Je unaijua THE SPEAR OF DESTINY?Kile kichwa cha mkuki uliotumika kumchoma YESU ubavuni mwake???

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
9,010
28,111
Jana nilikuwa maeneo ya Kkoo kijiwe story kimoja hivi kuna jamaa amebobea sana katika masuala ya kidini hasa Ukristo alianza kuongelea kuhusu hili suala la SPEAR OF DESTINY.
Alisema kuwa ni kile kichwa cha mkuki uliotumika kumchoma YESU KRISTO pale msalabani hadi akatokwa na damu na maji.Pia alieleza kwa kifupi kuwa kitu hiki kina nguvu za asili na yoyote anaefanikiwa kuwa nayo basi anakuwa na uwezo wa kutawala ulimwengu.
Pia alisema kuwa Hitler alikuwa nayo wakati wa vita vya pili vya dunia japo alishindwa vita hivyo maana biblia ilishatabiri kuwa hakuna mwingine atakaetawala ulimwengu mzima baada ya warumi.
Pia akaeleza kuwa Inawezekana kwa sasa Marekani wanayo hii kitu ndo mana wana ACT kama superpower duniani.
Nimeileta kwenu wakuu tuweze kushare mawazo yetu na tukapata chochote kitu....
Asanteni
 
Haujachambua vyema,yamkini hauna akili na kipaji cha udadisi ama kuelezea jambo,
Ulipaswa kumuuliza mleta stori nini hasa hyo spear of destiny,ni ule mkuki ulotumika kumchoma Yesu au ni kitu tofauti,maana haijaeleweka nini nini hasa zaidi tu ya neno la kiingereza ulilotumia,
Unamaanisha nn hasa,
Kuwa ni ule mkuki wenyewe?
Km ni huo hitler aliupataje na amerika wameupataje,
Km siyo ni nn hasa hii kitu na inakuaje ihusianishwe na mkuki alochomewa Yesu
 
Holy Lance.

Hiki ni kichwa cha mkuki , ambacho alichomwa nacho YESU alipokuwa msalabani , why?

Kipindi kile walio msulubisha , walikuwa wameplani kuvunja muguu ili njia ya kuhakikisha na kuharakisha kifo cha MESIA.

Lakini walipo kuwa wakitaka kufanya hivo , wakagundua MESIA amesha kufa , so katika kuhakikisha ndio walimchoma ubavuni. Ndipo maji na damu vikatoka.

Lakini katika ulimwengu kama ujuavyo vitu vingi ni asset katika utawala wa kiroho.

So imana ikatawala kwa baadhi ya watu wanaenda kiroho kuwa, kitu kilicho weza mtoa uhai mkuu wa ulimwengu, kimeshinda nguvu yake na kina nguvu. Kwa hiyo kupitia hiko mtu unaweza tawala na ku control dunia.

Maandiko mengi pia , huzungumza kuwa ile kitu ina ocult power , na Hitler alifahamu na kutumia hizi ocult power nyingi kufanikisha na kujiunganisha na super existance beings.

Ndio maana uliona jamaa alikuwa anafanya mengi na kujua utaalamu mwingi, kama ishu Ya atomic bomb kwa wakati huo.

Kifupi Hitler hakuwa mvivu wa kutafuta maandiko na kujifunza kupitia wataalamu wake na ukipata time chunguza kuhusu alama alizo kuwa akitumia katika sehemu zake mbalimbali utaweza connect dot nyingi sana.

Nikiweza kutulia siku moja naweza andika kitu juu ya hii ishu na maana, umuhimu wa alama mzionazo na connection zake rohon.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom