Je, unaijua hotuba ya mwisho ya Sokoine? Sokoine hakutaka watu walipe kodi ambao hawana uwakilishi imara Bungeni

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Ninashangaa sana watu wanapowalinganisha baadhi ya viongozi wa zamani kama Mwalimu Nyerere na Edward Sokoine na hawa wa sasa. Ninasema hivyo kwa sababu tukianzia kwa maarifa tu tofauti zao ni kubwa sana, tukija uadilifu ndiyo wanapishana mbali kabisa.

Katika pitapita zangu za vitabu, niliwahi kupitia kitabu kidogo sana lakini adimu kinachoelezea historia kwa ufupi ya Edward Sokoine. Mwisho wa kitabu kile, ilielezewa kwa ufupi hotuba yake ya mwisho kabisa aliyowahi kuitoa, ambayo aliitoa siku moja tu kabla ya mauti, yaani April 11, 1984.

Hotuba hiyo aliitolea akiwa katika kikao cha Bunge. Kwanza alilalamika kutokuwepo kwa wawakilishi muhimu wa Wizara zilizokuwa zinajadiliwa na pia mashirika ambayo yalikuwa yanahusika moja kwa moja na mijadala hiyo, kwa hiyo akashauri na kutoa ahadi kuwa kuanzia kikao kijacho cha Bunge ni lazima wawakilishi husika wa Wizara na Mashirika ya Umma wawepo Bungeni pale mijadala inayowahusu itakapokuwa inaendelea.

Lakini mwisho wa hotuba yake alisema kitu ambacho kinamuweka mbali sana na hawa watu tunaowaita viongozi wetu wa sasa.

Sokoine alikumbushia mjadala mkali uliootokea nchini Uingereza na Marekani uliokuja kupelekea Mapinduzi ya Marekani yaliyoleta uhuru wa nchi hiyo. Mjadala ule ni pale wapiga kura na wakoloni waliokuwa wanashikilia makoloni huko Marekani walipodai kuwa si sahihi kwao kuendelea kulipa kodi kwa Uingereza, wakati hawana uwakilishi katika Bunge la Uingereza. Wakaendelea kudai kuwa sheria na maamuzi yote yanayofanywa katika Bunge la Uingereza dhidi yao ni batili.

Sokoine akasema, kama ilivyokuwa kwa Uingereza walio na Bunge la Wawakilishi kama sisi, vivyo hivyo inabidi iwe kwa Tanzania. Akasema, maamuzi yanayofanyika ndani ya Bunge la JMT, inabidi yawakilishe moja kwa moja maslahi ya walipa kodi wa nchi hii. Akasema ni jukumu la Bunge kukemea na kupambana dhidi ya ubadhilifu wa mali za umma.

Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia ukandamizaji mkubwa na uonevu dhidi ya viongozi wa siasa wa upinzani, wengi wao wakiwa wawakilishi halali wa wananchi. Imefikia hadi wengine wanapigwa risasi hadharani na kufanyiwa uonevu mwingine na udhalilishaji. Tumeona ripoti kila mwaka zinakuja na kupita bila watu kuadhibiwa za ubadhilifu mkubwa wa fedha za umma. Je, imefika wakati kwa Watanzania nao kusema, hakuna kulipa kodi mpaka pale wawakilishi wao watakapoheshimiwa na kulindwa? Mpaka pale Bunge litakapokuwa tayari kuisimamia serikali?

Swali langu kwa wale mnaopenda kulinganisha viongozi hawa wa zamani na wa sasa, ni hili. Je, viongozi wa sasa wanaelewa dhana ya 'no taxation without representation'? Wanaelewa majukumu na wajibu wa siasa za ushindani katika taifa hili ambazo zinalindwa na sheria za nchi hii? Wanaelewa misingi ya sheria na katiba ambayo kwa kiasi kikubwa hawa viongozi wa zamani walijitahidi sana kuyaheshimu?
 
Ninashangaa sana watu wanapowalinganisha baadhi ya viongozi wa zamani kama Mwalimu Nyerere na Edward Sokoine na na hawa wa sasa. Ninasema hivyo kwa sababu tukianzia kwa maarifa tu tofauti zao ni kubwa sana, tukija uadilifu ndiyo wanapishana mbali kabisa.

Katika pitapita zangu za vitabu, niliwahi kupitia kitabu kidogo sana lakini adimu kinachoelezea historia kwa ufupi ya Edward Sokoine. Mwisho wa kitabu kile, ilielezewa kwa ufupi hotuba yake ya mwisho kabisa aliyowahi kuitoa, ambayo aliitoa siku moja tu kabla ya mauti, yaani April 11, 1984.

