombi kwangu.
 
Hili ni pendekezo zuri sana - tutajipanga na wezetu wa JF kuona kama tunaweza kuanza walau katika mikoa michache. Asante kwa ushauri ndugu.
 
Naam, bila shaka wadau wenzetu kutoka humu Jamvini watahudhuria kwa wingi.
 
Back
Top Bottom