Je unaijua ilani ya uchaguzi ya CCM 2005-2010? Hii hapa

MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,067
709
GONGA HAPA:

View attachment 226020

Harafu soma katiba tunayoitumia sasa ibara ya 19 na 20 kama inavyoonyesha hapa chini; je nani alithubutu kukifuta au kuhoji hata upinzani hawajui.

Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1992
Na.4 ib…
19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani
na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu
kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya
Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza
dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na
shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya
shughuli za mamlaka ya nchi.
(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike
kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na
maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo
nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
20
Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine Sheria ya 1984 Na.14 ib.6
20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria
za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani,
kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo
hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au
mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au
kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa
halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho
kutokana na Katiba au sera yake-
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-
(i) imani au kundi lolote la dini;
(ii) kundi lolote la kikabila pahala watu
watokeapo, rangi au jinsia;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya
Jamhuri ya Muungano;
(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri
 
Well noted, hapa katiba ya JMT ilikiukwa nasi twapiga makofi.
 
Ilani yenyewe ndiyo hii hapa

nb11UYSgE6AAAAAASUVORK5CYII=
 
Ukweli ndiyo huu lkn Watanzania hatujui chanzo ni nani? Rais Kikwete aliwahi kusema kuwa siyo yeye aliyevunja katiba Ilani hata yeye aliikuta ilani.
 
wakuu karibuni tena kuijadiri CCM km inafaa kuulinda umoja wetu?
 
Back
Top Bottom