Hotuba hiyo aliitolea akiwa katika kikao cha Bunge. Kwanza alilalamika kutokuwepo kwa wawakilishi muhimu wa Wizara zilizokuwa zinajadiliwa na pia mashirika ambayo yalikuwa yanahusika moja kwa moja na mijadala hiyo, kwa hiyo akashauri na kutoa ahadi kuwa kuanzia kikao kijacho cha Bunge ni lazima wawakilishi husika wa Wizara na Mashirika ya Umma wawepo Bungeni pale mijadala inayowahusu itakapokuwa inaendelea.

Lakini mwisho wa hotuba yake alisema kitu ambacho kinamuweka mbali sana na hawa watu tunaowaita viongozi wetu wa sasa.

Sokoine alikumbushia mjadala mkali uliootokea nchini Uingereza na Marekani uliokuja kupelekea Mapinduzi ya Marekani yaliyoleta uhuru wa nchi hiyo. Mjadala ule ni pale wapiga kura na wakoloni waliokuwa wanashikilia makoloni huko Marekani walipodai kuwa si sahihi kwao kuendelea kulipa kodi kwa Uingereza, wakati hawana uwakilishi katika Bunge la Uingereza. Wakaendelea kudai kuwa sheria na maamuzi yote yanayofanywa katika Bunge la Uingereza dhidi yao ni batili.

Sokoine akasema, kama ilivyokuwa kwa Uingereza walio na Bunge la Wawakilishi kama sisi, vivyo hivyo inabidi iwe kwa Tanzania. Akasema, maamuzi yanayofanyika ndani ya Bunge la JMT, inabidi yawakilishe moja kwa moja maslahi ya wapiga kura wa nchi hii. Akasema ni jukumu la Bunge kukemea na kupambana dhidi ya ubadhilifu wa mali za umma.

Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia ukandamizaji mkubwa na uonevu dhidi ya viongozi wa siasa wa upinzani, wengi wao wakiwa wawakilishi halali wa wananchi. Imefikia hadi wengine wanapigwa risasi hadharani na kufanyiwa uonevu mwingine na udhalilishaji. Tumeona ripoti kila mwaka zinakuja na kupita bila watu kuadhibiwa za ubadhilifu mkubwa wa fedha za umma. Je, imefika wakati kwa Watanzania nao kusema, hakuna kulipa kodi mpaka pale wawakilishi wao watakapoheshimiwa na kulindwa? Mpaka pale Bunge litakapokuwa tayari kuisimamia serikali?

Swali langu kwa wale mnaopenda kulinganisha viongozi hawa wa zamani na wa sasa, ni hili. Je, viongozi wa sasa wanaelewa dhana ya 'no taxation without representation'? Wanaelewa majukumu na wajibu wa siasa za ushindani katika taifa hili ambazo zinalindwa na sheria za nchi hii? Wanaelewa misingi ya sheria na katiba ambayo kwa kiasi kikubwa hawa viongozi wa zamani walijitahidi sana kuyaheshimu?
Yawezekana hotuba hiyo iliwakera...
 
Dhana ya uwakilishi na demokrasia ni pana na illusive,hasa kwa nchi zetu. Watawala wa leo wanachukulia uwingi wa wabunge wa ccm kama kibali cha kuhalalisha kila watutendealo bila kujali kama lina tija kwa Taifa. Uwingi umegeuka "udikteta wa wengi dhidi ya wachache". Ukiongeza na nadharia zilizothibitika kushindwa za "zidumu fikra sahihi" za kiongozi mkuu na kutohojiwa kunakoleza upogo wa maarifa ya uongozi,utashi wa kutumikia watu na kujikweza. Kamwe kizazi cha sasa cha viongozi mamboleo hakiwezi kufikia hata nusu ya hao wanaojinasibu kuwa sawa nao/kufananishwa. Wale hawakuwa na viburi,walikuwa wanashaurika,walikuwa na shauku ya kujifunza.Wa leo wanaokotwa hadi majalalani!
 
Keynez,

..kweli wewe umefuatilia hotuba ya mwisho ya Sokoine.

..kuhusu hoja ya walipa kodi vs uwakilishi, Sokoine alinukuu maneno ya Kiingereze, " No Taxation, without Representation. "

..kwa kweli umenikumbusha mbali sana.
 
Ninashangaa sana watu wanapowalinganisha baadhi ya viongozi wa zamani kama Mwalimu Nyerere na Edward Sokoine na hawa wa sasa. Ninasema hivyo kwa sababu tukianzia kwa maarifa tu tofauti zao ni kubwa sana, tukija uadilifu ndiyo wanapishana mbali kabisa.

Katika pitapita zangu za vitabu, niliwahi kupitia kitabu kidogo sana lakini adimu kinachoelezea historia kwa ufupi ya Edward Sokoine. Mwisho wa kitabu kile, ilielezewa kwa ufupi hotuba yake ya mwisho kabisa aliyowahi kuitoa, ambayo aliitoa siku moja tu kabla ya mauti, yaani April 11, 1984.

Hotuba hiyo aliitolea akiwa katika kikao cha Bunge. Kwanza alilalamika kutokuwepo kwa wawakilishi muhimu wa Wizara zilizokuwa zinajadiliwa na pia mashirika ambayo yalikuwa yanahusika moja kwa moja na mijadala hiyo, kwa hiyo akashauri na kutoa ahadi kuwa kuanzia kikao kijacho cha Bunge ni lazima wawakilishi husika wa Wizara na Mashirika ya Umma wawepo Bungeni pale mijadala inayowahusu itakapokuwa inaendelea.

Lakini mwisho wa hotuba yake alisema kitu ambacho kinamuweka mbali sana na hawa watu tunaowaita viongozi wetu wa sasa.

Sokoine alikumbushia mjadala mkali uliootokea nchini Uingereza na Marekani uliokuja kupelekea Mapinduzi ya Marekani yaliyoleta uhuru wa nchi hiyo. Mjadala ule ni pale wapiga kura na wakoloni waliokuwa wanashikilia makoloni huko Marekani walipodai kuwa si sahihi kwao kuendelea kulipa kodi kwa Uingereza, wakati hawana uwakilishi katika Bunge la Uingereza. Wakaendelea kudai kuwa sheria na maamuzi yote yanayofanywa katika Bunge la Uingereza dhidi yao ni batili.

Sokoine akasema, kama ilivyokuwa kwa Uingereza walio na Bunge la Wawakilishi kama sisi, vivyo hivyo inabidi iwe kwa Tanzania. Akasema, maamuzi yanayofanyika ndani ya Bunge la JMT, inabidi yawakilishe moja kwa moja maslahi ya walipa kodi wa nchi hii. Akasema ni jukumu la Bunge kukemea na kupambana dhidi ya ubadhilifu wa mali za umma.

Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia ukandamizaji mkubwa na uonevu dhidi ya viongozi wa siasa wa upinzani, wengi wao wakiwa wawakilishi halali wa wananchi. Imefikia hadi wengine wanapigwa risasi hadharani na kufanyiwa uonevu mwingine na udhalilishaji. Tumeona ripoti kila mwaka zinakuja na kupita bila watu kuadhibiwa za ubadhilifu mkubwa wa fedha za umma. Je, imefika wakati kwa Watanzania nao kusema, hakuna kulipa kodi mpaka pale wawakilishi wao watakapoheshimiwa na kulindwa? Mpaka pale Bunge litakapokuwa tayari kuisimamia serikali?

Swali langu kwa wale mnaopenda kulinganisha viongozi hawa wa zamani na wa sasa, ni hili. Je, viongozi wa sasa wanaelewa dhana ya 'no taxation without representation'? Wanaelewa majukumu na wajibu wa siasa za ushindani katika taifa hili ambazo zinalindwa na sheria za nchi hii? Wanaelewa misingi ya sheria na katiba ambayo kwa kiasi kikubwa hawa viongozi wa zamani walijitahidi sana kuyaheshimu?
Mkuu ni jimbo gani la uchaguzi halina mbunge wa kuliwakilisha hapa Tanzania kwa sasa? Ninavyojua, baada ya aliyekuwa mbunge Tundu Lissu "kutojulikana alipo" kwa zaidi ya miaka miwili na wapiga kura wake kutokuwa na mwakilishi Bungeni, Mh. Spika Ndugai akachukua uamuzi sahihi kabisa kama ilivyoshauriwa na Hayati Sokoine wa wananchi kutokukaa bila mwakilishi kwa kutangaza jimbo li wazi na sasa wana Iramba Mashariki wanawakilishwa vyema na Mh. Mtaturu (CCM) huku Lissu akiwa amelowea ughaibuni.
 
Sitakujibu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom